Jifunzeni kitu hapa

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Ukiambiwa Dr Salim Ahmed Salim aliteuliwa balozi nchini Misri akiwa na miaka 22 halafu ukalinganisha na vijana wa leo wenye elimu na umri huo utaona kama vile tunarudi nyuma badala kwenda mbele...

Na ukiambiwa miaka ya 1970 hadi 1990 nchi yetu ilikuwa na vyama vya ushirika kila mkoa vyenye nguvu kabisa vya kuweza kununua mazao ya wakulima bila matatizo halafu ukalinganisha na Sacco's za sasa hivi za wasomi wetu utaona tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele...

Ukiambiwa zamani nchi yetu bila wasomi ilikuwa na viwanda Mutex mwatex, kilitex urafiki n.k na mashirika ya umma yenye mafanikio makubwa sana lakini baada wasomi kuyaongoza ndo yamefirisika kabisa lazima utakuwa na mashaka na elimu za vijana wetu ...

Ukiambiwa zamani kwamba mzazi yeyote alikuwa anaweza kumchapa mtoto ambaye siyo wake na mtoto akienda kulalamika kwao anaongezewa kipigo utajua maadili yanazidi kuporomoka kuliko zamani ...

Ukiambiwa zamani vijana walikuwa wanachaguliwa wachumba na wazazi wao na wanakubaliana kuoana na ndoa zinadumu tofauti na sasa vijana wanachunguzana miaka mitano lakini wakioana ndoa hazidumu utagundua watu wa zamani hawakuwa na elimu lakini walikuwa na busara kuzidi wa sasa hivi...

Ukiambiwa kuwa mama wa zamani alikuwa anaenda shambani na mtoto mgongoni anapitia maji kichwani na kuni kwapani, lakini wa siku hizi hata kupika ugali hawawezi utaelewa kuwa Siku hizi wamebaki wanawake majina tu wanatamani kutumia computer kupika wali ...au simu kupika ugali.

Ukiambiwa zamani wazee wa kimila walikuwa na maadili sana tofauti na viongozi wa dini wa siku hizi..utagundua dini zimekuja kwa nia njema ila zinatumiwa vibaya pia.

Au wewe unaonaje? Kwamba baada ya miaka kadhaa ijayo tutakuwa na wasomi wengi wa mitandaoni lakini watendaji wa mikono hawatakuwapo.


Good night
 
Tatizo ni upigaji wa madili, miaka ya 70 SU yaani shirika la umma kirefu cha msomi ni"Soma ule" hapo unategemea uzalendo?mambo ni"chukua chako mapema"
 
Zamani tuliweza kubuni gari la nyumbu, sasa wasomi wetu wanabuni sanamu la mabati...
 
Ukiambiwa zamani Viongozi wa Timu za mpira za Simba na Yanga walijenga ofisi zilizopo hadi leo Lakini viongozi wasomi wameshindwa kujenga Viwanja vya timu hizo hata vilivyozungushiwa ukuta wa mabati chakavu tu ndiyo utajua kuwa tumerudi nyuma saaana.
 
Kama mimi nikiwa rais wa nchi hii matatizo yote kabisa yatakoma lakini ninachoamini ni kwamba mpaka nikifa sitakuja kuwa rais na hivyo nitakufa huku roho inauma
Kuendesha nchi ni kitu rahisi sana sijui wanapofeli hawa raia
 
Kipindi baba ana umri kama nilionao hivi sasa, alikuwa amejenga, alikuwa na watoto watatu (ambapo mimi ndo nilikuwa nimezaliwa) na alikuwa na miradi kadha wa kadha....kinyume chake kwangu ni bilabila...pamoja na yote hayo naamini kila mtu ana bahati yake...siilalii mlango wazi bahati ya dingi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom