Jihadharini na gari number t655 aqw kwa kupora mikoba

Ni bora ukaenda kuripoti police..... hata leo nenda. JF members naomba tuwe makini kuchangia post za namna hii kwani kichaa yeyote anaweza kutoa numba za gari lolote na kudai chochote. Pengine ana kisasi na mmiliki wa gari au jambo jingine lolote. Mkuu nenda police natumaini utapata msaada.
Thanx. Sio kichaa tu, wanaweza kuwa na ugomvi wao mtu akaamua kumfanyizia mwenzake ikawa shida sana.
 
Unatakiwa kwenda kutoa report polisi hata kama kesi ni ya siku nyingi!

Hii itasaidia kufuatilia kuanzia TRA na watajua hilo gari ni la nani na watawakamata hao jamaa.

Bado hujachelewa, nenda katoe taarifa polisi, kesi za namna hii Dar zimekuwa nyingi sana, na polisi wanashindwa kufuatilia kwasababu hatutoi taarifa muhimu kama hizi

Nahisi tabu si kuripoti polisi... tabu ni kwamba polisi wetu watachukua maelezo na hatutaona matokeo...! La muhimu ni kuwa katika mazingira salama hasa ukiwa na vitu vyako muhimu!
 
Pole sana muzachai,

Mimi najua uchungu ulioupata na naamini ni kweli kuwa walijaribu kukupora. Hii ni aina mpya ya wizi hapa mjini. Mimi ilinikuta mwezi August ama Julai mwaka jana siku ya jumapili saa kumi na moja na robo alfajiri. Nikiwa namsindikiza binamu yangu aliyekuwa anapanda basi kuelekea kanda ya ziwa pale “Millenium Park” katika ofisi za Mohamed Trans nilipaki gari aina ya Escudo, nikashuka kumsaidia mgeni wangu kubeba mizigo yake, hadi kwenye basi ndani.

Ilinichukua kama dakika tatu nikarudi kuchukua begi lingine lililobaki hapo ndipo nikaona mtu anatoka katika gari langu na kuanza kutimua mbio akiwa na begi, moja kwa moja nikajua ni mwizi, nikamkimbiza hadi kwenye gari lao kama hatua kumi hivi toka nilipopaki langu, ambapo aliwahi kuingia na kuanza kuondoka, Nami nikaingia kwenye gari langu nikaanza kuwafukuza, walisimama kupisha magari yaliyokuwa yanatokea Magomeni hivyo nikawa karibu nao kabisa. Gari hilo lilikuwa aina ya Escudo green Metallic likiwa namba zimefunikwa na karatasi ya njano ambayo bahati nzuri ilichanika nikaona baadhi ya namba hizo ambazo ni T4__ AFW.

Basi haraka nikaanza kufukuzana nao, tulipofika Manzese, kabla ya daraja niliona kuna gari la Doria la Polisi ( Saloon zenye taa juu) likiwa upande wa pili nikaamua kuanza kupiga simu wakati naendelea kuwafukuza. Bahati mbaya simu ilikuwa haipatikani, nikaendelea kufukuzana na wezi hao, waliingia magomeni kuelekea kwa shehe Yahya, nikala sambamba nao, wakafuata barabara ya Kawawa kuelekea Kigogo.

Walipofika Round about ya Kigogo wakaelekea njia ya kwenda Mburahati, Hapo ndipo nikakumbuka kuwa mimi nina tiketi ya Yule mgeni, pia kwenye gari sina hata manati, wakati huo ilikuwa kama saa kumi na moja na nusu alfajiri, na wao wako zaidi ya mmoja na watakuwa wapo tayari kwa lolote, hivyo nikaamua kurudia hapo


Nikaenda kwenye basi nikamweleza, nikampa tiketi akaendelea na safari. Niliripoti kituoni pale Urafiki na kuwaomba wachukue alama za vidole za gari langu kwani walichukua power window na begi pamoja na vitu vingine. Niliambiwa kuwa huduma hiyo haipatikani kila mahali inapatikana Central hata hivyo ni ngumu pia kuwakamata, kwa njia hiyo.

Niliwaeleza juu ya gari la doria la polisi ambalo kama wangekuwa na simu ya dharura inayofanya kazi wangenisaidia wakadai kuwa simu hiyo inafanya kazi kwa mtandao wa ZAIN tu!!!!. Mimi nilikuwa na simu (mchina) yenye laini mbili Tigo na Zantel.


Lakini niliomba wachukue maelezo yangu kwani yawezekana nitakuja kukutana na wezi hao walikubali na kuandika maelezo hayo, walinieleza kuwa wataipangia mpelelezi na kunitaarifu. Baada ya wiki kama tatu hivi niliona gari hilo hilo pale Tabata, nilikumbuka kwani Yule mwizi niliyefukuzana naye wakati anatoka kwenye gari langu alikuwepo pia akiwa amevaa vile vile kama siku aliyovunja gari langu na kuiba.

Alivaa fulana ya mistari ya pundamilia ya kulala rangi ya njano na mistari mingine blue/nyeusi, viatu vya safari boot, na Geans, pia gari hiyo ilikuwa imegongwa kwa pembeni kwenye bapa haya yote niliyaeleza kituoni yakaandikwa, Roho ilitaka kuniruka nikahamaki na kuendelea kufuatilia ambapo walipaki gari hiyo ktk gereji fulani, hizi gereji za nje na kumkabidhi kijana Fulani funguo nao wakaondoka wakiwa wawili, namba za gari hilo zilionekana vizuri T 430 AFW. Nilimuuliza kijana ni akina nani hao jamaa akadai ni washikaji wa fundi mwenzie yeye hawafahamu majina. Akanitaarifu kuwa gari litakuwa hapo kwa matengenezo.


Nikaenda urafiki kuelezea kuwa nimewapata wezi wangu lakini majibu niliyopata pale ni kuwa uwezekano wa kuwatia hatiani wezi hao ni mdogo sana na kwa kifupi hakuna kwani watakuwa tayari wameishaficha vitu walivyoiba na hakuna ushahidi wa kutosha. “Tunaweza jaribu lakini uwezekano wa kumtia hatiani ni mdogo sana ama hakuna”


Hivyo hao wanaoeleza kuwa siyo kweli ama ni chuki binafsi wajue mambo haya yapo sana wsubiri yawakute.

Nimeamua kutoa ushuhuda huu ili watu wajue kuwa haya mambo yapo sana hapa Dar Es Salaam na wachukue taadhari mapema.
 
Back
Top Bottom