JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Taarifa hizi zinaweza kutumika kufuatilia vitu anavyofanya na kupendelea mtu anapokuwa mtandaoni. Aidha, ifahamike kuwa taaifa hizi zikisha wekwa mtandaoni husalia hapo kwa muda mrefu napengine zikawa ni za kudumu. Data hizi zinajumuisha mambo yote unayoyafanya uwapo mtandaoni, kama vile mambo unayoandika, picha zako, video na miamala unayofanya
Uzi huu umelenga kukufahamisha kuhusu hizo Digital Footprint ili uweze kuzidhibiti na pengine kuzipunguza
Njia kubwa ya ukusanyaji wa hizi nyayo za kidigitali ni kwa kupitia kitu kinaitwa Cookies ambazo hujumuisha eneo ulilopo, kifaa unachokitumia, vitu unavyopenda kuvitafuta, tovuti na mitandao unayotembelea, aina ya kifaa unachotumia, browser unayoitumia, eneo ulilopo, barua pepe, bamba ya simu, picha zako na taarifa nyingine nyingi unazoziweka wewe au wanazoweka wengine.
Digital footprint zinaweza kusema nini kuhusu wewe?
Inashauriwa na inapendeza ukiwa na nyayo za kidigitali zilizobeba taarifa chanya kukuhusu kwasababu taarifa hizo ndio hubeba uwakilishi wa wewe ni nani hasa katika mitandao. Ikitokea Mtu akakutafuta au akatafuta jina lako basi apate taarifa chanya kukuhusu
Digital footprint zinaweza kutumika kuamua hatma yako katika nyanja mbalimbali za Maisha. Mfano: waajiri wanaweza kuzitumia kuamua kama wakuajiri au la, wasimamizi na watekelezaji wa sharia wanaweza kuzitumia, unapoomba Visa ya kuingia taifa tofauti na lako zinaweza pia kutumika kuamua kama upewe au unyimwe. Kuwa makini…
Je, kuna aina ngapi za Digital Footprints?
Nyayo za hiyari za Kidigitali | Active digital footprints
Hizi hujumuisha taarifa zote ambazo unaziacha wewe mwenyewe kwa kujua pale unapotumia majukwaa na tovuti mbalimbali. Kwa mfano kila unachokiandika na kukiweka kwenye kurasa zako za mitandao ya kijamii hubaki na hutambulika kama Nyayo hai za Kidigitali | Active digital footprints
Hapa nimeweka mifano ya Active Digital Footprints.
- Unapoweka maudhui kwenye Facebook, Instagram, Snapchat, Twitter, na mitandao mingine ya kijamii
- Kujaza fomu za mtandaoni na kukubali uwe unatumiwa taarifa kwa njia ya emai kwa jumbe fupi kupitia simu
- Unapokubali kuweka Cookies kwenye kifaa chako pindi unapoulizwa na mtoa huduma kupitia Browser yako.
Nyayo zisizo za hiyari za Kidigitali | Passive digital footprints
Hizi ni digital footprints ambazo zinachukuliwa kutoka kwako bila ya kujua lengo lake ni nini na bila ya wewe kujua kama zimechukuliwa
Kwa mfano: Kuna tovuti zinachukua taarifa za utembeleaji wako katika tovuti husika na kuziweka kama kumbukumbu kuhusu wewe. Mchakato huu umefichwa na ni wa siri. Matokeo yake taarifa zako hutumika kwa ajili ya matangazo na tafiti mbalimbali
Hapa kuna mifano kadhaa ya passive digital footprints.
- Tovuti zote ambazo zinakusanya cookies kutoka kwenye kifaa chako bila ya kukutaarifu
- Application na tovuti zinazotumia Location bila ya kukutaarifu
- Watangazaji kupitia mitandao ya kijamii. Watu wengi hupokea matangazo kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu walivyotafuta kwenye mitandao tofauti na sehemu waliyopokea tangazo. Mfano: Umetafuta kitu kupitia Google lakini wanapokea matangazo kwenye Instagram
1. Ingia kwenye Search Engen kama vile Google, Bing, Start Page au DuckDuckGo kisha search jina lako. Angalia matokeo yanasema nini kuhusu wewe? Je, yamejazwa taarifa chanya? Aidha, unaweza kuset kwenye google kila linapoandikwa jina lako basi wewe unapata notification ili uweze kujua nini kimeandikwa kuhusu wewe ili kama si taarifa chanya uweze kufuatilia uondoaji wake.
Jinsi ya Kuset : How to Set up Google Alerts (and Use It to Grow Your Business)
2. Angalia upya settings zako za faragha kwenye kifaa chako na browser na application unazozitumia. Hakikisha hazikusanyi taarifa zako kama location, namba ya simu, picha na videos
3. Tengeneza Nywila / passwords imara, hii itakusaidia kulinda vifaa vyako na kuepusha akaunti na kifaa chako kuingiliwa na wahalifu wa mtandaoni wanaoweza kuiba au kuchafua digital footprints zako
4. Hakikisha software na applications zote ziko up to date. Hii itasaidia kuongeza usalama zaidi na kukuepusha na hatari za mtandaoni.
5. Jijengee utamaduni wa kukagua kila unachokiandika na kukifanya mtandaoni hii itakusaidia kujijengea taswira nzuri na yenye manufaa kwako