Jifunze mambo yanayosababisha ushindwe kufanya jambo kwa viwango vikubwa

Dec 17, 2022
73
43
Habarini,

Ningependa tujifunze baadhi ya makosa tunayoyafanya,na husababisha tushindwe kufanya mambo kwa viwango vikubwa.

Ningependa kutumia kitabu cha ONE THING. Kitabu kinachoelezea kuwa umuhimu wa kufanya mambo kwa mpangilio.

Suala ni kwamba wote huwa tuna malengo,ila malengo au ndoto zetu huwa zinakuwa na plan B. Kuwa na plan B sio vibaya ila ni endapo kama utaitumia plan B kupata jawabu la plan A.

Wengi huwa tuna malengo, lakini mwisho wa siku kila tukishindwa huwa tunajikuta tunahamia mpango wa pili. Na endapo kama mpango wa pili ukifeli, huwa tunahamia mpango wa tatu.

Mwisho wa siku tunakuwa sio watu tunaoweza kukamilisha jambo.Yaani tunakuwa watu wa kurukaruka kwenye kila mpango.

Nakumbuka moja kati ya bilionaire aliwahi kusema ili uweze kutimiza mpango wako vizuri. Hakikisha huweki plan B. Unajiambia nifanye jambo hili au nisifanye kabisa.

Jaribu kufikiria ni mipango gani ulijiwekea? Je, uliweza kuitimiza,bila ukacha mpango wowote? Ukijua unapohitaji kwenda basi utaweza kufika unapopahitaji.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom