Jihadhari na matapeli wanaojifanya kama wafanyakazi wa TRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jihadhari na matapeli wanaojifanya kama wafanyakazi wa TRA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pianist, Mar 1, 2012.

 1. Pianist

  Pianist JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Kuna matapeli wanapita mitaani na gari na kujifanya wao wametumwa na TRA kuangalia biashara ndogondogo kama saluni, stationery, magenge na maduka kama zimesajiliwa. Hawana vitambulisho na gari wanayotumia ina namba za usajili za kiraia. Wakikuta hauna leseni na TIN number wanatoa vitisho vya faini kubwa (laki tano, milioni) na kisha kuomba rushwa (elfu hamsini) na kuchukua baadhi ya bidhaa unazouza kama; kopo la maziwa ya unga, dumu la mafuta ya kula bila ya kuwa na aibu. Hawa ni wezi na matapeli kama walivyo wengine. Siku ukiwaona wapo kwenye sehemu ya biashara ya mtu mjulishe mhusika kwamba hao ni wezi asiwape rushwa.
   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, taarifa muafaka sana hii, hasa katika kipindi hiki ambacho TRA wameamua kuwazungukia wafanyabiashara katika maeneo yao ya biashara. Kimsingi, mtumishi yeyote wa Serikali (TRA) anapokutembelea katika biashara yako basi muombe AKUONYESHE KITAMBULISHO. Usibabaishwe na uniform
   
Loading...