Jihadhari unapokuwa maeneo haya Dar es Salaam

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,457
154,323
Kijitonyama, Sinza na Mikocheni:
Mitaa ya Sayansi, Makumbusho na Maeneo ya Mikocheni Rose Garden ni hatari sana kwa kina dada na kina kaka ambao huninginiza mabegi ya laptop na mapochi makwapani mwao.
Kuna kundi la vijana linatumia magari kukwapua mabegi na mapochi hayo.
Wanachofanya ni kwamba dereva anapunguza mwendo na kukusogelea kisha abiria aliokuwa nao hukwapua mikoba hiyo na kukimbia.
Simu pia huibiwa kwa mtindo huo.

Mbagala:
Mitaa yote ya Mbagala Charambe, Hadi Kiburugwa hi hatari sana kwa kuwa kuna kundi la vibaka linaloitwa Mbwa Mwitu. Kundi hili hupora fedha, simu na kila ulichonacho hadi viatu. Ukikutana nao wanakushambulia kwa vipisi vya nondo na kukuibia huku wakikuacha huna fahamu.

Girrafe Hotel:
Kwenye maegesho ya hoteli hii ni hatari sana kwa wenye tabia ya kuacha mali za thamani ndani ya magari yao.
Kuna kundi la vijana likishirikiana na walinzi wa hoteli hiyo, huvunja vioo vidogo ya nyuma sehemu ya kiti cha abiria, hung'oa power windows na kuchukua kila wanachoweza.
Hoteli imekuwa ikijibu wanaoibiwa kuwa hapa kwetu Parking is at owners risk.

Posta:
Maeneo haya ni hatari kwa wanaotumia daladala na wale wanaogesha magari sehemu mbalimbali za katikati ya jiji hili.
Watumia daladala wa Posta huibiwa pesa na simu zao zilizomo kwenye mikoba na mifukoni wakati wakiwa wanagombania magari mida ambayo usafiri huwa mgumu.
Wenye magari huibiwa vitu kama power windows na laptop ikiwa utaacha ndani ya gari. Na wezi wakubwa ni vijana wanaozagaa maeneo ya maegesho.

Bonde la Jangwani, Selander Bridge na Bonde la Kigogo:
Maeneo haya ni hatari kwani hamna makazi, hivyo vibaka hutumia mwanya huo kufanya uhalifu mchana kweupe, na usiku maeneo haya ni hatari zaidi.
Ukipata pancha maeneo ya jangwani nakushauri utembelee ringi hadi eitha Faya au Magomeni Mapipa ambapo pana watu na pana usalama.
Vibaka hutokea kwa staili ya kukupa msaada na mwisho wa siku hukuacha ukiwa huna kitu na huku gari yako ikiwa skrepa.

Sea View, Ocean Road na Viwanja vya Golf Gymkhanna Club:
Maeneo haya kuna vibaka hatari sana ambao hushambulia kwa kikundi na kupora mali zote na kukuacha ukiwa majeruhi.
Maeneo haya yametulia sana na yanaonekana ni salama sana kwani yako jirani na ikulu, lakini hayana usalama wowote na ni hatari kabisa.
Usipite maeneo hayo kwa miguu mida ya kuanzia saa kumi na mbili na nusu giza likiwa linaingia, maana utakumbwa na dhahama.

Polisi wanayajua maeneo yote hatari kwa raia, lakini haiboreshi ulinzi maeneo hayo na wala haiwatahadharishi wananchi.
Cha kufanya ni sisi kutahadharishana. maeneo hatari hapa Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla yapo mengi sana, naomba na wenzangu muyaongeze maeneo ambayo sijayataja hapa.
 
Jeshi la polisi lipo kweli jamani katika hali hii?

Wengi wa vibaka wanapeleka mgao kwao sasa itakuwaje wawashughulikie? Imagine pale Selender bridge ni karibu kabisa na police lakini kuna vibaka hatari pale. Kuna ndugu yangu alikuwa anafanya mazoezi pale alipofika darajani Salender walipita vibaka wawili, wakamvua pete za ndoa(engagement na wedding) na saa wakakimbia. Hapo ilikuwa mida ya saa 12 jioni.
 
Wengi wa vibaka wanapeleka mgao kwao sasa itakuwaje wawashughulikie? Imagine pale Selender bridge ni karibu kabisa na police lakini kuna vibaka hatari pale. Kuna ndugu yangu alikuwa anafanya mazoezi pale alipofika darasani Salender walipita vibaka wawili, wakamvua pete za ndoa(engagement na wedding) na saa wakakimbia. Hapo ilikuwa mida ya saa 12 jioni.

Mkuu,

kwanza hapo Selander bridge nimeshangaa sana maana kituo kipo karibu
na polisi afu najua kuna watu wameenda kulalamika. That is a very sad state of affairs.
 
Jeshi la polisi lipo kweli jamani katika hali hii?

Polisi wa Bongo ni miyeyusho tu. Kama kuna tukio la ujambazi kupiga simu Polisi ni sawa na kujisumbua tu maana Polisi wakijua kuwa majambazi wapo kwenye eneo la tukio hawatokei kuja kusaidia, wao husubiri mpaka wakishajua Majambazi wameondoka ndipo hujitokeza.
 
polisi wa bongo ni miyeyusho tu. Kama kuna tukio la ujambazi kupiga simu polisi ni sawa na kujisumbua tu maana polisi wakijua kuwa majambazi wapo kwenye eneo la tukio hawatokei kuja kusaidia, wao husubiri mpaka wakishajua majambazi wameondoka ndipo hujitokeza.
tena ukipiga 112 wanaiweka pembeni kabisa hadi majambazi wamalize kupiga show yao ndio wanaanza kupokea tena simu.
 
Buji Buji,Manzese kwa mfuga mbwa,darajani,na Uwanja wa Fisi.Tandika Wireless,Kwa Maguruwe na Pale Sokota.Ubungo Stand ya Mkoa,Kituo Kidogo cha Daladala,Kimara Stop Over na Mwenge yote haya ni maeneo ya Vita mithili ya Ukanda wa Gaza.Vibaka wanapiga watu miereka kila kukicha polisi wanajua tena pengine wanaona lakini mkondo ndo huo.

Mkoani kule Tabora Ng'ambo,Isevya na Mwanza Street
 
Nashukuru sana mkubwa Bujibuji kwa taarifa lakini tunamuomba mkubwa wa polisi kanda maalum atoe maelekezo maeneo haya yazibitiwe manake kama pale kigogo na jangwani tangu niko mdogo inajulikana sio maeneo salama sasa dah mpaka leo ?Watanania sasa tuseme inatosha kwakweli
 
Masaki kwenye makutano ya barabara ya Toure na Mwaya (karibu na Ubalozi wa South Africa). Wengi wamelizwa na vibaka wanaorusha mayai kwenye windscreens za magari.

Corner ya St. Peter's bado ni hatari sana. Vibaka wana target wakina mama wanaoweka mikoba yao kwenye passenger seats.

Parking ya Mlimani City. Yaani hapo sielewagi wale walinzi wanafanya kazi gani. Maana ni kama tu hawapo.
 
Hawa jamaa wanatumia pikipiki kwa maeneo ambayo huwa na folleni style ni ile ile ya kupunguza mwendo kama anakugonga halafu ana pitia kilichopo simu, mikoba nk
 
tena ukipiga 112 wanaiweka pembeni kabisa hadi majambazi wamalize kupiga show yao ndio wanaanza kupokea tena simu.

Jeshi letu ni la kisiasa zaidi muda mwingi wanatumia kusimama barabarani kwa ajili ya kuongoza misafara na kuwepo kwenye matukio ambapo viongozi wanahutubia na kuacha wananchi wa kawaida wakisulubiwa.

Kama kiongozi anaenda labda whitesands toka atokapo mpaka whitesands, kila ambapo barabara ndogo inaingia kwenye barabara kubwa lazima kuwe na askari. Hawa ni maaskari wanotakiwa kushika majambazi, kufanya upelelezi na kutoa ushahidi mahakamani etc lakini wote wanaacha kazi zao na kushughulikia misafara.

Sidhani kama ni usalama wa raia kama ngao yao inavyosema hiyo ni understatement.
 
naona TZ sasa inataka kuwa kama Somalia. Maana yake kuna Serikali ya Kikete, Serikali ya mafisadi na sasa imeanza Serikali ya Vibaka.

Tuombe isije ikawa kama ile ya Kiboko msheli enzi zile.

Poleni aTanzania.
 
Wengi wa vibaka wanapeleka mgao kwao sasa itakuwaje wawashughulikie? Imagine pale Selender bridge ni karibu kabisa na police lakini kuna vibaka hatari pale. Kuna ndugu yangu alikuwa anafanya mazoezi pale alipofika darajani Salender walipita vibaka wawili, wakamvua pete za ndoa(engagement na wedding) na saa wakakimbia. Hapo ilikuwa mida ya saa 12 jioni.
..Nakubaliana na wewe, kuna siku nilishuhudia tukio la ajabu pale coco beach binti mmoja aliporwa simu ya mkononi jamaa mmoja akatokea kwenda kumsaidia alimkimbiza yule kibaka na kuipata ile simu na kumrudishia mwenyewe. Kilichotokea vibaka wengine wakamzonga yule jamaa aliyemsaidia yule dada kwa madai kuwa amewazibia riziki kwani wao hiyo ndio kazi yao na huwa nawanapoza hata polisi wanaofanya doria maeneo hayo na wakatishia kuwa watamlengesha jamaa kuwa ana bangi ili nae wamkomoe. Nilisikitika sana kama hata wahalifu nao wanatumia polisi kujilinda dhidi ya uhalifu wao.
 
..nakubaliana na wewe, kuna siku nilishuhudia tukio la ajabu pale coco beach binti mmoja aliporwa simu ya mkononi jamaa mmoja akatokea kwenda kumsaidia alimkimbiza yule kibaka na kuipata ile simu na kumrudishia mwenyewe. Kilichotokea vibaka wengine wakamzonga yule jamaa aliyemsaidia yule dada kwa madai kuwa amewazibia riziki kwani wao hiyo ndio kazi yao na huwa nawanapoza hata polisi wanaofanya doria maeneo hayo na wakatishia kuwa watamlengesha jamaa kuwa ana bangi ili nae wamkomoe. Nilisikitika sana kama hata wahalifu nao wanatumia polisi kujilinda dhidi ya uhalifu wao.

hii ndio faida ya kuwa na jeshi la polisi lililogubikwa na rushwa
 
Mwanza pale mabatini ,miti mirefu,kirumba Kiss night club ,Rumours,Delux,hala hala na watoto wa wakoma,pale Kiss night club mabaunsa na tazi drivers hushirikiana na vibaka na vyangu
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom