Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

Discussion in 'JF Chef' started by gfsonwin, Dec 24, 2012.

 1. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  Haya jamani leo ni siku nyingine ambayo ninataka tupike mkate kwaajili ya familia.

  Mkate ni chakula ambacho huliwa wakati wa kufungua kinywa.hupikwa kwa kutumia unga wa ngano ama wa muhogo lakin huwa na kiasi kukubwa cha wanga na hivyo unapotumiwa kama kifungua kinywa hukusudiwa kumpatia mlaji nguvu na joto mwilini.

  Sasa tuangalie jinsi ya upishi wa mkate.
  Mahitaji:
  a) unga wa ngano kg 1 (kwa familia yenye watu wengi let say 4)
  b)hamira gm 50
  c)mayai 4
  d) chumvi kijiko kimoja cha chai
  e)sukari nijiko 2 vya chakula
  f) maziwa fresh robo l500 ml kama unauwezo kama la basi tumia maji.

  Namna ya kupika
  1) chekecha unga wa ngano kwenye chekeche ili kuondoa particles kubwa pamoja na kuingiza hewa ndani ya chembe za unga.

  2) weka hamira chumvi pamoja na suukari kisha koroga kwa mkono hadi uchanganyike vizuri kabisa.

  3) koroga mayai yako 4 pembeni kwenye bakuli kisha mimina koroga yachanganyike ndipo uyamimine kwenye mchanganyiko wako uyachanganye kwa mikono.

  4) Weka maziwa kwenye mchanganyiko wako na kisha ukande unga kwa vidole vyako hadi ulainike uwe kama wa kupikia chapati. hakikisha wakat unaukanda usizidishe maji manake kadiri unga unavyozidi kuumuka ndivyo unavyozidi kuwa laini. wakati wa kukanda kunja vidole vyako vinne na uvitumie kukandia unga usitoboe unga kwa vidole kwani hautaukanda zaidi ya kuutoa hewa tu.

  5) Chukua chombo chako cha kukokea kipake blue band kwa ndani kisha kata unga kwa size ya chombo chako na uutengeneze kwa umbo la tin yako ndipo uuweke. kama huna baking tins za mkate waweza kutumia hata tin ya cake ila uzikate kwa maumbo ya mstatili. kama nacho hiki huna basi tumia sufuria yako ipake blue band ukate unga kwa umbo la viduara uueke ndani visiwe vikubwa sana yawe na umbo dogo la wastani tu.

  6) Washa oven yako kwa nyuzi joto 120 dk kabla, kisha weka chombo chako cha kuokea na funga mlango. subiria baada ya dk 30 mkate wako utakuwa umesha iva. ii kujua kama umeiva vizuri chukua kitu chenye ncha kali choma kwenye mkate basi kile chombo kikitoka kikavu jua mkate wako uko tayari.

  Zima jiko na toa mkate wako nje uweke pakavu ili upoe. kumbuka kwamba mkate kwa ajili ya afya hufaa uliwe siku moja baada ya kuokwa. hapa ahauwa na ladha nzuri zaid na huwa umesha lainika vya kutosha. usiufunike mkate wako kama bado haujapoa usije ukajaa mvuke. na usiuweke kwenye unyevu.
  mkate huu waweza kuutumia kutengenezea sand wich ama kuliwa jinsi ulivyo tu.

  haya basi nawatakieni mapish mazuri kwa ajili ya sikukuu ya x-mass na mwaka mpya.

  mke mwezangu AshaDii nakuomba uwaekee ile picha ya mkate tunayopikaga nyumbani kwajili ya chai

  ==================
  Kutoka kwa Mdau
  ==================

  "Chibudee

  MKATE WA MAYAI

  Vipimo

  Mayai 4
  Sukari ¼ Kikombe
  Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula
  Hiliki ya kusaga ½ kijiko cha chai
  Baking powder ½ Kijiko cha chai
  Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, iliki na vunja YAI MOJA BAADA YA JENGINE KWENYE KIBAKULI KANDO NDIPOSA UMIMINE KWENYE BAKULI KUBWA LA SUKARI
  2. Changanya sukari, iliki na mayai kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.
  3. Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto au makaa..kwa watumiao makaa…
  4. Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari.
  5. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge. Na kupunguza madonge..chunga unga wako kwa tungio…
  6. Mimina unga ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.
  7. waweza kuweka karatasi kwa ndani ya sufuria umbo la mduara au kama ni baking tray umbo la mraba kwa kuipakia mafuta ili mkate usishike unapotaka utoa baadae.
  8. Ingiza sufuria ndani ya jiko (oven) na oka kwa dakika 20 au 30 vile vile makaa ya chini yawe kiasi tu kuliko ya juu ya mfiniko.
  9. Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
  10. Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.


  [​IMG][​IMG]

  =====================================
  =================================
  ==========================================
  ==========================================
  =================================
  =====================================
  Threads nyingine zinazohusu ujuzi na utaalamu wa mapishi mbalimbali ya mkate.....

  1. Mkate wa ufuta
  2. Mkate Wa Sinia - Mkate Wa Kumimina Aina Ya Kwanza
  3. Naan bread
  4. Jinsi ya kupika mkate wa haba soda
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa hizi recipe unazotumia tena mbele ya baba nanihii wakati wa maandalizi hadi uokaji ndoa yako lazima idumu.
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,696
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  gfsonwin usinyime mkate kama utaoka kweli. Afu huyu AshaDii na wewe uke wenza wenu uko vipi? Na Mume wenu ni nani?

  Na kama mtu akitaka kuwaposa wote inakuwaje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  sasa wewe nenda kampikie mama Thanda leo tena uschelewe saa 12 tu rudi home anza kazi keso asbh mtakunywa chai tamu kweli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  nitaoka mkate wa sikukuu mchana wa leo. sasa ngoja nifanye mapema nikuletee wa moto uone jinsi ulivyo mtamu.
  mie na AshaDii tumeolewa na Kaizer.hatuolewi tena kwani mwanamke hanaga mitala.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  jamani hivi wadada wote wa humu jamvini sio wapish?? mbona jukwaa halina watu hili?? wakati nilijua ndo sehem ya kwanza watu wote kuingia lol!

  sasa mie naanza kuwavuta mmoja baada ya mwingine hadi mje mpike mkate khaa1
  haya Smile, Preta, Kongosho amu ( ooh wewe unaumwa pole mwaya), King'asti tena wewe unapendeleaga sana kula sandwich njoo hapa folen za shop rite zipungue, Zion Daughter, Ciello, lara 1 sio kila siki nyie na mmu tu hao washefa mtawapikia nn ama ndo kuwalisha junky foods za migahawani?? snowhite sio wewe na miiko tu njoo ujfunze mapish mapya aatii cacico sio kila siku folen city bakery njoo ujifunze hapa upike mwenyewe, Paloma, BADILI TABIA Juliana Shonza sio unakalia majungua tu njoo ujifunze kupika. na wengine woote njooni

  tueni mwanamke anasifiwa mapish na usafi toopppppppppp!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Mdogo wangu gfsonwin mkate huu hapa nimeleta.... Kuna lingine dear?

  [​IMG]
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  ewaaa! umeona enh..........dada mkubwa! asante sana kwa hilo sasa watu wajionee wenyewe.
  BTW mbona wadada wa humu jf hawapendi kupika?? tuwaanzishie mpango kabambe wa kuwavuta kupika .
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Alafu nimeona hapo juu Superman anataka kuleta posa... Utanipa feedback umeamua vipi! Maana kama wewe unaondoka hata mimi nitaondoka, siwezi tena maisha bila uke wenza... :becky:

  Usisahau kumkaribisha na chai yetu ile ya special recipe kunywea huu mkate wako mtamu.. Lol.


  [​IMG]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Umegungua eeeh? Tuwe tunawakaribisha siku moja moja weekend nyumbani kwetu waone namna gani kupika kumeongeza ukaribu na upendo ndani ya familia... Tena basi tuna bahati mume wetu siku moja moja weekend hutu grillia nyama ama samaki... We are so lucky! Lol

  Tena mabingwa wa utegezi kwa kupika ni Husninyo, Zion Daughter, FP , Smile, Ciello, Madame B na Arabela. Afadhali hata ya Mwali, Michelle, Preta, Zinduna na charminglady.. Hivi lara 1 anajua kupika kweli? Napenda nijue.. Kuna kakangu kampenda na anapenda kula! ha ha ha!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 48,767
  Likes Received: 18,903
  Trophy Points: 280
  Mmh? Upendeleo na ubaguzi huu sasa.....

  BTW unaifanyia promo Blue Band au? Nikitumia Tan Bond au siagi nyingine mkate utageuka kitumbua au?

  Huku Torabora Blue Band haifiki, tutakoma tunaopenda mkate.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,318
  Likes Received: 1,843
  Trophy Points: 280
  Yaani unitake radhi kabisaa. Mie sinunui kitafunwa hata siku moja, kila siku ni home made fresh produce.
  Napenda sana fresh bred kwa kweli, harufu tu inanichanganya. Mie napika xmas cake, cha ajabu sipendi icing sugar. So hata bday cakes huwa sitii icing.

  Kitu nilichochemsha ni kupika mkate wa mchele na vitumbua. Wifi AshaDii aliahidi kunisaidia practice manake nshapewa recipe, namngpjea siku akipata neema hiyo.

  Nb: usisahau kutupia sesame seeds juu na kublaze na yai ama blueband
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  nimemkatalia mie nishazoea maisha yetu pamoja sasa ta utengano siyawezi kabisa.
   
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  thats ma gal............ napenda wewe mm acha tu.
  kuhusu kupika mkate wa mchele najua dada AshaDii atakusaidia kama akikosa muda nitakuja kukuonyesha utaufurahia sana tu. mie muda mwingine hata sultanas huwa naweka kwenye mkate hivyo huleta ladha nzuri sana lol!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  basi dada wakati huu tukiwa vacation tujitahd kuwavuta waje wajionee wenyewe ili wasilale tu bali wadumishe upendo na furaha ya familia kwa kuwapa chakula kitamu kuliko wote!
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160

  Shem nakusalimu... Kwa mkate mkono wa kulia (uliopikwa na gf) na Chai mkono wa kushoto (iliyopikwa na mimi). Natumaini ushafanya maandalizi mema ya Xmas. This year mimi gfsonwin na baba watoto nasikia tunaispend kwako. Katika vinywaji usisahau Amarula... :smiling:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  hapana sina maana hiyo kwenye blue band. binafsi nimeitaja kwani ndio ambayo naitumia kwenye mapish yanau mengi ila kwa mwenye kupenda tan bond ama kcc anaweza kutumia sio mbaya.

  BTW nataka nikupikie uji wa maziwa ya mtindi na siagi utapenda kuuonja??
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  mke mwenza hiyo itifakai ya salam hapo juu mie sina nyongeza.
   
 19. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #19
  Dec 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160

  Kipenzi wifi yangu tatizo wewe toka tumeongezeka ndani ya familia unatoa kila sababu kutofika home hadi unamfanya gfsonwin asikujue vizuri... Uwe unakuja saana kama zamani. Mdogo wangu ako so loving... Hili hata baba watoto Kaizer atakuambia. ha ha ha!

  Vitumbua nitakuja na nanilihuu tukwelekeze... usijali kabisaaaa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hahahahahah mnanisema mm nn????
   
Loading...