Jihadhari na tapeli huyu

debon

Senior Member
Oct 6, 2011
134
62
Kuna mtu anajiita Joshua, kanipigia simu eti nimsaidie kununua dawa za waterguard ana kampuni ya kuchimba visima.

Nilivyomuhoji sana kaishia kunitukana.
 
Mimi alinipigia simu akinitaka nimsaidie kununua majembe ya trekta zake eti ana kampuni la kilimo kwanza pale mtwara halafu nimtumie,nilipomwomba pesa akadai nitumie zangu atanirudishia
 
kumkamata chukua namba yake nenda kituo cha polisi kilicho karbu nawe kisha toa taarfa tukio lilivyokuwa . kukamatwa ni rahisi sana.
 
Mimi alinipigia simu akinitaka nimsaidie kununua majembe ya trekta zake eti ana kampuni la kilimo kwanza pale mtwara halafu nimtumie,nilipomwomba pesa akadai nitumie zangu atanirudishia

huyu naona ni sugu
 
Mimi alitaka nimnunulie vinyago wazungu wanavihitaji haraka yeye yuko mbali
 
huyu ni yule aliyetakakumdhurumu mamdogo kwakudai wafanye dili la vinyago teeeh hatare sana huyu
 
Mimi alinipigia anataka nimsaidie kumpeleka kununu trekta ndugu yake kikosi cha JKT yaani ni full utapeli lakini nikamshtukia maana mtu toka kusikojulikana anajifanya anakufahaamu.
 
Hata mimi alinipigia eti nikamnunulie waterguard wizara ya kilimo eti nijidai mimi ni mjasiriamali hvyo nitapata kwe bei ndogo.nilimwambia sina huo mda
 
Hata mimi alinipigia eti nikamnunulie waterguard wizara ya kilimo eti nijidai mimi ni mjasiriamali hvyo nitapata kwe bei ndogo.nilimwambia sina huo mda
hahaha hiyo ndo gia kajanayo kwangu
 
Mi nilipigiwa na mtu ambaye nilikuwa nafahamiana naye kabisa katafuta na mtu mwingine anabana pua eti ni mzungu. Wanataka mimi ninunue sample ya dawa sijui ya kusafishia maji ya visima thamani ya sample 7M halafu nikiwaonuesha wanikabidhi dili ya 200M!!

Sasa nikashangaa jamaa ananielekeza mwenyewe mtu wa kuniuzia hiyo sample nikajiuliza kama ni hivyo kwa nini anipe hiyo dili kiulaini hivyo... nikawabana kwamba huyo mtu namuonyesha hela anipe hiyo sample tuwe naye hadi mnaponokabidhi hiyo dili wakaingia mtini
 
0758 084133 (anajiita David Msuya), 0685 526710 (anajiita Samson Jackson), 0742088063 (anajiita Patrick Mapunda), 0742 087984. Watu hawa wanajifanya ni wataalamu wa kilimo. Walipotaka kunitapeli niliwashtukia. Inasemekana wanaishi Arusha, Mwanza na Dar. Polisi wakidhamiria watawashika kirahisi kwa kufuatilia minara ya simu wanayotumia
 
0742 087984 (anajiita mzee pita) anajifanya mwanajeshi wa suma JKT (Nyegezi) MWANZA.
 
Duuuuuuuuh, kwahiyo nyinyi wote hamkuibiwa !!!!!!!!!! ina maana ni mimi peke yangu ndio walifanikiwa kuniibia tsh 700 milioni, lakini poa nimewasamehe kwa vile vihela vyenyewe vilikuwa ni kwaajili ya kumnunulia mwanangu midoli.
 
haha, midoli ya million 700 na una jina TV za kichina?
 
Back
Top Bottom