Jiji la Arusha katika kashfa nzito, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia matatani

MKURUGENZI wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia ameingia matatani baada ya kujiidhinishia lita 1900 za mafuta kwa ajili ya matumizi ya gari lake ndani mwezi mmoja kinyume cha kanuni,taratibu na sheria za zinazosimamia serikali za mitaa.

Katika bajeti ya Jiji la Arusha Mkurugenzi wake ametengewa lita 70 kwa wiki ambayo ni sawa na lita 280-300 kwa mwezi.

Nyaraka zilizofikia gazeti hili kutoka ndani ya Jiji la Arusha zinadai kuwa Agusti 30 mwaka huu kupitia Afisa Usafirishaji wake Edward J. Mwaliko aliandika dokezo sabili ya kuomba lita 900 za mafuta kwa ajili ya ofisi ya Mkurugenzi kwa mwezi Septemba.

Katika dokezo hilo Kihamia ametia saini Septemba 1 akisisitiza Afisa Manunuzi wa Jiji kushughulikia na kuidhinisha manunuzi ya lita hizo 900 kwa thamani ya shilingi 1,705,500.

Katika dokezo lingine la siku hiyo hiyo ya August 30 kupitia kwa Afisa Usafirishaji Kihamia aliaomba kuidhinishiwa lita 1000 za mafuta ya Dizeli kwa ajili ya matumizi ya ofisi yake.

Dokezo hilo lenye kichwa habari Maombi ya mafuta ya dharura nje ya GPSA (wakala wa huduma za manunuzi serikalini) anaandika kuwa:Ninaomba idhini ya kununua mafuta ya dharura nje ya GPSA lita 1000 (Diesel) kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Mkurugenzi.

Habari zinadai kuwa mafuta hayo yalinunuliwa kampuni binafsi ambayo ina kituo maarufu cha mafuta kilichopo katikati ya mji wa Arusha.( jina linahifadhiwa kwa sasa)

Hata hivyo juu ya dokezo Afisa Manunuzi wa Jiji alimshauri mkurugenzi huyo kuwa kwa mujibu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011(PPA.07, 5.50, kanuni ya 130 (1)na GN:446 inataka kufanya manunuzi yetu kupitia kwa wakala wa serikali wa mafuta (GPSA) kwanza kabla ya kwenda kununua kampuni binafsi na kushauri kuwa wafuate taratibu huo.

Akijibu hoja ya Afisa Manunuzi Kihamia alindika tena juu ya dokezo hilo kwa kusisitiza Afisa Manunuzi kutekeleza manunuzi hayo kwa kuwa ni dharura (emergency).

Akijibu hoja hiyo Afisa Manunuzi alimwagiza msaidizi wake kutafuta bei ya kituo hicho binafsi na serikali ili kufanya uwiano .Fedha za kituo hicho zililipwa katikati ya wiki hii kwa njia ya TISS

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Jiji zinasema mafuta hayo ni mengi sana kwa matumizi ya gari la Mkurugenzi kwani hesabu zinaonyesha kuwa kwa gari analotumia linaweza kusafiri umbali zaidi ya kilomita 15,000.

“Hiyo ni sawa na umbali kutoka Captown nchini Afrika ya Kusini hadi Cairo nchini Misri ambayo ni kilomita 12,000 na mafuta yakabaki kwenye gari kwa ziada ya kilomita 3,000”alieleza moja wataalamu wa Jiji.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuwa tangu Mkurugenzi huyu kuteuliwa kumekuwa na matumizi mabaya kwa kuhudumia ofisi ya mkuu wa wilaya(DC) na ofisis ya mkuu wa mkoa (RC) kwenye mafuta ya ziara za viongozi hao ,hata kuwalipia posho wasaidizi wao na polisi wawapo ziarani ndani ya jiji ambazo hazinauhusiano na shughuli rasmi za Halmashauri,pia kulipia tume zinazoundwa na wateule hao Rais.

Uswahiba wa mkurugenzi huyu na RC ndio umemponza hata kuingia kwenye kashfa nzito ya kuagiza mafuta yasiyoelezeka.Kumbuka Jiji la Arusha haina uhaba wowote wa mafuta na hata kutaka mafuta ya dharura lakini kinyume chake ni kuhudumia ofisi zingine.
Kama aliyatoa kwa ajili ya DC au RC hakuna tatizo. Ni matumizi sahihi.

Ulichopaswa kuandika mtoa hoja ni kwamba DED ametoa mafuta kwa DC na RC, basi.
 
Ngoja nkusaidie kukupa elimu .Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa wilaya wana bajeti yao. Ofisi ya Meya wana bajeti alichokifanya Mkuregenzi amevunja sheria kuingilia majukumu ambayo yapo nje ya uwezo wake kisheria wakati Waziri wa Tamisemi Simbachawene alipiga marufuku wakuregenzi kuingilia mambo yapo nje uwezo wao kisheria.
 
Kweli w
Kama aliyatoa kwa ajili ya DC au RC hakuna tatizo. Ni matumizi sahihi.

Ulichopaswa kuandika mtoa hoja ni kwamba DED ametoa mafuta kwa DC na RC, basi.
watz tuna ubongo kama wa chura,wewe unaambiwa huyu jamaa ni mwizi.JPM aamuru alamatwe Mara moja akanyee debe ndio ataacha kuiba
 
MKURUGENZI wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia ameingia matatani baada ya kujiidhinishia lita 1900 za mafuta kwa ajili ya matumizi ya gari lake ndani mwezi mmoja kinyume cha kanuni,taratibu na sheria za zinazosimamia serikali za mitaa.

Katika bajeti ya Jiji la Arusha Mkurugenzi wake ametengewa lita 70 kwa wiki ambayo ni sawa na lita 280-300 kwa mwezi.

Nyaraka zilizofikia gazeti hili kutoka ndani ya Jiji la Arusha zinadai kuwa Agusti 30 mwaka huu kupitia Afisa Usafirishaji wake Edward J. Mwaliko aliandika dokezo sabili ya kuomba lita 900 za mafuta kwa ajili ya ofisi ya Mkurugenzi kwa mwezi Septemba.

Katika dokezo hilo Kihamia ametia saini Septemba 1 akisisitiza Afisa Manunuzi wa Jiji kushughulikia na kuidhinisha manunuzi ya lita hizo 900 kwa thamani ya shilingi 1,705,500.

Katika dokezo lingine la siku hiyo hiyo ya August 30 kupitia kwa Afisa Usafirishaji Kihamia aliaomba kuidhinishiwa lita 1000 za mafuta ya Dizeli kwa ajili ya matumizi ya ofisi yake.

Dokezo hilo lenye kichwa habari Maombi ya mafuta ya dharura nje ya GPSA (wakala wa huduma za manunuzi serikalini) anaandika kuwa:Ninaomba idhini ya kununua mafuta ya dharura nje ya GPSA lita 1000 (Diesel) kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Mkurugenzi.

Habari zinadai kuwa mafuta hayo yalinunuliwa kampuni binafsi ambayo ina kituo maarufu cha mafuta kilichopo katikati ya mji wa Arusha.( jina linahifadhiwa kwa sasa)

Hata hivyo juu ya dokezo Afisa Manunuzi wa Jiji alimshauri mkurugenzi huyo kuwa kwa mujibu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011(PPA.07, 5.50, kanuni ya 130 (1)na GN:446 inataka kufanya manunuzi yetu kupitia kwa wakala wa serikali wa mafuta (GPSA) kwanza kabla ya kwenda kununua kampuni binafsi na kushauri kuwa wafuate taratibu huo.

Akijibu hoja ya Afisa Manunuzi Kihamia alindika tena juu ya dokezo hilo kwa kusisitiza Afisa Manunuzi kutekeleza manunuzi hayo kwa kuwa ni dharura (emergency).

Akijibu hoja hiyo Afisa Manunuzi alimwagiza msaidizi wake kutafuta bei ya kituo hicho binafsi na serikali ili kufanya uwiano .Fedha za kituo hicho zililipwa katikati ya wiki hii kwa njia ya TISS

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Jiji zinasema mafuta hayo ni mengi sana kwa matumizi ya gari la Mkurugenzi kwani hesabu zinaonyesha kuwa kwa gari analotumia linaweza kusafiri umbali zaidi ya kilomita 15,000.

“Hiyo ni sawa na umbali kutoka Captown nchini Afrika ya Kusini hadi Cairo nchini Misri ambayo ni kilomita 12,000 na mafuta yakabaki kwenye gari kwa ziada ya kilomita 3,000”alieleza moja wataalamu wa Jiji.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuwa tangu Mkurugenzi huyu kuteuliwa kumekuwa na matumizi mabaya kwa kuhudumia ofisi ya mkuu wa wilaya(DC) na ofisis ya mkuu wa mkoa (RC) kwenye mafuta ya ziara za viongozi hao ,hata kuwalipia posho wasaidizi wao na polisi wawapo ziarani ndani ya jiji ambazo hazinauhusiano na shughuli rasmi za Halmashauri,pia kulipia tume zinazoundwa na wateule hao Rais.

Uswahiba wa mkurugenzi huyu na RC ndio umemponza hata kuingia kwenye kashfa nzito ya kuagiza mafuta yasiyoelezeka.Kumbuka Jiji la Arusha haina uhaba wowote wa mafuta na hata kutaka mafuta ya dharura lakini kinyume chake ni kuhudumia ofisi zingine.

Kweli tabia ni kama kidonda kuacha ngumu kwelikweli nauhakika hawa na mwenzake mkuu wa mkoa hapo hawatadumu Muhongo alipambana, Mary Chitanda alipambana wote wameondoka sijui hata wameishia wapi especially Muhongo yule mama nadhani yuko back benches na wenzake kule Dodoma bungeni pamoja na kujitoa kwake muhanga kukitetea chama hapo Arusha, muda utaongea
 
Wacheni propaganda za kuchafuana wakuu. Najuwa Halmashauri imebanwa mambo mengi kwa sasa madiwani wanamsukia zengwe ionekane Mkurugenzi ni tatizo. Mambo huwa hayaendi hivyo.
Na ukikaa na imani hiyo hutokaa uelewe lolote kwa undani ,wakati mwingi ujinga huwa unasaidia.
 
Wacheni propaganda za kuchafuana wakuu. Najuwa Halmashauri imebanwa mambo mengi kwa sasa madiwani wanamsukia zengwe ionekane Mkurugenzi ni tatizo. Mambo huwa hayaendi hivyo.

Kiongozi mm nadhani hamna cha zengwe wala nini unaposema, dharura ni kuwa kuna nini, mleta mada kaleta hoja na vithibitisho ni jukumu la wao kutoa ufafanuzi imekuwaje hii na ndio maana hata afisa manunuzi alikuwa na hofu na maamuzi ya mkurugenzi
 
Kote huko upinzani umetamalaki! Huwezi tofautisha upinzani na ufisadi!

Wewe ni wale wanaofafanisha kifo na usingizi imekula kwenu hata za tetemeko mnapiga kweli sitamsahau mwenyekiti mstaafu aliposema ndani ya chama kuna ma..........................i
upload_2016-10-4_23-20-52.png
 
Wacheni propaganda za kuchafuana wakuu. Najuwa Halmashauri imebanwa mambo mengi kwa sasa madiwani wanamsukia zengwe ionekane Mkurugenzi ni tatizo. Mambo huwa hayaendi hivyo.
Unalalamika bila kuleta data zako kuonesha kwamba kweli zengwe... Jifunzen kwenye nyeupe kuita nyeupe... Nchi yetu wote hii... Mungu anawaona na atawaumbua sana serious unatetea hapo daaah inauma kweli... Mungu wetu wote..
 
Arusha acheni majungu
mbona lita 1900 kwa Mkurugenzi ni chache
ina maana ofisi nzima ina gari moja tu
jueni maana ya ofisi ya Mkurugenzi ni kwamba anabeba mpaka mafuta ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa bado posho na dharura za wageni km ujio wa Serikali, Mwenge nk
Tangu hile account nyingine ifunguliwe kagera sasa hivi siamini mtu.Hayo mafuta ni mengi sana kama ni kweli.
 
Naona madiwani nao wameamua kumwaga mboga

Hii ni TIT4TAT!
Huyu Mkurugenzi ameingia kwene 18 za Madiwani wa CHADEMA na LAZIMA AISOME NAMBA. Kwa taariifa tu hili halitaishia kwa CD tu lazima na hao walionunuliwa Mafuta kwa maana ya RC Mrisho Gambo na DC wake! Yote hii ni matokeo ya kutaka kukomoa Wapinzani!!!!
CD Arusha ameingia kwa mbwembwe kwa kuanza kubadilisha kanuni za malipo ya Meya na Madiwani na hili limeleta sintofahamu nchi nzima.
Naomba Mhe. Lema ukishirikiana na Madiwani wa CHADEMA simamieni hilo ili kukomesha uhuni wa HAWA WATEULE WA JPM wanaojifanya miungu wadogo!
 
Na hapo ndio mjue faida ya jiji kuwa chini ya upinzani.....

Wangelikuwa wale magamba wenzangu sizani kama tungezipata hizi.......

Huyu akilala hatoamka.......

Akiamka atolala........

Hivi kuna vidagaa bado wanacheza na huyu mzinza wa magogoni ......

Angalau ingekuwa sangara
Yaani mzinza wa magogoni anaweza kumwadhibu kwa kosa dogo kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom