JZHOELO

Senior Member
Sep 20, 2011
196
350
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?

Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop the US Online and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT


Habari Watanzania, Heri ya miaka 58 ya uhuru!

Bila kupoteza muda ngoja tuongee namna ya kununua vitu kutoka nchini China hasa kupitia platform ya Alibaba (Made in China).

Kwanza kabisa Alibaba sio platform peke yake ya kuweza kununua vitu nchini China kuna platforms kama Global sources, Made-in-China, Banggood na kadhalika.

Najaribu kufikiria unafahamu kuingia kwenye mtandao wa alibaba na unaweza kutafuta bidhaa. Sasa nataka kukuonesha namna ya kuwa mbele ya wauzaji wa kichina kwenye platform ya alibaba na vitu vya kufanya kuepuka kupoteza muda na kuumia kichwa mbeleni.

1. Bidhaa (Product)
Hakikisha muuzaji wa kichina (supplier) anafahamu nini kabisa unataka kununua hapa inamaanisha (products specifications). Hakikisha unaeleza vizuri kwa ufanisi na kiundani unataka nini hasa kwenye bidhaa yako. Ushauri Chukua dakika 10-15 kuandaa maelezo ya bidhaa, vitu kama
- Size (Ukubwa)
- Material (Materio)
- Grade (kiwango cha ubora)
- Application (In use)
- Packaging (uhifadhi wake)
- Quantity (Uwingi)
- Shipping Terms (namna ya usafiri)
- Target Price (Bei uliyopanga) HII NI MUHIMU SANA

2. Fanya Kuhakiki (Evaluation)
Mara zote unapoongea na muuzaji wa kichina ( supplier ) jaribu kuhakikisha vitu vingi tu nje na mbali ya bei ambayo watu wengi wao wanaangalia sana hii na kukosea kuto kuangalia vitu vingine. Jaribu kufirikia kwa namna hii
- Je wanajibu message zako kiusahihi na kwa wakati ) Are they responsive?
- Je wanauliza maswali yanayoendana na nini unataka katika bidhaa yako au wanakupa tu maelezo ya bidhaa zao?
- Je wanapicha za bidhaa unazozitaka wewe?
- Je mnaweza fanya mawasiliano kwa kuwapigia calls, whatsapp call au skype?
- Je wao ni watengenezaji au wao ni kampuni ya kuuza na kununu ( Manufactures Vs Trading company) Hii tutaiongelea siku zijazo
- Je wanatoa maelezo kiuwazi au kuna vitu wanaficha kuuliza?
- Nchi zipi sana wanauza hiyo products zao? Hii ni kubwa sana kwasababu hii inaweza kuonesha ni UBORA gani ambao hawa wanatengeneza.


3. Mazungumzo zaidi ya Biashara (Negotiations)
Wachina wanamsemo unasema “一分钱一分货” “Yi fen qian Yi fen huo” maana yake "unapata unacholipia"
Hii inamaanisha sio kila wakati ufanye manunuzi ya bei ya chini chini sana, mara nyingi bei za chini na ubora wa bidhaa huendana sana.

Wakati unapokua unaongea na wauzaji wengi kwa wakati mmoja unapotaka biadhaa jaribu kuweka mahusiano ya muda murefu unapoengea nao na useme " unataka biashara ya muda mrefu sio biashara ya siku moja tu" kwahiyo ni vizuri kutengeneza urafiki nao ( Hii ni mtazamo wa biashara wa kichina)

Pointi ya kubeba, hata kama una haraka vipi at least ongea na wauzaji zaidi ya 3 kujua vizuri bei ya bidhaa unayoitaka.

Pia Jaribu kuulizia Bei za bidhaa zako zikiwa na uwingi tofauti, kwasababu katika ulimwengu wa wachina uwingi ndiyo kila kitu . Unaweza uliza bei ya piece 5,000 na Bei 50,000 ukakuta gap lililopo ni kubwa sana. Katika mazunguzo zaidi, usisahau kuongelea bidhaa kuwa nyingi.

4. Hakikisha Kimtandao (Online Research & Due Diligence)
Sio kila king'aacho ni almasi, Yes ni kweli sio kila muuzaji wa kichina ni wa kweli, hakikisha unapitia maelezo yake vizuri kuogopa kuibiwa na kudanganywa mtandaoni. Yes watu wanaibiwa kila siku na kila saa kwa wauzaji wapo kwenye mitandao ya kina alibaba. Kwa teknolojia ya photoshop na kuedit vitu, hata vijana wa chuo wanaweza weka profile zao kwenye alibaba na kuuza.

