Jifunze namna ya kulainisha viganja au mikono

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Moja ya hasara ya mwanamke aliye hodari na kazi za nyumbani ni viganja vya mikono kuwa vigumu au vikavu.Kama unafua na maji na sabuni,kuosha vyombo,kusafisha nyumba,kubadili watoto nepi au diapers,kupika n.k . usishangae kuwa na viganja vigumu au vikavu.

Hakuna haja ya kuogopa na toa wasiwasi hii ni aina ya kufanya mikono yako iwe laini na ya kuvutia.Huna haja ya kwenda kwa spa’s wala kwa wataalamu.Baada ya kazi zako fanya haya;

Kunywa maji kwa wingi na kisha tumia njia hizi zifuatazo;
Chukua container weka chumvi kiasi.
Weka olive oil ndani ya container.

Weka sabuni ya maji ya kuoshea mikono, tumia aina unayoipenda inaweza kuwa anti-bacterial au yoyote ya maji. Ni vizuri kutumia sabuni ya maji sababu hautaosheka vizuri mkono sababu maji na mafuta hayachanganyiki.

Kausha mikono yako vizuri, kisha weka mchanganyiko huo kwenye viganja vyako kiasi cha ½ kijiko cha chai kisha sugua pole pole. Sugua ndani na nje ya viganja na ndani ya vidole na kucha.

Osha kwa maji ya uvuguvugu .
Kausha mikono kwa kutumia taulo kavu.
Pakaa lotion ya mikono .


AU

Osha mikono na maji ya uvuguvugu na sabuni kuondoa grease na bacteria.kisha kausha na taulo kavu.
Chukua sukari vijiko viwili(2) vya chai na olive oil pia vijiko viwili(2).

Pakaa mikononi kwa pamoja haraka .
Sugua mikono yote kwa pamoja ndani na nje kwa kutumia mchanganyiko huo.


Osha mikono kwa maji ya uvuguvugu.

Tumia rose water pia nzuri .
Kisha pakaa lotion ya mkononi.

Waweza tumia pia sunflower oil na hata mafuta ya nazi pia mazuri.

TIPS
  • Usifanye mara moja ukategemea matokeo ya kudumu au milele.
  • Tumia baby oil au lotion kabla ya kulala.
  • Tumia lotion zinazotengenezewa na mimea zaidi.
  • Acha lotion kwa dakika kumi(10)kwenye viganja,ile layer ya juu ya ngozi itanyonya lotion na italoki moisture ndani ya ngozi.Fanya hivi mara mbili(2) kwa wiki.
  • Vaa gloves au plastic wakati unafanya kazi kama kuosha vyombo au gardening.
  • Tumia Vaseline.
Kwa mikono mikavu zaidi unaweza kulala na gloves ukiwa umepakaa lotion.


Usiache mikono kwenye maji baridi kwa muda mrefu,huondoa mafuta na unyevu wa asili mikononi.
Kuwa muangalifu na aina ya lotion utayotumia kuepusha athari za allergies.
 
Miss Zomboko, kwa kutumia chumvi sio haikaushi ngozi zaidi kweli?!

Sukari hata kwenye lips wanashauri kutumia kwa kuzilainisha zaidi, ukichanganya na Vaseline.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Na pia, baada ya kuosha mikono ni vizuri kukausha kiasi, kisha weka lotion au cream wakati ngozi ina maji mpaka ikauke. To lock in the moisture.
Na sio mikono pekee, hata mwili mzima.
 
Miss Zomboko, kwa kutumia chumvi sio haikaushi ngozi zaidi kweli?!

Sukari hata kwenye lips wanashauri kutumia kwa kuzilainisha zaidi, ukichanganya na Vaseline.
Chumvi haipaushi kwa sababu unakuwa umeichanganya na mafuta. Angalia hata wali ukipikwa kwa chumvi bila mafuta na pale unapopikwa kwa chumvi na mafuta unavyokuwa
 
  • Thanks
Reactions: kui
Back
Top Bottom