Jifunze Kutengeneza wateja wako mwenyewe, Wateja ndio Msingi wa biashara yako

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,935
22,915
Unajua ujasiriamali ni Kitu pana yenye inahitaji elimu kila siku jinsi ya kui master na kujua nini ufanye na nini usifanye ili kuepuka kile watu wanaita HASARA,hamna mtu anapenda hasara kila mtu anafungua biashara ili apate faida na hii faida huwa huwezi kufungua tu droo ukakuta hela zimeongezeka,hii faida inaletwa na watu.

watu ambao sisi tunawaita wateja,unajua hamna biashara nzuri na tamu kama ile yenye wateja,ukiniuliza mimi biashara gani nzuri ya kufanya nitakujibu simple and short "biashara yeyote yenye wateja" hiyo ndio biashara ya kufanya na nzuri.

Mziki wake unakujaga sasa jinsi ya kuwapata hao wateja,hapa ndio panafanyaga sharobaro atembee peku,boss ajigeuze mfanyakazi kufanya kazi za wafanyakazi wake sio kwamba yeye hana kazi,au sio kwamba kakosa chakufanya ila yote hiyo ni Tafuta ya wateja.

Umeshawahi enda sehemu ukaingia ukashindwa gundua boss nani mfanyakazi nani? najua umewahi..Sasa basi huyo boss usifikiri yeye hana kazi zingine la hasha! kaamua kuuingia front ili kuzidi kunasa wateja akikaa chini akabweteka yule mteja akakosa huduma unafkiri atabaki? hapana lazima aondoke,sasa ili asiondoke ni lazima apate huduma na nani wakumpa hiyo huduma sasa kama wafanyakazi wote wako busy? ndipo BOSS anaaingia kati anaokoa jahazi ili asimpoteze yule mteja.

Tutoke huko kwenye mastory ya town!

SASA leo nataka niseme kidogo na wale iba iba,wezi wezi,macho kodo wa wateja wa wengine!

Unajua kila biashara ina ups and down mpk inafikia unaona biashara ya mtu wateja wanapishana kama wanaingia kukata ticket za kuingia taifa ujue yule mtu alisota,alivumilia,aliumia lakini hakukata tamaa alisimama na leo ndio hivyo unaona wateja wanapishana.

sasa kuna mtu mmoja kajibanza mahali baada ya kuona wateja wa mwenzake ni wengi,anaona hii ndio fursa sasa (kosa kubwa sana) Labda nitolee mfano Kuna sehemu kuna BAR imefunguliwa mpya,kufunguliwa tu yule mwenye bar kila week end analeta band,wanamuziki,wanatumbuiza so inapelekea wateja kwenda kwa wingi sana kwenye ile BAR.

sasa kuna kajizi ka wateja kamoja baada ya kuona wateja wanafurika kwenye ile bar anaona yes hapa hapa,kichwani mwake anakuja na Idea za biashara akilenga wateja watakua ni wale wale wa ile bar. Utamuona huyooo anakurupuka anaenda kuweka mpesa/tigo pesa pembeni ya ile BAR, utamuona huyooo anakurupuka anaenda kufungua saloon pembeni ya ile BAR,utamuona huyo kurupu kurupu anaenda fungua CARWASH pembeni ya ile BAR yaniiii ni fujoo kwa kwenda mbele.

wakishafungua hizo biashara zao sasa unajua kinachofuata ni nini? kwakua wao akili yao haikuwaza kutafuta wateja wao binafsi ila waliwaza kuiba wateja wa wengine ili waje wawe wao kinachofuata sasa...

Mwenye ile BAR anapata tatizo la kibinadamu ambalo mimi na wewe hatulijui,anayumba ki pesa ule uwezo wa kuleta band kila week end hana tena,ule uwezo wakuleta wasanii hana tena,BAR inapoteza mvuto,kasoro zinaongezeka na kwakua wateja wanapenda vitu vizuri huwa Woteeeee wanaanza ondoka mmoja mmoja,week end wateja walikua wanakuja 1000 taratbu namba inashuka 500 mara 300 mara 100 mara 50 Bar inabaki jina tu.

kasheshe linakuja kwa wale ndugu zetu kule nnje,utawasikia mkipishana huko njian anakwambia "Biashara ngumu ndugu yangu" utamsikia Biashara ya Tigo Pesa saivi haina hela kabisa,utamsikia akilalamika tu wateja hamna, Unajua kwann hawa watu wanalalamika? wanalalamika kwasababu vichwani mwao walijua Biashara ni MTAJI tu (ooh maskini) wakasahau biashara ni MTAJI + WATEJA.