5. Uliza Sample (Sample)
Baada ya kuona huyu supplier ni mzuri na unaweza kumuamini kwa kiwango kikubwa, na bei nakila kitu kimekamilika, wakati mzuri wa kuomba Sample.

Hapa hatuongelei imani tu kwa kuamini kwa macho, omba SAMPLE utumiwe uone. Sample inaweza tumia siku 5-12 kufika kwa DHL, Fedex na wengine lakini ni vyema zaidi ya kuanza kutengeneza vitu vyenye uwingi mkubwa na vikawa tofauti na unachokihitaji.

6. Pokea Sample (Evaluate Sample)
Ihakikishe sample yako kama ipo sawa na kile unachokihitaji, kama unataka kubadirisha na kufanya design yako pia ni muda sahihi wa kufanya hivyo.

7. Purchase Order (P.O)
Unaponunu kitu chochote kwenye mtandao wa alibaba au platform ya China au hata kwa mikataba ya uso wa uso hakikisha unakua na Purchase order ambayo itakulinda kwa siku za usoni. HAKIKISHA Purchase order inakua na maelezo yote unayotaka kuanzia

8. Payments
Unapofanya malipo ya aina yoyote kwanza kabisa hakuna 100% inalipwa bila kupata kitu chochote upfront.
Hakuna standard inayosema lazima ulipe 30% advance payment na baadaye ulipe 70% hii ni imekua kama kawaida lakini kuna wauzaji ( supplier) wanataka 50% advance na 50% kabla hawajatuma kwa meli.

Unaweza kuongeza zaidi na mnaweza kubadirisha mawazo namna mnavyotaka iwe.

Usikubali kutuma kwa njia ya Western Union, mara nyingi 98% ni utapeli. Kwa order ya aina yoyote hakikisha unafanya Bank Transfer.

DIRTY TRICK: HAKIKISHA MPOKEAJI WA PESA NA JINA LA USAJILI WA KAMPUNI AU KIWANDA VINAFANANA. KAMA HAIFANANI HII NI BENDERA NYEKUNDU KABISA KUNA MCHEZO UNAWEZA FANYIKA WA UTAPELI ( KUA MAKINI)

9. Usafirishaji (Shipment)

Inashangaza kwamba watu wananuna kontena na kontena, lakini hawakagui mzigo kabla haujasafirishwa kutoka China kuja Tanzania. Nimesikia case sio moja ni zaidi ya tano watu wanaagiza A wanapokea Z ( wanapokea tofauti na wanachoagiza). Hakikisha unafanya ukaguzi kabla mizigo yako haijaondoka kuanza safari kuja Tanzania.

Kuna makampuni ya ukaguzi ambayo yanafanya hii, lakini mengine yanakua na deal na viwanda kuwaandikia report kua mzigo ni sawa japokua ni mzigo mbovu. (Kuwa makini)

Baada ya kufanya ukaguzi ndiyo unaweza kuruhusu mzigo kuondoka na kuja sehemu husika.

Kiufupi hii ni namna unaweza kufanya unaponunua bidhaa kutoka China.

Kama unataka wasiliana nami unaweza nitafuta kwa number +255627637767

Karibu Pia ofisini kwangu Mikocheni, Hekima Garden kwa maelezo zaidi.

Asante.
 
  • Katika list ya forwarding company ongeza hii " ComGateway"
  • Iko safi zaidi - ukilinganisha na myusu.com
  • Tena wana application yao ya android inayokuwezesha kufanya ulinganifu wa bei toka masoko tofauti tofauti.
  • Iko salama zaidi, hakuna charges zilizojificha, Kujiunga ni free JZHOELO
 
Last edited by a moderator:
  • Katika list ya forwarding company ongeza hii " ComGateway"
  • Iko safi zaidi - ukilinganisha na myus.com
  • Tena wana application yao ya android inayokuwezesha kufanya ulinganifu wa bei toka masoko tofauti tofauti.
  • Iko salama zaidi, hakuna charges zilizojificha, Kujiunga ni free JZHOELO
comgateway.png

Hapo kwenye red sijaona sababu ambayo inawaonesha ubora wao zidi ya myus.com
Infact mm myus.com niewatumia na ndo nawaamini kwa maana wana ship mzigo wako hata kama umefuria nafikiri hii ni feature ambayo mm nilipenda kati ya zote...
Juzi wamenitumia email wakinambia kuwa wameanza pia kupewa discount kutoka kwa DHL na FEDEX hivo huduma itakuwa bomba zaidi...

