Jifunze: Mahaba

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,442
Nataka kukutia moyo wa kuendelea na ndoa yako hata kama imejaa matatizo namna gani.

Kitu cha msingi cha kuangalia ni kutokufa moyo na kusonga mbele.

Imani niliyonayo ni kwamba ikiwa unataka kuifanya ndoa yako kuwa sehemu ya amani, hakika inawezekana. Hakuna lisilowezekana.

Mchawi mkubwa wa ndoa ni wewe mwenyewe angalia kwa makini kauli yako, angalia kwa makini matendo yako. Kuna watu wengine wana visasi. Ukiwa hivi ni ngumu kuwa na ndoa nzuri.

Wakati fulani huwa najikuta natokwa na machozi namna baadhi ya watu wanavyofanyiana mambo yasiyo mazuri katika ndoa.

Utakuta baadhi ya wanaume wamebaki uanaume jina, lakini kimatendo sifuri; mfano utakuta hatimizi majukumu ya nyumbani. Wanaume wengine ni wapumbavu, haijali familia.

Ndugu zangu wanaume naomba tukubaliane kwamba tunapaswa kuelewa hata kama mkeo ana kazi au hana kuna mambo mnapaswa kuendelea kupeana.

Eeeh bwana mimi sijui ni mara ya mwisho lini ulimnunulia mkeo "kufuri" ni nguo ndogo, lakini haileti raha mtu kujinunulia mwenyewe.

Vivyo hivyo kwa mwanamke. Mnapaswa kuonyesha kujaliana. Ni kweli wengi tunapenda furaha katika ndoa, lakini tunapaswa kuelewa kuwa furaha hutafutwa, haiji yenyewe.

Sio tu kufuri, kuna wanaume wengine hawanunulii nguo wake zao hivi wewe ni mwanaume wa namna gani? Unatia aibu.

"Mwaka wa mwisho kuninunulia nguo ni 2005, yaani hata upande wa khanga hajawahi kuninunulia," analalamika mwanamke mmoja mkazi wa Moshi.

Mwanaume badilika bwana. Mwanaume unapaswa kujua hata mavavi ya watoto wako. Baba yeyote ambaye hawajibiki kwa mkewe au watoto, huyo ni mpumbavu.

Kuna wengine wanatelekeza watoto, eti kwa sababu wamegombana na wake zao. Huu ni ujinga, kwani mtoto kosa lake nini? Ndugu zangu hapa duniani tunapita, tuache roho mbaya.

Mwanaume amka, wajibika kwa familia yako. Hata kama kuna kasoro katika ndoa, imani niliyonayo ni kuwa zinaweza kuondolewa, cha msingi ni kukaa chini na kuangalia wapi ulikosea, kisha chukua hatua.

Inasikitisha sana kusikia baadhi ya wanaume hawajui hata watoto au familia yake imekula nini au inavaa nini.

Ndoa yoyote ambayo watu wake hawawajibiki ni vigumu sana kuwa na amani. Duniani kote inajulikana kuwa mwanaume ni kichwa, lakini kuwa kichwa sio kitandani tu, eeh bwana yakupasa kuwajibika, usikwepe majukumu.

Hata kama imetokea mume umezaa nje ya ndoa, huna sababu ya kumtelekeza mtoto, msaidie awe na maisha kama wengine.

Acha kuwa mbaya, timiza wajibu wako kama baba, wafanyie wengine yale ambayo wewe ukifanyiwa utajisikia raha.

Kuwajibika kwingine ni katika raha, eeeh bwana maana kuna wanaume wamekuwa ni watu wa kujipendelea sana. Nyumbani anaacha fedha ya kununua chapatti, yeye anakwenda kula chai na mayai, supu nk, hii si haki. Mwanaume bora ni yule ambaye anaipenda nyumba yake, yuko tayari asile, familia yake ishibe.

Kuwajibika kwingine ninakotaka kuzungumzia ni umuhimu wa kuwa karibu. Hata kama uko mbali na mwenzi wako, hakuna ubaya kuwasiliana japo kwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Acha kuendeleza kinyongo, hata kama mligombana.

Vivyo hivyo kwa wanawake, wanapaswa kubadilika, kuna wengine hawajipendi kama walivyo baadhi ya wanaume. Wengine ni maarufu wa kusengenya wanaume zao kwa watu wengine.

Ndugu zangu kama ndoa ina tatizo sawa hakuna ubaya kuomba ushauri, lakini ubaya ni kutangaza mabaya eeeh maana mwingine labda mwenzi wake ana kasoro fulani anatangaza vibaya kwa wengine. Tangaza na mazuri basi?

Wengine katika suala la mahaba, hadi ubembeleze weee kama unaomba kibarua. Acha kuwa hivyo, uliingia kwenye uwanja mwenyewe, cheza, acha kuwa kero kwa mwenzi wako.

Watu wanaingia katika ndoa kusaka furaha, kwa hiyo inakuwa ni kosa kubwa kuonekana ni mwenye kero. Inakuwa ni mbaya kuonekana ni mtu ambaye huwajibiki kwa yale ambayo unapaswa kuwajibika nayo.

Kuna wanawake wengine wamekuwa na marafiki wabaya, marafiki ambao kwa mfano wanawashawishi kuwa na wapenzi wengi na mambo mengine yasiyofaa kama haya.

Je uliolewa au kuoa ili uwe kero kwa mwenzio? Je ni kweli unaona ni sahihi kuwasikiliza zaidi wengine zaidi ya mwenzi wako? Maana kuna wengine wamekuwa wakiwajali zaidi marafiki au ndugu badala ya wenzi wao. Hali hiyo inapoingia kwenye ndoa ni hatari, ndoa ni kusikilizana. Hakuna kusikilizana, hakuna ndoa.

Ndoa nzuri ni mke kutenga maji ya kuoga kwa mumewe, kutenga chakula kwa mumewe, lakini pia ndoa nzuri ni ile ya mume kufanya haya, hasa wakati ambao mke hawezi, mfano anaumwa nk au siku tu ambayo ataamua kufanya.

Hakuna ubaya siku baba anaingia jikoni na kupika, kisha anawapakulia watoto na mkewe. Ni njia nyingine nzuri, lakini isiwe kila siku itapoteza heshima fulani kwa jamii na hata familia kwa sababu sio utamaduni wa mwafrika mwanaume kupika au kutenga chakuka.

Ninachotaka kusisitiza katika mada hii ni umuhimu wa kuwajibika;wajibika kwa kutenda haki, wajibika kwa kuwatendea wengine ambayo wewe ukitendewa utajisikia raha, wajibika kwa kuonyesha kumjali mwenzi wako, wajibika kwa kuzingatia kuridhishana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom