Wadau nataka kufanya manunuz aliexpress lkn sijui nianzie wap kabisaa, nahitajika kua na vitu ganii
 
mtandaoni je hata mastercard ya CRDB wanatoza pesa ukifanya malipo mtandaoni, Kama ndio je wanatoza kiasi gani?
Kila mtoa huduma, hizi benki, zinazotupatia visacard / mastercard huwa na makato fulani pindi kadi husika inapotumika,

Makato yako katika makundi mawili.
- Kuna baadhi ya benki huwa na flat rate , kiasi kidogo sana, (Hutumia neno bure, kwamba hakuna makato,i ila kiuhalisia yapo) kwa kila muamala unaofanyika mtandaoni.
- Na kuna benki zingine huwa ni asilimia fulani ya kiasi cha muamala unaofanyika.
 
Asante ndugu
Nitawauliza watu wa Bank ya CRDB Ili nijue makato yao
Kila mtoa huduma, hizi benki, zinazotupatia visacard / mastercard huwa na makato fulani pindi kadi husika inapotumika,

Makato yako katika makundi mawili.
- Kuna baadhi ya benki huwa na flat rate , kiasi kidogo sana, (Hutumia neno bure, kwamba hakuna makato,i ila kiuhalisia yapo) kwa kila muamala unaofanyika mtandaoni.
- Na kuna benki zingine huwa ni asilimia fulani ya kiasi cha muamala unaofanyika.
 
Bulldog na wadau wengine nimenunua mzigo TABLET PC aina ya Lenovo kwa shillingi 250,000 ALIEXPRESS imefika within two weeks sikutoa kodi hata mia, nimenunua pia simu aina ya i ocean x8 mini ya ukweli balaa level za i phone 5 na galaxy s4 kwa shillingi laki 270-280

nimeagiza (bado inakuja) wireless router inayotumia Line ya simu, iko unlocked kwa shillingi elfu 80 na huku ni laki na 50...inaweza ku transfer 21 mbs per second

kwa uzoefu wangu wa miaka 3 kununua vitu online AMAZON kuna bei mkasi sana, ikifuatia EBAY, ali express ndio watu wengi hasa wafanya biashara wanapaweza na ALIBABA

LENOVO TABLET YENYEWE HII HAPA

lenovo-ideatab-a3300-quad-core-2gb-ram-8gb-rom-ori-msia-set-welllinkmobile-1404-18-WellLinkMobile@1.jpg


Haina haja ya kuogopa kununua mtandaoni ndugu zanguni kama watu wengi wanavyodhania
Mkuu Mimi pia nawakubali AliExpress.Wapo cheap.
 
Kila mtoa huduma, hizi benki, zinazotupatia visacard / mastercard huwa na makato fulani pindi kadi husika inapotumika,

Makato yako katika makundi mawili.
- Kuna baadhi ya benki huwa na flat rate , kiasi kidogo sana, (Hutumia neno bure, kwamba hakuna makato,i ila kiuhalisia yapo) kwa kila muamala unaofanyika mtandaoni.
- Na kuna benki zingine huwa ni asilimia fulani ya kiasi cha muamala unaofanyika.
Mwl.RCT huu mzigo kwa haraka hadi nautia mkononi unaweza gharimu malaki mangapi?
Screenshot_20190428-194031.png
 
Kila mtoa huduma, hizi benki, zinazotupatia visacard / mastercard huwa na makato fulani pindi kadi husika inapotumika,

Makato yako katika makundi mawili.
- Kuna baadhi ya benki huwa na flat rate , kiasi kidogo sana, (Hutumia neno bure, kwamba hakuna makato,i ila kiuhalisia yapo) kwa kila muamala unaofanyika mtandaoni.
- Na kuna benki zingine huwa ni asilimia fulani ya kiasi cha muamala unaofanyika.
Mkuu nataka kuagiza mzigo wa dola 130 hivi, makato yake ya kodi nikitumia DHL yatakua shilingi ngapi? na nikiamua kutumia posta kawaida itakua makato kiasi gani?
 
Hatimaye! Unaweza kufanya malipo mtandaoni kwa M-Pesa
Inaweza ikapokea pesa ukitumiwa say from bank ingine??
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?

Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: http://comgateway.com/ - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT
iko poa sana i think ni kitu kizuri kujua kabla hujaanza respect sana
 
Usiogope mkuu,Mimi niliwahi kufanya majaribio kule AliExpress Kwa kununua earphone kwa Buku jero(1,500/=) na zikafika.Ni original na ninazo mpaka Sasa hivi.
UPDATE
Nimeipokea hi Simu tarehe 29/4/2019.Ilichukua wiki mbili na kidogo tangu naagiza na kunifikia.
AliExpress ndiko nilikonunulia hiyo Simu.

IMG_20190430_150846.jpeg
IMG_20190430_092141.jpeg
 
Malipo ya kodi TRA huwa yanakuwaje? Nataka kuagiza mzigo, shida sijui hapa Tz nitaulipia shilingi ngapi!
 
Back
Top Bottom