Naomba kujulishwa hiyo yako ina kipi kipya kumzidi myus.com
 
Hapo kwenye red sijaona sababu ambayo inawaonesha ubora wao zidi ya myus.com
Infact mm myus.com niewatumia na ndo nawaamini kwa maana wana ship mzigo wako hata kama umefuria nafikiri hii ni feature ambayo mm nilipenda kati ya zote...
Juzi wamenitumia email wakinambia kuwa wameanza pia kupewa discount kutoka kwa DHL na FEDEX hivo huduma itakuwa bomba zaidi...

Naomba kujulishwa hiyo yako ina kipi kipya kumzidi myus.com

Hawa myus.com wanatuma kwa njia ya posta?
 
  • Nimetumia huduma za kampuni zote mbili
  • Nilianza na myus mwezi March na comgateway mwezi July [ screen shot zinajieleza ]
# Kitu ambacho sikupenda upande wa myus ni kuwa hawana option ya kufanya malipo kwa njia ya Paypal, Makato yao huwa ni automatic toka kwenye kadi yako.
# Kama account yako haina fedha na huna mpango wa kuitumia tena waweza kuwaliza - Nadhani hiki ndicho kimekuvutia zaidi
Infact mm myus.com niewatumia na ndo nawaamini kwa maana wana ship mzigo wako hata kama umefuria nafikiri hii ni feature ambayo mm nilipenda kati ya zote...
>> Hilo ni kweli iwapo account yako hana kiasi cha fedha cha kutosha, ila ukiweka tu fedha wanachukuwa chao - Kama lengo ni kupata huduma bila ya kulipia basi kwa point hii myus inakufaa
# Kitu nilichopenda upande wa comgateway.
  • Waweza tumia Paypal kufanya malipo
  • Kwangu mimi - hupendelea kufanya malipo kwa paypal na si kwa kutumia kadi, Huwa naamini niko salama zaidi
  • Mteja uamuzi ni wako ni wakati gani ufanye malipo ili mzigo wako utumwe
  • Cost yao kidogo ni nafuu ukilinganisha na myus.
vs1.png

VS
vs2.png


Hapo kwenye red sijaona sababu ambayo inawaonesha ubora wao zidi ya myus.com
Infact mm myus.com niewatumia na ndo nawaamini kwa maana wana ship mzigo wako hata kama umefuria nafikiri hii ni feature ambayo mm nilipenda kati ya zote...
Juzi wamenitumia email wakinambia kuwa wameanza pia kupewa discount kutoka kwa DHL na FEDEX hivo huduma itakuwa bomba zaidi...

Naomba kujulishwa hiyo yako ina kipi kipya kumzidi myus.com
 
Kupokea hela Tanzania lazima utumie US Mastercard Services ambazo ku sign up tu unapata 25$ lkn payout ni mpaka ifikie 100$
Na hela ya kutoa hela ATM za mastercard ni 1% ya hela unayo cashout
Na kwa mwaka unalipa 25$ za service kutumia service yao ambayo iko fair iwapo hiyo acct itakua inakuingiza hela nyingi
Maelezo zaidi angali Chati niloweka chini

Hiyo sio shida faida yao ni nn hawa jamaa?

1.Unafanya maombi ya BURE ya Master Card ambayo inakua ya US kupitia hapa US Mastercard Services
2.Maombi yanachukua mda kidogo lazima uwe mpole kabla hawajakukubalia
3.Wakiyakubali maombi yako utatumiwa Master card yako kupitia FEDEX/DHL
4.Hatua ya pili uta activate card kwenye website yao
5.Baada ya hapo fungua PayPal account kisha weka details za Master card uliyotumiwa
6.Kishautakua unalipwa na kupokea malipo bila shida yoyote
5.Lakini bei zao kutoa hela katika ATM yoyote e.g NBC,CRDB,BARCKLAYS,STANBIC e.t.c makato yao ni kama ifatavyo


ItemPrice (USD)UnitHow Applied
Card Account
Annual Account Maintenance$29.95Per yearFrom available balance - each year
Card Replacement$12.95Per cardOne Time - when issuing a replacement card
ATM/Cash Withdrawals or Transactions *
ATM Withdrawal or POS/Bank Teller Cash Disbursement$3.15Per TrxWhen withdrawal or disbursement is requested
(*surcharge may also be applied by your ATM/POS service provider)
ATM Decline Fee$1.00Per TrxWhen withdrawal request is declined
(*surcharge may also be applied by your ATM service provider)
ATM Balance Inquiry Fee$1.00Per TrxWhen ATM balance inquiry is made
(*surcharge may also be applied by your ATM service provider)
 
Mwl.RCT upo sahihi kabisa ku charge hela direct kutoka kwenye account yako sio secure na hainipi amani
Hiyo ndo weakness yao kubwa na by so saying huko sahii kwa asilimia fulani kuwa comgateway ni bora zaidi
Ntawajaribu kwa vitu cheap ndo ntawaamini na ntajua shipping rates zao ila kwa sasa nakomaa na myus.com

Sasa wakuu mnisaidie mm sijawai fanya malipo yoyote Amazon ila sasa nataka laptop lkn hiyo laptop haiuzwi na Amazon wenyewe inauzwa na mtu tu mwingine feedback score yake iko poa japo hiyo laptop haijawai kupewa REVIEW na mtu yeyote(maana yake haijawai nunuliwa na mtu yeyote)
refund policy zao vp?

Basi naomba kujua hawa jamaa refund policy zao zikoje na vitu gani ni muhimu kuwa makini navyo

cc JZHOELO

amazon in general ni nzuri kwa upande wote, amazon inanipa kujiamini maana wao hawatumii paypal kama substitute wa kufanya payment,wao wanatumia direct deduction from your account na humlipi muuzaji direct bali unalipia amazon kwenyewe then amazon watamlipa muuzaji baada ya kuwatumi shipping bill,pia amazon unaweza kufungua claim au kesi na ukawa refunded DIRECTLY in your account kaka, amazon by far ni most expensive market kwa upande wa sellers,yaani kujisajili amazon kama muuzaji ni gharama na ukipewa reviews mbaya amazon wanakufungia shop account yako kama seller,hii ndio imepelekea amazon kuwa trusted zaidi marekani na kote zaidi hata ya ebay. amazon wana kitu inaitwa A-Z guarantee, usiwe na wasi wasi kabisa bwana njunwa wamavoko in amazon you are super safe mkuu chukua mzigo wako tu na utakufikia in time na as it is described. nilinunua tab iliyokuwa inauzwa na mtu sio amazon wenyewe ,ilikuwa termed used like new na kweli nilivyoifungua ilikuwa just as described.. pitia hii link pia kaka link- http://www.amazon.com/gp/help/customer/display.html?nodeId=537868
 
Hii mifumo bado pia ingefafanuliwa zaidi kwa njia ipi ni mzuri na salama kwa mtu ambae yupo wilayani kupata (huduma) mzigo wake kupitia hizi services DHL,Fedex na usps.

mkuu inategemea na mahali ulipo,ila DHL ipo almost mikoa yote,hivyo kama upo wiliyani unaweza order tu,ukifika DHL watakupigia simu kuwa mzigo wako umewasili na watataka ukauchukue. nadhani kama umeuagiza nje ya nchi haitokuwa ngumu kuchukua usafiri kufuata mzigo wako mkuu.DHL wanaweza kukuletea mpaka mlangoni kwako ila wilayani ni mbali na huwa hawatoko nje ya mji.FEDEX wapo sehenu chach na USPS ni posta hivyo naamini wilayani masanduku yapo na utapokea mizigo yako palepale posta mkuu.
 
amazon in general ni nzuri kwa upande wote, amazon inanipa kujiamini maana wao hawatumii paypal kama substitute wa kufanya payment,wao wanatumia direct deduction from your account na humlipi muuzaji direct bali unalipia amazon kwenyewe then amazon watamlipa muuzaji baada ya kuwatumi shipping bill,pia amazon unaweza kufungua claim au kesi na ukawa refunded DIRECTLY in your account kaka, amazon by far ni most expensive market kwa upande wa sellers,yaani kujisajili amazon kama muuzaji ni gharama na ukipewa reviews mbaya amazon wanakufungia shop account yako kama seller,hii ndio imepelekea amazon kuwa trusted zaidi marekani na kote zaidi hata ya ebay. amazon wana kitu inaitwa A-Z guarantee, usiwe na wasi wasi kabisa bwana njunwa wamavoko in amazon you are super safe mkuu chukua mzigo wako tu na utakufikia in time na as it is described. nilinunua tab iliyokuwa inauzwa na mtu sio amazon wenyewe ,ilikuwa termed used like new na kweli nilivyoifungua ilikuwa just as described.. pitia hii link pia kaka link- Amazon.com Help: A-to-z Guarantee Protection

Mkuu sha place order ila inaonesha hela haijakatwa maana kwanza hela ilikua haitoshi maana mm niliweka kiasi in terms of 1$ is equal 1700TZS...Sasa wakadai kuna Taxation hivo dollar ikapanda mpaka 1776TZS lakini order nime place...Sasa hii inakaa je? watanikata hiyo hela saa ngapi?
Nasema hawajanikata hela sababu wakikata hela natumiwa message kwenye simu yangu na message ilokuja ilionesha USD 0.0...
Order ipo active kabisa wanasubiri seller a-ship mzigo maana wanadai mzigo ana ship 3-4days baada ya order kuwa placed
saada hapo inakaa je?
 
Mkuu sha place order ila inaonesha hela haijakatwa maana kwanza hela ilikua haitoshi maana mm niliweka kiasi in terms of 1$ is equal 1700TZS...Sasa wakadai kuna Taxation hivo dollar ikapanda mpaka 1776TZS lakini order nime place...Sasa hii inakaa je? watanikata hiyo hela saa ngapi?
Nasema hawajanikata hela sababu wakikata hela natumiwa message kwenye simu yangu na message ilokuja ilionesha USD 0.0...
Order ipo active kabisa wanasubiri seller a-ship mzigo maana wanadai mzigo ana ship 3-4days baada ya order kuwa placed
saada hapo inakaa je?

Njunwa inabidi wakukate hiyo pesa the moment unaweka order yako ili iwe ready for shipment after those days,kisha ndo wakutumie email au notification kwenye account yako kuwa mzigo umetumwa na ETA ya kufika kwenye address yako.. jaribu kuangalia kiwango chako cha pesa na ile total cost ya amazon,raha ya amazon wanakuconvert wenyewe na ile total inaweza kuandikwa in terms of tsh.hivyo hakikisha na ujaribu tena kama still pesa iko bank...pia network yetu bongo si unaijua tena..jaribu kisha utaona tu payment inatoka kwenda amazon.
 
Njunwa inabidi wakukate hiyo pesa the moment unaweka order yako ili iwe ready for shipment after those days,kisha ndo wakutumie email au notification kwenye account yako kuwa mzigo umetumwa na ETA ya kufika kwenye address yako.. jaribu kuangalia kiwango chako cha pesa na ile total cost ya amazon,raha ya amazon wanakuconvert wenyewe na ile total inaweza kuandikwa in terms of tsh.hivyo hakikisha na ujaribu tena kama still pesa iko bank...pia network yetu bongo si unaijua tena..jaribu kisha utaona tu payment inatoka kwenda amazon.

Hii Bank naiaminia hawana mambo ya "System down" nasema hawajanikata sababu hata hela yenyewe ilikua haijatimia maana mm nili estimate kwa 1700 ila wao wakasema ni 1776TZS

Katika soma soma yangu nimebaini kwamba kitu kama kinauzwa na Amazon prime basi hela haikatwi mpaka Initiation ya Shipping process

Ila kwa third part sellers basi either utakatwa Automatically on the instant una place order au baadae

Mm seller wangu yupo hii category ya third party ila nimeamua nim contact nione kama order yangu iko valid for shipment au laa!

Pia baada ya ku place order seller kabadilisha status ya hiyo laptop na kasema "Item unavailable"

Go thru this it can be helpful

http://www.amazon.com/gp/help/customer/display.html?nodeId=773768
 
Hii Bank naiaminia hawana mambo ya "System down" nasema hawajanikata sababu hata hela yenyewe ilikua haijatimia maana mm nili estimate kwa 1700 ila wao wakasema ni 1776TZS

Katika soma soma yangu nimebaini kwamba kitu kama kinauzwa na Amazon prime basi hela haikatwi mpaka Initiation ya Shipping process

Ila kwa third part sellers basi either utakatwa Automatically on the instant una place order au baadae

Mm seller wangu yupo hii category ya third party ila nimeamua nim contact nione kama order yangu iko valid for shipment au laa!

Pia baada ya ku place order seller kabadilisha status ya hiyo laptop na kasema "Item unavailable"

Go thru this it can be helpful

Amazon.com Help: Proceed to Checkout

Aisee ni kweli kabisa,nimekuelewa mkuu. shukran sana nilikuwa najua each payment ni imediate transaction inafanyika kumbe order ni tofauti mkuu hapa nimeelewa sasa..so inabidi usubiri mpaka item ikiwa available ndio wachukue pesa na kuship.sawasawa mkuu.
 
Back
Top Bottom