Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,316
- 24,183
Tumesikia sasa kitambo ati kampuni za simu zinaweza kukukopesha kwa kupitia simu yako. Hakuna dhamana wala vurugu za kuomba mkopo. Na mkopo huo unaingiziwa katika akaunti yako kama X-Pesa.
Tatizo liko hapa:
Ukikopeshwa shilingi 100, riba yake ni 18% hadi 25% ambazo muda wa malipo ni WIKI MBILI au kipindi kifupi sana. Yaani ukikopa Tsh 100, kama riba ni 25% basi baada ya wiki mbili unalipa 125. Au ukikopa 100,000, baada ya wiki mbiki unalipa 125,000.
Hii ni principle ya mapapa wa kukopesha yaani LOAN SHARKS. Ni wizi wa mchana, daylight robbery!
Kulingana na gazeti la The Guardian-The Banker, la leo 5/10/2017, watuhumiwa waliotajwa ni TigoPesa na AirTel Money(Timiza). Benki Kuu(BOT) na FCC-Fair Competitions Commision wamesha sema shughuli hizo za "kibenki" hazijakaa sawa wateja wajihadhari sana na miradi hiyo za mitandao hiyo.
Kwa kufikiria tu, ni biashara ipi mtu unaweza kufanya ukakopa laki(100,000) , ukarudisha laki na ishirini na tano(125,000) na bado ukapata faida juu pamoja kulipia gharama za biashara!
Tuwe macho wajameni!
Kwa hiyo wateja wa huduma hizo shitukeni!