Guys nmecheki kwenye shipping calculator kwa baadhi ya sites zilizotajwa hapo juu ni gharama sana kuship even a package ya 0.5 kg, mfano Comgateway gharama ya kuship 0.5kg ni around 77 USD
Ghalama ndio changamoto kwa hizi kampuni za USA, maaana wanatumia Volumetric weight (W*L*H) sambamba na uzito halisi wa kitu

Nimeanzisha hii huduma, ya kusafirisha mizigo kama wafanyavyo myus, comgateway, usaddress n.k

Mimi natumia uzito halisi wa kitu kukokotoa ghalama ya kusafirishia, na sio volumetric weight, hivyo ghalama kuwa ndogo

na hizi ndio ghalama zangu.

Mfano:
a) 0.1 - 0.5kg Gharama ya kusafirisha ni USD 15
b) 0.6 – 1kg Ghalama ya kusafirisha ni 27.14 USD
c) 1.1kg – 1.5kg Gharama ya kusafirisha ni 38.94 USD
d) 1.6kg – 2kg Gharama ya kusafirisha ni 50.74 USD

Utaongeza USD $7.5, kwenye viwango tajwa hapo juu, kama my service charge.

Ghalama za kusafirishia utalipa baada ya mzigo kuondoka nchi husika, iwe ni DUBAI, USA, UK, CHINA, JAPAN, GERMAN, THAILAND n.k, Pia waweza kuwasiliana nami na kuomba ulipie ghalama za shipping baada ya mzigo kufiaka Tanzania.

Je nini unatakiwa kufanya.

1. Wasiliana nami ili nikupe ADDRESS yako ya nchi husika - mfano DUBAI, USA, UK, CHINA, JAPAN, GERMAN, THAILAND n.k

2. Anwani nitakayokupa ndio utajaza kama shipping address yako katika website kama AMAZON, 6PM nk

3. Nitakupa (a) ghalama ya kusafirisha mzigo na (b) tracking number ya mzigo pindi mzigo umepokelewa na unasafirishwa toka Nchi husika kuja Tanzania.

4. Mzigo wako utaupokea DSM wewe mwenyewe au nitapokea na kukutumia mahala ulipo - kama upo mkoani

Mawasiliano
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: +255 (0) 625 955 137 au 0784 496 856
2. Barua Pepe (Email): mw1rct @ outlook.com
3. Whatsapp: +255 784 496 856
4. Skype: mw1rct
5. Telegram: @mw1rct au 0784496856
6. JF PM
- Thread ya rejea: www.v.ht/buy4me
 
Asante ndugu kwa elimu yako nilikitamani kitabu fulani nikashindwa jinsi ya kukinunua lakini kwa muongozo huu naweza jaribu.Nikishindwa nitarudi kwako kwa muongozo zaidi.
Vp mdau umefanikiwa kununua icho kitabu mana mm nina shida na kununua vitabu pia
 
Vp mdau umefanikiwa kununua icho kitabu mana mm nina shida na kununua vitabu pia
Kitabu chochote unachohitaji naweza kukufikishia TZ kutoka AMAZON(.com au .co.uk au .in)

Vitabu havina tozo la kodi pindi uingizapo hapa nchini

Ghalama ya kukusafirishia ni US $15 iwapo uzito wake ni chini ya uzito 500g, na ghalama yake ya usafirishaji ni US $27.14 iwapo uzito wake ni kati 501gm hadi 1000gm
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?


Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao:
watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop US Stores and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT

Kuna kitu nimeagiza lakini sijapitia hizo njia za maajenti, nimelipa on line na nimejaza adress yangu, ndio mara yangu ya kwanza kufanya haya manunuzi, je itanifikia kweli mkuu?
 
Kuna kitu nimeagiza lakini sijapitia hizo njia za maajenti, nimelipa on line na nimejaza adress yangu, ndio mara yangu ya kwanza kufanya haya manunuzi, je itanifikia kweli mkuu?
Mzigo utakufikia. Iwapo umetumia address sahihi. Na iwapo muuzaji anatuma kuja Tz

Karibu
 
Weka tracking number kwenye moja ya hizi link.

Link 1:
TrackingMore - All in one package tracking tool

Link 2:
http://41.59.0.101:1120/tracking/

Nimetruck imeniletea hivi mkuu
6f1f1cdeca78baf831da220423fe9d07.jpg
956b65c395d230d6d08af8a71bb350eb.jpg
efd813595a5de131abbc5c93c7aacea1.jpg
 
Kinachokuunganisha Amazon na comgateway ni shipping adress/Billing Adress

Comgateway wanakupa adress ya US ambayo utaijaza kwenye Amazon account

Mzigo utasafirishwa kuja Hiyo Adress ya comgateway na baada ya hapo comgateway watasafirisha kwa adress yako ulo wapa wakati wa usajili
Asante sana kwa maelezo mkuu ata mm nilikuwa naanza kufuatilia nilipofika hapa ikawa changamoto
 
Back
Top Bottom