Natoa huduma za Website and Mobile Application Development

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
1,072
2,307
Price yangu ni affordable na ya makubaliano.

Nina Business Centric Approach, yenye lengo ya kuipush idea yako ifanikiwe kwenye market ikiwemo na ushauri wa bure jinsi gani inaweza fanikiwa.

Technologies ninazotumia;
1. Laravel (version 6 up to 8)
2. Vuejs(Version 2 up to 3)
3. Database(Mysql)

Kwa upande wa Mobile development;
1. React Native and Expo.

CSS frameworks;
1. Tailwindcss
2. Bootstrap

Web na app nitakayo kutengenezea zote zitatumia modern technologies zilizo kwenye soko hivi sasa. Kwangu Web ni SPA.

Kama ukiwa interested call 0748333586.
 
Pia natoa ushauri wa kitaalam kuhusu Web na App technologies free kwa walio interested
 
Pia natoa huduma ya Website Modifications kwa upande wa frontend na Backend pia

Kama una Website ambayo unataka Ku improve muonekano wake au Ku add baadhi ya new Features...

Usisite kuni check....0748333586
Mda wote nipo available
 
MAHITAJI
  • Laptop au Desktop yenye Window Operating System(Version 10)
  • Internet Connection
  • Uelewa mdogo wa lugha ya kingereza
  • Unapenda au unatamani kujua Web Design


MANENO YA MSINGI (KEY TERMINOLOGIES)
  • Website
    is the collection of two or more webpages connected by hyperlinks
    MAELEZO:
    Website ama tovuti ni mkusanyiko wa web pages (kurasa za tovuti) zilizounganishwa kwa kutumia Hyperlinks
    Neno "Hyperlinks" lisikutishe ni "links" hizi hizi tunazotumiana.Kwa maana ya hapo juu Website ama tovuti ni muunganiko
    wa web pages mbili au zaidi.
    Kwa Mfano, www.jamiiforums.com ni webisite ambayo inaweza kuundwa na mamia au maelefu ya Web pages kulingana na ukubwa wake
    Unaweza tazama Website kama kitabu kilichoundwa na kurasa nyingi (Web pages) na gundi zilizotumika kuunganisha hizi kurasa pamoja ndiyo "Hyperlinks"

  • Web Page
    Web page is document written in HTML
    MAELEZO
    Web page, hii ni document inayoandikwa kwa kutumia HTML
    Tukirudi kwenye "analogy" au mfano wetu wa kitabu,HTML ndio kalam inayotumika kuandika kurasa zetu
    NOTE: Neno "Document" na "File" huwa yanatumiwa na watu wengi kama maneno yenye maana sawa
    Japo kuna tofauti,File huwa halina aina maalum ila tuna aina tofauti tofauti za document
    Na aina ya document husika huwa tunaitambua kwa kutumia extension
    Ushakutana na file kwenye Computer yako au Simu lenye jina kama "photo.jpg" au "movie.mp4" au "audio.mp3"
    Yote ni ma files kwenye computer yako lakini kila file hapo lina aina yake,moja la picha , moja la video na lingine la audio
    .jpg , .mp3 ,na .mp4 hizo ndio tunazoita extension....
    Extension ndio zinazotuwezesha kujua file lipi ni la aina gani,then tukalifungua kwa kutumia Application inayo deal na aina hio ya file

    So Web page pia ni document, na kwakua zinaandikwa kwa kutumia HTML basi extension yake ikapewa jina la .html
    So document ya web page inaweza kuwa na jina kama hili "index.html" au "home.html"
    index na home ni majina tu ya documents zetu yakifatiwa na .html extension

    Kama VLC Media Player ilivyo na uwezo wa kusoma documents zenye extensions za Mp4 (Video) au Mp3(Audio)
    Web Browsers zina uwezo wa kusoma documents zote za HTML (Yaani documents zenye extension ya .html)


  • Web Browser
    Web Browser is application that can access,read,nterpret Web Pages and return the defined Layout to the users screen
    Example of browsers are Google Chrome,Microsoft Edge,Safari,FireFox,Opera na bibi kizee Internet Explorer
    MAELEZO:
    Web Browser ni application kama ilivyo VLC media Player ila hii ni special kwa ajiri ya kutumia,kusoma na kutafsiri Web Pages,kisha
    Baada ya kazi hizo,Browser inarudisha Muonekano wa hizo Kurasa au Web Page kwa mtumiaji

    Najua mambo yashaanza kuchanganya hapa,Twende Taratibu
    Tunaposema "Browser ina soma na kutafsiri hizi Web Pages" tuna maana gani?
    Ni hivi,hizi Web Page huwa zinaandikwa kwa kutumia HTML kama Tulivyoona hapo Juu
    Turudi kwenye mfano wetu wa kitabu,kurasa za kawaida za vitabu huwa tunaanda kila kitu sisi wenyewe
    Tutataka juu ya kurasa yetu kuwe na kichwa cha habari yaani HEADING , chini yake kuwe na kifungu cha maneno
    yaani PARAGRAPH chini ya PARAGRAPH kuwa na PICHA etc

    Lakini tunapoandika kurasa za tovuti,badala ya kuandaa Muonekano wa kurasa yetu sisi wenyewe kama tulivyofanya
    Kwenye kurasa za kawaida hapo juu,tunaanda maelekezo ambayo Browser sasa inakuja kuyasoma na kuyatafasiri kisha
    inatengeneza muonekano wa kurasa yetu kupitia yale maelekezo tuliyoipa......

    Haya maelekezo ya jinsi gani kurasa ya tofauti yetu ionekane (Layout) ndio tunayooita HTML Codes.....
    Codes kwenye Computer Science ni maelekezo ambayo tunaipa Computer au Software ya Computer (Mfano Browser)
  • HTML
    Stands for Hypertext Markup Language, is the language used to write a web page
    MAELEZO
    Kama tulivyoona hapo Juu HTML ni lugha tunayotumia kuandika kurasa zetu za Web pages..
    Na tunachoandika ndani ya kurasa hizi ni nini?
    Ni mkusanyiko wa maelezo (HTML Codes) ya jinsi gani tunataka kurasa yetu ionekane kwa mtumijai...
    Browser ita soma na kutafsiri haya maelekezo ili kuunda muonekano tuliyoutaka kwenye kurasa yetu,
    Muonekano huu ndio unaorudishwa kwa mtumiji.....
  • URL
    Stands for uniform Resource Locator
    This defines the location of specific web pages in the internet
    Eg.https://www.jamiiforums.com , Jifunze Leo Web Design (HTML ,CSS,TAILWINDCSS)-Beginners etc
    MAELEZO
    URL ndio inayotupa maelezo ya wapi ilipo kurusa fulani ya Website
    Tukirudi kwenye mfano wetu wa kitabu,URL ni kama namba za kurasa yetu,so tunaweza jua kwa urahisi wapi
    kurasa iliyo kwa kutumia nambari ya huo ukurasa
    Mfano URL kama hii JamiiForums ni location ya Home Page ya jamiiforums......
    So haijalishi Jamiiforums ina web pages nyingi kiasi gani,tukitaka kwenda kurasa yake ya nyumbani tunatumia tu hio URL kufika
    Pia haijalishi Jamiiforums ina posts milioni ngapi tukitaka kwenda kwenye kurasa yenye huu uzi tunatumia URL hii

    So URL ni kama nambari katika kurasa zetu za tovuti
    NOTE(Baadae tutajifunza kuhusu URI(Uniform Resource Identifier) lakini kwa sasa sio ya muhimu kwenye Lecture hii

  • Internet
    is network of all computers system in the world
    MAELEZO:
    Internet ni muunganiko unao unganisha Computers zote duniani
    Tukirudi kwenye mfano wetu wa kitabu.....Internet ni kama Maktaba inayobeba Vitabu vyote duniani
    (NOTE huu mfano wa kitabu nautumia kuelezea concept tu)
    Pia watu wengi wanapenda kutumia neno "Internet" na "www" kama maneno yenye maana moja hapana...

  • WWW
    is the information system where by HTML documents with their URLs can be accessible over the internet
    MAELEZO:
    WWW ni mfumo wa taarifa unaotuwezasha kupata hizi Webpages tunavyoperuzi mtandaoni wakati Internet ni
    Muunganiko wa System zote za computers duniani
  • IP Adress
    This is special format of number used to identify each device across the internet
    MAELEZO:
    IP Adress ni mfumo wa tarakimu unao tumika kutambua kila kifaa kinachotumia mtandoa wa internet
    Unaweza tazama IP Adress kama nambari za simu,kila mtumiaji wa simu ana nambari yake tofauti na mwingine
    Vile vile kwenye Internet kila kifaa kina nambari yake ya pekee hii nambari ndio inaitwa IP Adress

    Kwanini IP Adress?
    Ushawahi fikiria vipi kama kila mtu angekua na namba ya simu sawa na mwenzake?
    Au namba za simu zisingekua unique(za kipekee) kwa kila mtumiaji wa mtandao wa simu?

    Communication Error.......tungekuwa tuna mpigia JOHN anapokea AISHA
    Sasa kama ilivyo kwenye mitandao ya simu,kila kifaa kinachotumia mtandoa wa internet kina unique namba
    Thus why huwezi Click link ya jamiiforums ukapelekwa Wikipedia...
  • HTTP
    stands for Hyper Text Transfer Protocol is the protocol used to transfer data (web pages) over the internet
    MAELEZO
    Hii ni njia inayotumika kusafirisha hizi Web Pages,kwa kawaida tunakua na aina mbili za Computers
    (Ninaposema computer na include pia Simu yako ya mkononi,nayo ni Computer kwa tafsiri..)
    Tuna computer ya kwanza inayo omba kurasa fulani

    Mfano unapo click iliyokuvutia,maana yake umeomba kurasa (document) yenye huo uzi,lakini document hio
    haipo kwenye Simu au Laptop yako,ipo kwenye Computer nyingine ya mbali ambayo Jamiiforums wametumia
    kuhifadhi Web pages zao
    Sasa kiuhalisia,Computer yako (Simu au Laptop) inatuma maombi kwenda kwenye hio Computer ya mbali
    Kisha nayo inarudisha majibu kwa Computer yako kwa kuipatia Kurasa yenye huo uzi....
    Kwa kua Computer yako itakua na Browser,hii Browser itapokea hio documents ya HTML iliyoletwa
    itazisoma HTML codes zilizo ndani kisha itatengeneza kurasa kwenye screen ya mtumijai yaani hii unayoiona hivi sasa
    Huo mchakato wote unafanyika kufumba na kufumbua.....Maombi yanayotumwa na Computer ya mtumiaji tunayaitwa
    HTTP Requests na majibu yanayo rudishwa na Computer ya website husika tunaita HTTP Responses
    Computer ya mtumiaji tunaitwa Client na Computer ya Website husika tunaipata Server
  • Client
    is the computer that send HTTP requests to the client and waiting for responses
  • Server
    is the computer that host the particular website (24 hours ,7 days a week),receiving the HTTP requests and returning the corresponding HTTP Responses to the client
    NOTE: Server ni aina ya Computer ambayo mda wote ipo on na imeunganishwa na internet kwa ajiri ya kupokea na kujibu
    Maombi ya Client,thus why unaweza kufungua jamiiforums hata saa sita usiku

  • Client Server Architecture
    Is the model that describes how Server should provides resources or services to the clients
    Kama umeona jinsi gani mawasiliano katika internet yanavyofanyika,mda wowote unapotembelea tovuti fulani
    tunakua na Computers mbili zinazowasiliana moja ambayo ni Client inatuma maombi na nyingine ambayo ni Server
    ina respond
    Mpangilio huu wa Client na Server ndio tunaoita Client Server Architecture
    CLIENT SERVER ARCH.png
  • Domain Name
    is the special name (nickname) used by users to access your website
    MAELEZO:
    Tuliona kuwa kila Kifaa kwenye internet kina nambari maalum IP Adress inayokitambulisha
    Hii ina maana kuwa hata Server ya Jamiiforums inaweza kuwa na IP Adress ya nama hii
    67.43.14.98(Mfano tu)
    Ili kulipata mtandaoni tulitakiwa ku google hizo namba...

    Kwasababu ni vigumu kwa mtumiaji wa kawaida kukariri hizo namba,ndipo Domain name zilizokuja
    Kama wewe unapo save namba ya simu kwa kutumia jina la muhusika
    Badala ya kutumia IP Adress,mtumiaji inabidi apaswe tu kujua domain name ya website kisha Domain name itabadilishwa
    nyuma ya pazia na kuwa IP Adress husika.....kama ilivyo IP Adress domain names ni unique,kila website duniani ina domain name yake
  • DNS
    Stands for Domain name system,is the service that translate the domain names into IP Adressess
    MAELEZO:
    Hii ni huduma inayobadili domain names kwenda kwenye IP Adressess
    Hii ni kama Phone Book ya internet
  • HTTP VS HTTPS
    Tumeona kuwa HTTP ni mfumo au njia inayotumika kusafirisha Web pages kutoka kwa Server kwenda kwa Client
    au lugha nyepesi ni namna gani Client na Server zinazungumza
    Sasa fikiria wakati HTTP requests inatoka kwa Client na kwenda kwa server au wakati HTTP responses hapa inatoka kwa
    Server na kupelekwa kwa Client....hapa katikati yoyote anaweza kuzisoma hizo Requests na Responses kama Client na Server zikitumia HTTP kuwasiliana

    Website zinazotumia HTTPS zina alama ya kufuli kwa mbele
    not secured.PNG

    secured.PNG

    Ku solve hili tatizo HTTPS ikazaliwa....HTTP na HTTPS ni kitu kile kile isipokua hii s ya mwisho maana yake securedyaani mazungumzo kati ya server na client hayawezwi sikilizwa na mwingine
  • Search Engine
    is the software service designed to search website's contents
    Kama tunavyojua kuna Mamilion ya Website yenye mabilion ya taarifa,bila search Engine ingekua ngumu kutafuta
    chochote mtandaoni
    Mfano wa Search Engine ni Google,Baidu,Bing

    Mpaka hapo utakua na solid foundation ya Websites na jinsi gani zinafanya kazi
    Part ya hapa chini itakua Special kwa ajiri ya HTML codes

    Less talk,more codes

    HTML CODES.........


    contact 0748333586
 
HTML CODES -- LECTURE 02
Kama tulivyoona Lecture iliyopita,HTML ndio language inayotumika kutengeneza Web Pages
Na Web page ni just document yenye extension ya .html

Unakumbuka unapotaka kuandaa document ya Microsoft Word?,document ya Microsoft word huwa
unaiandika kwa msaada ya Software maalumu inayoitwa Microsoft word

Vile vile,hapa tunapotaka kuandika au kuandaa document yetu ya HTML huwa tunaifanya kwa msaada wa
Special software inayoitwa TEXT EDITOR

Text Editor - is software application that allows you to create,and edit text documents in your computer

Text Editor ni application inayoturuhusu kutengeneza na kuhariri text documents yoyote kwenye Computer zetu
Na simple na sio complicated kama ilivyo Microsoft Word.....
Na ninaposema "text documents" na maana ya kuwa documents yetu ita contain "plain text" , maneno tu

Sasa kabla hatujaanza kuandika HTML Codes.....
Inabidi tu install TEXT EDITOR kwenye Computer yetu
Sasa kuna aina nyingi za TEXT EDITOR zinazotumika ila my Favorite ni Text Editor moja inayoitwa Visual Studio Code

Link ya kupakua Hio Visual Studio ni hii hapa,Follow instructions sawa sawa utakazopewa na Visual Studio Code
itakua installed bila shida yoyote kwenye PC yako
NOTE:Kwenye hio link Chagua Version ya Visual Studion Code itakayoendana na Version yako ya Window au Operating system
Kwa window ni kwanzia Version ya 7,8 mpaka 10
Download Visual Studio hapa

Sitoweka kila hatua hapa(Ya ku download Visual Studio Code),ni rahisi tu lakini kama unahitaji muongozo
unaweza check pia hii Video kidogo


Baada ya ku install Visual Studio na kuifungua utakutana na Interface ya Namna hii
code.homeScreen.PNG


Kama kuna changamoto umepata kwenye ku install Visual Studio,let me know kwenye comments

VISUAL STUDIO CODE EXTENSION
Visual studio code inaturuhusu ku install plugins au applications ndogo ndogo zinazo rahisisha baadhi ya mambo
tunapotaka kuandika HTML documents zetu
Kabla hata hatujajua HTML ipo katika mfumo gani au ni language ya aina gani,hebu tu install kwanza hizi extension za Visual Studio
Code zitakazo tusaidia tutakapo anza kuandika HTML documents zetu

Hizo Extensions ni

  • HTML Boilerplate
  • Live Server
  • Browser Preview
  • Prettier - Code formatter

Kazi ya hizo extensions tutaiona tutakoanza kuandika Codes zetu za HTML lakini kwa sasa
Tuzi install kwanza kwenye Visual Studio code zetu

Follow hizi links ku install hizo extensions
Click Continue na Visual Studio ita install hio extension
 
Back
Top Bottom