Jifunze TENSES hapa

Mimi nagombana na wadogo zangu kila siku kwenye group la family, na unakuta ni graduates kabisa.

Sijui hata report wanaandikaje.
Wengi wanachukulia poa ila ukiwakuta katika academic issues wanaandika vizuri tu. Usasa tu unawaharibu wengi
 
Hapo nakupata, bahati mbaya old schools tunakagua hadi SMS. Unaanza kum-judge mtu kwenye mwandiko, then content.
Hahaaaaa i'm not old school ila hizi new ways huwa zinanipa tabu kiasi mfano kutumia x kwenye s, Kutumia K badala ya ok.
 
ukitaka kumuuliza mtu wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa kwenu hapo kwa english inakuaje?
Utunzi wa sentensi kwa kila lugha hotofautiana na huwezi kutafsiri lugha kwenda lugha nyingine kwa kufikiri kwa lugha yako au kwa kufikiri kwa tamaduni yako. Kiheshima za tamaduni husika inabidi uulize swali kama wenye lugha watavyouliza. "Are you the first born in your family?" Na hata hapo inabidi uwe na mazowea ya ukaribu sana na unaemuuliza na akikuheshimu atakujibu yeye ni wangapi kuzaliwa, la sivyo anaweza kukushangaa kwa kumuuliza vitu vya familia yake. Wanajali sana "privacy".

Hata kuulizana umri tu kwa tamaduni za wazungu ni jambo lisilo pendeza.
 
II. Present continuous tense ( wakati uliopo hali ya kuendelea )

Tumeshasoma kuhusu simple present tense . Sasa hapa tunaangalie " the present continuous tense . "

Vitenzi vya " the present continuous tense " huwa vinaongezewa ING mbele.

MUUNDO WA SENTENSI ZA PRESENT CONTINUOUS TENSE :

Hapa tuna miundo mitatu ya sentensi ambayo ni :

1. Sentensi za kukubali / chanya
2. Sentensi za kukanusha
3. Sentensi za kuuliza maswali

1. Sentensi za kukubali / chanya

SUBJECT + AM / IS / ARE + MAIN VERB+ING

Ufafanuzi

AM - inatumika na I
IS
- inatumika na nafsi ya tatu umoja , yani " He, shena It " .

ARE - inatumika na " You , We na They"

Examples :

I am cleaning my room
( Nina safisha chumba changu )

She is listening to music now.
( Anasikiliza mziki sasa )

They are waiting for me.
( Wananisubiria mimi )

You are watching TV
( Unaangalia TV )

2. Sentensi za kukanusha

SUBJECT + AM / IS / ARE + NOT + MAIN VERB + ING

Examples :

She is not eating food .
( hali chakula . )

He is not watching television .
( Haangalii runinga . )

I am not reading a book now
( Sisomi kitabu kwa sasa . )

3 . Sentensi za kuuliza maswali

Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :

AM / IS / ARE + SUBJECT + MAIN VERB + ING

Examples :

Is he watching TV ?
( je , anaangalia TV ? )

Are they waiting for john ?
( je wanamsubiria john ? )

MATUMIZI YA THE PRESENT CONTINUOUS TENSE ( WAKATI ULIOPO UNAOENDELEA ) :

1. Kwa vitendo au vitu ambavyo vinaendelea kwa sasa yani muda huu .

Examples :

They are eating right now .
( wanakula chakula sasa hivi . )

I am learning to drive a car .
( Ninajifunza kuendesha gari . )

He is living with his sister until he finds a room .
( Anaishi na dada yake mpaka pale atakapopata chumba . )

2.Tunatumia kuongelea vitu vijavyo au vitakavyofanyika wakati ujao.

Pia tunaweza kutumia the present continuous tense kuongela mambo yajayo - kama tukiongezea neno la wakati ujao kama vile : tomorrow , next year , next week n.k .

Tunatumia present continuous tense kuongelea vitu vijavyo ikiwa tayari tushaamua na tushapanga kabla ya kuongea .

Examples :

I am starting my new job next month
( ninaanza kazi yangu mpya mwezi ujao )

We are eating at mama ntilie tonight . We have already booked the table .

( Tunakula kwa mama ntilie usiku . Tayari tushaweka ( oda ) .... )

When you are starting your new job ?
( Lini unaanza kazi yako mpya ? )

SHERIA ZA VITENZI KATIKA PRESENT CONTINUOUS TENSE .

Vitenzi vya present continuous tense huwa tunaongezea " ING " katika kitenzi kikuu ( main verb )

Mfano : go / going , do / doing , look / looking , read / reading , stay / staying .

- Ila kwa vitenzi ambavyo vinaishia E , huwa tunaondoa E na kuongezea ING , Mfano : come / coming , mistake / mistaking .

- Kwa vitenzi ambavyo vinaishia na IE , huwa tunabadilisha IE kuwa Y . Mfano : lie / lying , die / dying .

.......................
 
III. Present perfect tense ( wakati uliopo hali timilifu )

The present perfect tense
ni moja wapo ya nyakati muhimu sana ambayo unatakiwa kuifahamu wakati unapoanza kujifunza lugha ya kiingereza .

Nyakati hii tunaitumia kuzungumzia mambo ambayo tayari yameshafanyika tayari ( au yameshakamilika kufanyika tayari au tukio ambalo limekamilika kufanyika ) .

MUUNDO WA SENTENSI ZA " THE PRESENT PERFECT TENSE " .

1. Sentensi za kukubali/ chanya

SUBJECT + HAS / HAVE +MAIN VERB

Ufafanuzi

" Has " inatumika kwa nafsi ya tatu umoja, yani => He , she na It .

" Have " inatumika kwa => I , You , We na They .

Main verb - hiki ni kitenzi kikuu , katika tense hii huwa tunatumia vitenzi ambavyo vipo katika muundo wa past participle . Mara nyingi huwa vinaishia na ED .

2. Sentensi za kukanusha/hasi

SUBJECT + HAS / HAVE + NOT + MAIN VERB .

Mfano : I have not done ( sijafanya ) .

3. kwa sentensi za kuuliza maswali

HAS / HAVE + SUBJECT + MAIN VERB

Examples :

Have you finished ?
( umemaliza ?)

Have they done it ?
( wameifanya ? )

VIFUPISHO VINAVYOTUMIKAKATIKA PRESENT PERFECT TENSE .

I have = I've
You have = You've
He has = He's
She has = She's
It has = It's
We have = We've
They have = They've

SASA TUANGALIE BAADHI YA MIFANO YA SENTENSI ZA NYAKATI HII .

1. You've told me that before .
( Uliniambia hilo kabla .)

2. She has seen it .
( Ameiona )

3. You have eaten my food .
( Umekula chakula changu )

4. We have not played football .
( Hatujacheza mpira )

5. Have they done it ?
( Wameifanya ? )

6. He's seen Harry Potter .
( Ameiona Harry Potter )

Jinsi ya kutumia SINCE na FOR

Mara nyingi huwa tunatumia SINCE na FOR katika tense hii

👉 Tunatumia FOR kuongelea kipindi cha muda , mfano : For 6 years , for 2 hours , for 4 weeks , for 8 minutes ... N.k

👉Tunatumia SINCE kuongelea muda wa kitu kuanza ... SINCE ( tangu ) . Mfano : Since yesterday ( tangu jana ) , since wednesday ( tangu jumatano ) n.k

Mifano zaidi

I have been here since morning
( Nimekuwa hapa tangu asubuhi )

He has worked here since 2001.
( Amefanya kazi hapa tangu mwaka 2001 )

I have worked here for 3 years
( Nimefanya kazi hapa kwa miaka mitatu )

She has known your parents for long time .
( Amewajua wazazi wako kwa muda mrefu )
..……...............................................
 
Utunzi wa sentensi kwa kila lugha hotofautiana na huwezi kutafsiri lugha kwenda lugha nyingine kwa kufikiri kwa lugha yako au kwa kufikiri kwa tamaduni yako. Kiheshima za tamaduni husika inabidi uulize swali kama wenye lugha watavyouliza. "Are you the first born in your family?" Na hata hapo inabidi uwe na mazowea ya ukaribu sana na unaemuuliza na akikuheshimu atakujibu yeye ni wangapi kuzaliwa, la sivyo anaweza kukushangaa kwa kumuuliza vitu vya familia yake. Wanajali sana "privacy".
Hata kuulizana umri tu kwa tamaduni za wazungu ni jambo lisilo pendeza.
asante
 
IV.Present perfect continuous tense

1107761



Tumeshasoma tayari " present perfect tense " . Sasa leo tuangalie " The present perfect continuous tense " .

