Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

Attachments

  • 1431102012683.jpg
    1431102012683.jpg
    23.8 KB · Views: 551
Last edited by a moderator:
Haiwezekani hicho kinachotokana na ingredients ulizozitaja kiitwe 'mkate wa sembe' wakati ngano ni 50% na sembe 50%, halafu 'sembe' inatoa ugali na 'ngano' inatoa mkate. Hivyo huo sio mkate wa sembe bali ni mkate wenye sembe ndani yake kwa maana ngano ndio inafanya uitwe mkate.

Kwa kifupi huko ni kula ugali wenye ngano ndani yake, na kama unauzwa madukani na mahotelini ni wizi mtupu.

Mhh...
 
Habari za jioni wapendwa. Za masiku kadhaa?

Mahitaji:
Unga sembe glass 1
Unga ngano glass 1
Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo)
Maziwa glass 1
Mafuta 1/2 glass
Mayai 4
Iliki iliosagwa 2tbs
Bp 2tbs

Jinsi ya kupika:
Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe.
Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.

Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.

Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.

Picha zinagoma ...

Umenikumbusha mbali sana, bi mkubwa alikuwa akiupika huu lakini yeye akitumia unga wa dona tu na tuliuita MKATE WA DONA. Miye hupenda lile tandu (sijui kama ni sahihi kuliita hivyo kama la wali) lake la juu hasa.
Asanteee...upishi mpya huu ntajaribu in shaa Allah
 
Upo huu hupikwa kwa sembe tupu. Hua unakorogwa tu km uji na tui la nazi na ingredients zengingine ukishakua mzito huokwa.
 
Mrs kharusy na ule unasongwa si mkate wa sembe pia? Nliwahi kumuona mama akimpikia wifi yangu alikua mjamzito aliutamani ila ni mtamu sana unakua kama brown hivi.

Huu unausema ww jaan ndo wenyewe haswaa unawekwa hadi mdalasini...very tasty hauchanganywi na ngano huwa..
 
Je, badala ya kuweka sembe, ukaweka dona inakuwaje? Mimi naupa jina 'mugate' kwa maana ya mchanganyiko wa mkate na ugali ambavyo ni ingredients kuu (50% each).
 
upo huu hupikwa kwa sembe tupu. Hua unakorogwa tu km uji na tui la nazi na ingredients zengingine ukishakua mzito huokwa.
basi mie nlokuwa naujua ni huu. Na sukari yake huunguzwa kama ya puding. Unakolezwa na spices. Mkate nlikuwa naupenda huu. Kwa wiki lazima niupate mara 3 au hata 4 kula.
 
Habari za jioni wapendwa. Za masiku kadhaa?

Mahitaji:
Unga sembe glass 1
Unga ngano glass 1
Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo)
Maziwa glass 1
Mafuta 1/2 glass
Mayai 4
Iliki iliosagwa 2tbs
Bp 2tbs

Jinsi ya kupika:
Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe.
Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.

Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.

Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.

Picha zinagoma ...

Hiyo ni cake au mkate? wingi wa sukari na mayai unaondosha hilo jina na hivyo kuwa keki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom