Jihadhari mtanzania usitegemee mabeberu watakulinda kwenye mambo ya kisiasa

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,999
4,480
Sio kama naunga mkono mambo yanayoendelea nchini ila tukae tukijua sasa Tanzania inaenda kuwa kama China kwa upande wa demokrasia na uhuru wa habari.

Nimefurahi sana leo TCRA kupiga nyundo baadhi ya vituo fulani vya radio japo kwa nia ovu lakini ninafurahi kwa sababu hakuna alie salama kwa sasa.

Andamana ukitegemea BBC na mashirika ya nje yatatangaza mnavyopigwa lakini sasa wamepigwa pini.
Toka 2015 tuliona uhuru wa vyombo vya habari kubadilika na TCRA kuanza na makucha makali.

Kwa ninachokiona huku mbele tunaanza kuelewana na kuongea lugha 1. Twendeni tu,mnaosifia endeleeni kusifia,waimbaji pazeni sauti ya juu.

Ila wana harakati,wakosoaji na wapinzani bora mjiweke pembeni tu mana ukipigwa unazikwa na hakuna atakaekusaidia,hata kama ana nia ya kukusaidia(beberu) lakini hana taarifa.

Kila mtu anawajibika kwa uhai wake mwenyewe. Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom