John kisomo
Member
- Jan 21, 2019
- 22
- 39
MAANA YA UTAFITI AND AINA ZA UTAFITI
Wataalam wengi wametafsiri neno research/utafiri katika mirengo tofauti. Kiujuumla Research/Utafiti ni ni uchunguzi wa asili wenye mpangilio unaofanywa ili kuongeza ujuzi na uelewa kuhusu jambo au tukio. Lengo kubwa la utafiti wa aina yoyote ni kuhakiki ukweli wa mambo, kutoa matazamo mpya kuhusu suala linalosibu jamii na kuvumbua vifaa vipya na utaratibu mpya katika kufanyia jambo husika na kutatua matatizo yanayoikabili jamii.
*Aina za Tafiti(Types of Research)*: Utafiti hugawika katika matapo mbalimbali kwa kutegemea madhumuni na maksudi ya utafiti:-
*1.Utafiti wakimakusudi*
*a.Utafiti wa Kimsingi (Basic Research)*: Hii ni aina ya utafiti ambao hutumiwa kujaliza ufahamu ambao jamii au mtafiti hana kuhusu swala fulani katika jamii.Utafiti huu hutumiwa katika kujaribu kujifunza mambo au vitu ambavyo kwa kawaida havikai kuwa wazi au havionyeshi umuhimu wake mara moja.
*b.Utafiti Tumikizi (Applied Research)*: Utafiti tumikizi hutafiti kuhusu swala maalum na kutambua ikiwa nadharia fulani inatimiza matakwa yake au la. Hivyo basi utafiti tumikizi hutumiwa data moja kwa moja ili kutoa suluhisho kuhusu tatizo lililopo wakati uo huo.
*c.Utafiti Kiutendaji (Action Research)*: Ni aina ya utafiti ambao kwamba hufanywa na wale ambao wana nia na lengo la kuchukua hatua katika kusuluhisha jambo fulani katika jamii. Jambo au tatizo hili huwa lile ambalo limeibuka na limeikumba jamii wakati maalum na utatuzi wake huhitajika papo kwa papo wala si wakati mwingine.
*d.Utafiti wa Kutathmini (Evaluation Research)*: Utafiti wa aina hii hufanywa kwa lengo la kuthibitisha iwapo yaliyotarajiwa ndiyo yaliyotimia. Hivyo basi, utafiti huu huwa wa utaratibu fulani wa kukusanya data kisha kuichanganua data hiyo. Kwa mfano, utafiti wa aina hii unaweza kufanywa kuthibitisha kama mpango wa elimu ya bure umefaulu au la.
*2. Uainishaji kwa kutumia mbinu za uchanganuzi*
*a.Utafiti wa kueleza (Descriptive Research)*: Ni aina ya utafiti ambao unakusanya data ambayo data hiyo itauwezesha utafiti huo kufanya majaribio au kuyajibu maswali yanayohusu mada ya utafiti wakati ule. Huu ni utafiti ambao hueleza jinsi mambo yalivyo.
*b.Utafiti Linganishi (Casual – Comparative Research)*: Huu ni utafiti ambao hutumiwa katikaulinganishaji wa vigeu ukiwa na nia au lengo la kutaka kuonyesha sababu za jambo au hali kuwa jinsi ilivyo.
*c.Utafiti Wiani (Correlation Research)*: Kwa ujumla, utafiti wiani ni utafiti ambao unavigeu viwiliau zaidi kutoka katikasampuli moja. Hivyo basi mtafiti huwa kwake anajaribu kutafiti iwapoupo uhusiano mabadiliko katika vigeu hivyo.
*3.Uainishaji Kulingana na Aina za Utafiti.*
*a.Utafiti wa Kukagua (Survey Research)*: Hii ni aina ya utafiti ambapo mtafiti hukusanya data kutoka kwa makundi husika na ili kutambua haliyake kwa wakati ule kwamujibi wa kigeu kimoja au zaidi.
*b.Utafiti wa kihistoria (Historical research)*: Huu utafiti unahusu usomi unaohitajika katika kukusanya ujumbe/taarifa kutoka wakati uliopita. Mtafiti hutafuta data ambayo tayari ipo.
*c.Utafiti wa Uchunzaji (Observation Research)*: Kwenye utafiti wa aina hii, jambo linachunguzwa kwa kuliangalia tu. Utafiti huu hutoa taarifa ambayo haina hisia za kibinafsi kwa sababu mtafiti huchunuguzana kuangalia hali katika mazingira yake halisi au ya kawaida.
*d.Utafiti wa majaribio (Experimental Research)*: Aina hii ya utafiti hufanyika kwa kuhusisha vitu, wanyama au binaadam kwa kuchunguza tatizo katika chumba maalum(maabara). Miongoni mwa lengo la utafiti huu nikuangalia casual effect baina ya variables.
Kwa maelezo ya ziada unaweza kutembelea:
>
>
>
>
Masomo mengine; uzi #6 na Uzi # 7.
muda ummenda na unashindwa kufanya kumaliza Research yako kwa wakati?.au muandika andiko? Uwe bachelor, masters su PHD, njoo uhudumiwr na team ya ma docta.(phd holders) njoo tujifunze zaidi, kwa kina. Pia kukuongoza kuandika utafiti wako,