Unapofungua biashara yako mahali lazima ujue wateja wangu ni kina nani? wanatoka wapi? nitadumu nao kwa muda gani? lazima ujiulize hayo maswali yote kabla hujafungua biashara yako.

Unakuta mtu anakwambia controla Nataka kwenda kufungua biashara paleeee,namuuliza wapi? ananiambia Pembeni ya ile shule pale kuna wanafunzi sana,yani nikifungua pale nitapiga sana hela unajua....

au mtu anakwambia Controla nataka kufungua biashara paleee nimepata eneo flani amaizing sana,namuuliza wapi hapo? anakwambia si pale kwenye lile soko Jipya,au si pale kwenye ile STAND MPYA yani ile stand ikifunguliwa ni hatari nakwambia kutakua na biashara sana.

Basi mimi huwa ni mtu wakumkodolea sana mtu macho anaponiambia kitu chake,muda wote huo ananisimulia mimi kimyaa namsikiliza tu,Moyoni namsikitikia sana kwasababu namuona Huyu kwenye biashara BADO SANA kuna kitu ana miss.

unajua ndugu zangu ukiona unataka kufungua biashara mahali halafu wateja wako unategemea wale wa eneo lile unaloenda kufanya biashara "My dear usifungue hiyo biashara" utalia tu siku 1.Trust me.

Shida sio kufungua biashara shule,shida sio kufungua biashara stand mpya,nk nk shida nii Wewe kutojua jinsi yakutafuta wateja wako permenent,tuache kudanganyika na wateja wa "msimu" tuache kudanganywa na wateja wanaokuja kama vipindi vya Mvua leo wapo kesho wapo,mtu anaenda fungua biashara pembeni ya shule,shue zikifungwa au serikali ikisema wanafunzi wabaki majumbani "mtu analalamika biashara mbaya".

Mtu anaenda weka biashara stand ikifika saa 12 jioni hamna hata mpita njia wa maana halafu analalamika biashara mbaya,siku ikifululiza kunyesha mvua siku nzima ndio kabisaa anapiga ukunga biashara mbaya,sasa unalalamika biashara mbaya wakati unajua kbsa eneo hili wateja wake wapo vipi..

Jifunze kujua unapata wapi wateja wako kabla hujafungua biashara yako mahali popote,kama unamezea mate wateja wa wengine tambua hutochukua round kwasababu biashara yako inategemea ufanisi na ubora wa biashara ya mwingine.

Mimi ni mtu nisietaka wateja wa msimu au wateja wa Muda tu,unakuta unafungua biashara eneo ambalo wateja wapo asubuhi - 12 jioni kwisha,au mtu anafungua biashara pembeni ya kanisa as if kila siku ni jumapili,yani kuna watu hawafikiriii kbsaaaaa.

Ili uweze furahia ujasiriamali/biashara yako Jifunze mbinu za kutafuta wateja,kuvuta wateja wawe wako,watu wengine ndio kupitia wewe walete huduma yani waje kwasababu wewe ndio soarce ya wateja sio wewe uende wakati wao ndio soarce (chanzo) usikubali.

Serikali ikifungua stand MTAA A hautoisha mwezi ule mtaa utakua na biashara nyingi sana,kwanini? kwasababu stand ni chanzo cha wateja,sasa usitake kwenda kufanya biashara mahali ambapo source ya wateja sio wewe (sijui naeleweka) kwasababu kwakufanya hivyo ikitokea serikali ikisema hii STAND ihame maana yake hata wale wateja uliotegemea nao watahama lakini wewe kiwa ndio chanzo cha wateja STAND ihame isihame,ije isije wateja wako watakua pale wapo muda wote.

Guys hivi naeleweka kweli?! namalizia kwakurudia tena kwamba Unapofungua biashara yyte hakikisha wewe binafsi uwe chanzo cha wateja eneo unaloenda kufungua,kama unajiona huwezi kuwa chanzo cha wateja huwezi sababisha wateja wakatokea ACHA HIYO BIASHARA UNAYOTAKA KWENDA FUNGUA ACHA.

inatakiwa uweze ku master kutafuta/kuzalisha wateja wako mwenyewe kwa asilimia 70% kisha hizi 30% acha ndio ziongezwe na mazingira yanayotuzunguka lakini kumbua 70% inatakiwa iwe wewe,na sio iwe vice versa.

wewe unaetaka fungua biashara pembeni ya shule,chuo,kanisa,stand,barabarani,nk Hii naomba uichukue na uipokee kama jinsi ilivyo ukiona haikufai iache hapa kisha endelea na plan zako usije sema hukuambiwa.

Biashara zote ni nzuri Guys Zoteeee kama tu Utajua wateja wako wanatoka wapi.
 
Ni biashara gani isiyofuata wateja yaan niogope kufungua biashara karibu na stendi kwenye wateja wengi kisa kuogopa ipo siku itafungwa ukiogopa risk kwenye biashara hutofanikiwa maana risk haziepukiki kwenye biashara ni wewe kuwa flexible tu
 
Nimeipenda hi..Nimeona jinsi Watu wanavyoshindwa kulipa mikopo na wanayumba Sana pale stand zinapohamishwa mfano Dodoma pale Jamatini.
Hapo bado wale wanaolia kwa kuvunjiwa Frem zilizo barabarani yani ukikutana nao ni vilio kwa kwenda mbele,wakati kwenye biashara unatakiwa ukihama,unahama na wateja wako,ukienda uchochoroni wanakufata

ukienda mafichoni wanakufata,ila hii mambo ya kudanganyana eti biashara ni "location" naonaga haina akili kabisa na waangalia location wakati wanapofungua biashara zao ndio hawa ambao stand zikihamishwa wanalia,frem wakipandishiwa kodi wanalia,yani they are weak ukitaka kuwaporomosha chini tu wahamishe pale walipo halafu utaona.

Watu hawajui tengeneza wateja permanent,watu wanafanya biashara hawana uhakika hata kama mteja flani atakuja au hatokuja hajui hata ana wateja wangapi na ratiba zao zakuja ofisini zikoje,hawajui.

Mtu anaenda fungua ofisi anasubiri wapita njia waje ndio wanunue bidhaa,sasa huyu mtu ana tofaut gani na machinga? tena heri ya machinga ana move,yeye hatembei kaganda kwenye frem yake anasubiri wateja asiojua wanakuja au hawaji,Ujinga mtupu.

Halafu utamsikia analalamika biashara ngumu,biashara haiendi,biashara hailipi,lawama chungu mzima wakati makosa na ugumu wote anajisababishia mwenyewe.
 
Unajua ujasiriamali ni Kitu pana yenye inahitaji elimu kila siku jinsi ya kui master na kujua nini ufanye na nini usifanye ili kuepuka kile watu wanaita HASARA,hamna mtu anapenda hasara kila mtu anafungua biashara ili apate faida na hii faida huwa huwezi kufungua tu droo ukakuta hela zimeongezeka,hii faida inaletwa na watu.

watu ambao sisi tunawaita wateja,unajua hamna biashara nzuri na tamu kama ile yenye wateja,ukiniuliza mimi biashara gani nzuri ya kufanya nitakujibu simple and short "biashara yeyote yenye wateja" hiyo ndio biashara ya kufanya na nzuri.

Mziki wake unakujaga sasa jinsi ya kuwapata hao wateja,hapa ndio panafanyaga sharobaro atembee peku,boss ajigeuze mfanyakazi kufanya kazi za wafanyakazi wake sio kwamba yeye hana kazi,au sio kwamba kakosa chakufanya ila yote hiyo ni Tafuta ya wateja.

Umeshawahi enda sehemu ukaingia ukashindwa gundua boss nani mfanyakazi nani? najua umewahi..Sasa basi huyo boss usifikiri yeye hana kazi zingine la hasha! kaamua kuuingia front ili kuzidi kunasa wateja akikaa chini akabweteka yule mteja akakosa huduma unafkiri atabaki? hapana lazima aondoke,sasa ili asiondoke ni lazima apate huduma na nani wakumpa hiyo huduma sasa kama wafanyakazi wote wako busy? ndipo BOSS anaaingia kati anaokoa jahazi ili asimpoteze yule mteja.

Tutoke huko kwenye mastory ya town!

SASA leo nataka niseme kidogo na wale iba iba,wezi wezi,macho kodo wa wateja wa wengine!

Unajua kila biashara ina ups and down mpk inafikia unaona biashara ya mtu wateja wanapishana kama wanaingia kukata ticket za kuingia taifa ujue yule mtu alisota,alivumilia,aliumia lakini hakukata tamaa alisimama na leo ndio hivyo unaona wateja wanapishana.

sasa kuna mtu mmoja kajibanza mahali baada ya kuona wateja wa mwenzake ni wengi,anaona hii ndio fursa sasa (kosa kubwa sana) Labda nitolee mfano Kuna sehemu kuna BAR imefunguliwa mpya,kufunguliwa tu yule mwenye bar kila week end analeta band,wanamuziki,wanatumbuiza so inapelekea wateja kwenda kwa wingi sana kwenye ile BAR.

sasa kuna kajizi ka wateja kamoja baada ya kuona wateja wanafurika kwenye ile bar anaona yes hapa hapa,kichwani mwake anakuja na Idea za biashara akilenga wateja watakua ni wale wale wa ile bar. Utamuona huyooo anakurupuka anaenda kuweka mpesa/tigo pesa pembeni ya ile BAR, utamuona huyooo anakurupuka anaenda kufungua saloon pembeni ya ile BAR,utamuona huyo kurupu kurupu anaenda fungua CARWASH pembeni ya ile BAR yaniiii ni fujoo kwa kwenda mbele.

wakishafungua hizo biashara zao sasa unajua kinachofuata ni nini? kwakua wao akili yao haikuwaza kutafuta wateja wao binafsi ila waliwaza kuiba wateja wa wengine ili waje wawe wao kinachofuata sasa...

Mwenye ile BAR anapata tatizo la kibinadamu ambalo mimi na wewe hatulijui,anayumba ki pesa ule uwezo wa kuleta band kila week end hana tena,ule uwezo wakuleta wasanii hana tena,BAR inapoteza mvuto,kasoro zinaongezeka na kwakua wateja wanapenda vitu vizuri huwa Woteeeee wanaanza ondoka mmoja mmoja,week end wateja walikua wanakuja 1000 taratbu namba inashuka 500 mara 300 mara 100 mara 50 Bar inabaki jina tu.

kasheshe linakuja kwa wale ndugu zetu kule nnje,utawasikia mkipishana huko njian anakwambia "Biashara ngumu ndugu yangu" utamsikia Biashara ya Tigo Pesa saivi haina hela kabisa,utamsikia akilalamika tu wateja hamna, Unajua kwann hawa watu wanalalamika? wanalalamika kwasababu vichwani mwao walijua Biashara ni MTAJI tu (ooh maskini) wakasahau biashara ni MTAJI + WATEJA.

Unapofungua biashara yako mahali lazima ujue wateja wangu ni kina nani? wanatoka wapi? nitadumu nao kwa muda gani? lazima ujiulize hayo maswali yote kabla hujafungua biashara yako.

Unakuta mtu anakwambia controla Nataka kwenda kufungua biashara paleeee,namuuliza wapi? ananiambia Pembeni ya ile shule pale kuna wanafunzi sana,yani nikifungua pale nitapiga sana hela unajua....

au mtu anakwambia Controla nataka kufungua biashara paleee nimepata eneo flani amaizing sana,namuuliza wapi hapo? anakwambia si pale kwenye lile soko Jipya,au si pale kwenye ile STAND MPYA yani ile stand ikifunguliwa ni hatari nakwambia kutakua na biashara sana.

Basi mimi huwa ni mtu wakumkodolea sana mtu macho anaponiambia kitu chake,muda wote huo ananisimulia mimi kimyaa namsikiliza tu,Moyoni namsikitikia sana kwasababu namuona Huyu kwenye biashara BADO SANA kuna kitu ana miss.

unajua ndugu zangu ukiona unataka kufungua biashara mahali halafu wateja wako unategemea wale wa eneo lile unaloenda kufanya biashara "My dear usifungue hiyo biashara" utalia tu siku 1.Trust me.

Shida sio kufungua biashara shule,shida sio kufungua biashara stand mpya,nk nk shida nii Wewe kutojua jinsi yakutafuta wateja wako permenent,tuache kudanganyika na wateja wa "msimu" tuache kudanganywa na wateja wanaokuja kama vipindi vya Mvua leo wapo kesho wapo,mtu anaenda fungua biashara pembeni ya shule,shue zikifungwa au serikali ikisema wanafunzi wabaki majumbani "mtu analalamika biashara mbaya".

Mtu anaenda weka biashara stand ikifika saa 12 jioni hamna hata mpita njia wa maana halafu analalamika biashara mbaya,siku ikifululiza kunyesha mvua siku nzima ndio kabisaa anapiga ukunga biashara mbaya,sasa unalalamika biashara mbaya wakati unajua kbsa eneo hili wateja wake wapo vipi..

Jifunze kujua unapata wapi wateja wako kabla hujafungua biashara yako mahali popote,kama unamezea mate wateja wa wengine tambua hutochukua round kwasababu biashara yako inategemea ufanisi na ubora wa biashara ya mwingine.

Mimi ni mtu nisietaka wateja wa msimu au wateja wa Muda tu,unakuta unafungua biashara eneo ambalo wateja wapo asubuhi - 12 jioni kwisha,au mtu anafungua biashara pembeni ya kanisa as if kila siku ni jumapili,yani kuna watu hawafikiriii kbsaaaaa.

Ili uweze furahia ujasiriamali/biashara yako Jifunze mbinu za kutafuta wateja,kuvuta wateja wawe wako,watu wengine ndio kupitia wewe walete huduma yani waje kwasababu wewe ndio soarce ya wateja sio wewe uende wakati wao ndio soarce (chanzo) usikubali.

Serikali ikifungua stand MTAA A hautoisha mwezi ule mtaa utakua na biashara nyingi sana,kwanini? kwasababu stand ni chanzo cha wateja,sasa usitake kwenda kufanya biashara mahali ambapo source ya wateja sio wewe (sijui naeleweka) kwasababu kwakufanya hivyo ikitokea serikali ikisema hii STAND ihame maana yake hata wale wateja uliotegemea nao watahama lakini wewe kiwa ndio chanzo cha wateja STAND ihame isihame,ije isije wateja wako watakua pale wapo muda wote.

Guys hivi naeleweka kweli?! namalizia kwakurudia tena kwamba Unapofungua biashara yyte hakikisha wewe binafsi uwe chanzo cha wateja eneo unaloenda kufungua,kama unajiona huwezi kuwa chanzo cha wateja huwezi sababisha wateja wakatokea ACHA HIYO BIASHARA UNAYOTAKA KWENDA FUNGUA ACHA.

inatakiwa uweze ku master kutafuta/kuzalisha wateja wako mwenyewe kwa asilimia 70% kisha hizi 30% acha ndio ziongezwe na mazingira yanayotuzunguka lakini kumbua 70% inatakiwa iwe wewe,na sio iwe vice versa.

wewe unaetaka fungua biashara pembeni ya shule,chuo,kanisa,stand,barabarani,nk Hii naomba uichukue na uipokee kama jinsi ilivyo ukiona haikufai iache hapa kisha endelea na plan zako usije sema hukuambiwa.

Biashara zote ni nzuri Guys Zoteeee kama tu Utajua wateja wako wanatoka wapi.
Saluti kwako mkuu
 
Back
Top Bottom