Present perfect continuous tense - nyakati hii hutumika kuonyesha vitendo ambavyo vipo katika hali timilifu inayoendelea ( Yani
kitendo kilikuwa kimefanyika lakini katika hali ya kuendelea ) .

JINSI YA KUTENGENEZA SENTENSI ZA " PRESENT CONTINUOS TENSE " .

1. Kwa sentensi za kukubali / chanya

SUBJECT + HAS / HAVE + BEEN + MAIN VERB + ING

Ufafanuzi

MAIN VERB - Hiki ni kitenzi kikuu , kitenzi hiki tunaongeza ING mbele . Mfano : live / living , go / going , see / seing .

" Have " inatumika na I , You , We na They ( Nafsi ya kwanza umoja , na nafsi zingine isipokuwa nafsi ya tatu umoja )

" Has " inatumika na He , She na It.

Mfano :

I have been living here for 2 years
( Nimekuwa nikiishi hapa kwa miaka miwili ) .

She has been working here for 4 months .
( Amefanya kazi hapa kwa miezi minne )

2. Kwa sentensi za kukanusha / hasi
SUBJECT + HAS / HAVE + NOT + MAIN VERB + ING

Mfano : I have not been ......

3. Kwa sentensi za kuuliza maswali

HAS / HAVE + SUBJECT + MAIN VERB + ING

Mfano : Have you been.......

MIFANO ZAIDI .

I have been waiting for you 4 hours .
( Nimekuwa nikikusubiri kwa masaa
manne )

I'm tired because I have been running .
( Nimechoka kwa sababu nimekuwa
nikikimbia )

You have been talking to him since
morning .
( Umekuwa ukiongea nae tangu asubuhi )

It has not been raining.
( Haikuwa ikinyesha )

We have not been playing football .
( Hatukuwa tukicheza mpira )

You don't understand now because you
have not been listening
( huelewi sasa kwa sababu haukuwa
ukisikiliza .)

Have they been doing this work ?
( je , wamekuwa wakifanya kazi hii )

***************************
 

Attachments

  • images (11).jpeg
    images (11).jpeg
    8.5 KB · Views: 39
IV.Present perfect continuous tense

View attachment 1107761


Tumeshasoma tayari " present perfect tense " . Sasa leo tuangalie " The present perfect continuous tense " .

Present perfect continuous tense - nyakati hii hutumika kuonyesha vitendo ambavyo vipo katika hali timilifu inayoendelea ( Yani
kitendo kilikuwa kimefanyika lakini katika hali ya kuendelea ) .

JINSI YA KUTENGENEZA SENTENSI ZA " PRESENT CONTINUOS TENSE " .

1. Kwa sentensi za kukubali / chanya

SUBJECT + HAS / HAVE + BEEN + MAIN VERB + ING

Ufafanuzi

MAIN VERB - Hiki ni kitenzi kikuu , kitenzi hiki tunaongeza ING mbele . Mfano : live / living , go / going , see / seing .

" Have " inatumika na I , You , We na They ( Nafsi ya kwanza umoja , na nafsi zingine isipokuwa nafsi ya tatu umoja )

" Has " inatumika na He , She na It.

Mfano :

I have been living here for 2 years
( Nimekuwa nikiishi hapa kwa miaka miwili ) .

She has been working here for 4 months .
( Amefanya kazi hapa kwa miezi minne )

2. Kwa sentensi za kukanusha / hasi
SUBJECT + HAS / HAVE + NOT + MAIN VERB + ING

Mfano : I have not been ......

3. Kwa sentensi za kuuliza maswali

HAS / HAVE + SUBJECT + MAIN VERB + ING

Mfano : Have you been.......

MIFANO ZAIDI .

I have been waiting for you 4 hours .
( Nimekuwa nikikusubiri kwa masaa
manne )

I'm tired because I have been running .
( Nimechoka kwa sababu nimekuwa
nikikimbia )

You have been talking to him since
morning .
( Umekuwa ukiongea nae tangu asubuhi )

It has not been raining.
( Haikuwa ikinyesha )

We have not been playing football .
( Hatukuwa tukicheza mpira )

You don't understand now because you
have not been listening
( huelewi sasa kwa sababu haukuwa
ukisikiliza .)

Have they been doing this work ?
( je , wamekuwa wakifanya kazi hii )

***************************
Pls mkuu tuendelee na somo....

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom