JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Uvaaji wa barakoa au “mask” ni moja ya njia za kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza. Katika kudhibiti kusambaa kwa Virusi vya #Corona
Barakoa inapaswa kuvaliwa endapo unakohoa au kupiga chafya, mtu wa karibu yako ana dalili za #COVID19, uko kwenye mikusanyiko ya watu au muda wote kama ugonjwa umeshatapakaa kwenye jamii
Matumizi ya barakoa yaende sambamba na kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka. Barakoa si mbadala wa kunawa mikono
Barakoa ivuliwe na kutupwa mara tu inapoloa au masaa 4 yakipita. Barakoa za kutumiwa mara moja zisitumiwe zaidi ya hapo
Barakoa ivuliwe kwa kushikwa kwenye nyuma (kwenye kamba) na kutupwa kwenye eneo la taka lililo na mfuniko au mbali na makazi ya watu bila kushika eneo la katikati ili kuepuka kuhamisha maambukizi
Mikono itakaswe kwa maji tiririka na sabuni au kitakasa mikono mara baada ya kutupa barakoa kabla ya kufanya jambo lolote
NI WAKATI GANI NATAKIWA KUVAA BARAKOA?
Wataalam wanaeleza kuwa Virusi vya Corona vinaenea kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa mwingine pale mmoja wao anapokuwa amepata maambukizi
Mtu mwenye maambukizi anaweza kumuambukiza mwingine pale anapokohoa, kupiga chafya na majimaji yatakayomtoka muathirika na kumrukia Mtu mwingine
Maelekezo ya Uvaaji wa Barakoa;
Vaa Barakoa: Unapolazimika kwenda kwenye maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi. Aidha, kama huna sababu ya kwenda maeneo haya unashauriwa kukaa nyumbani kwako
Vaa Barakoa: Watu wenye maambukizi pia wanashauriwa kuvaa Barakoa ili kuwalinda wengine dhidi ya maambukizi ya #COVID19
Vyanzo: WHO na John Hopkins Medicine