Jifunze kutengeneza Bamia kwa uharaka na ladha safi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,317
33,115
Jifunze kutengeneza Bamia kwa uharaka na ladha safi


bamia%201.jpg



MAHITAJI:
500 gms bamia mbichi (Ladiesfinger)
2 vitunguu vikubwa kata slice
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi iliyosagwa
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu kilichosagwa
1 kijiko kidogo cha chacumin binzali nyembamba
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa manjani (turmeric)
1 kijiko kidogo cha chai unga wa giligilani -(coriander powder)
1 kijiko kidogo cha chai unga wa pili pili (chilli powder)
1/2 kijiko kidogo cha chai juisi ya limao (lemon juice)
1/21 kijiko kidogo cha chai Garam Masala
5 gram chumvi




MUDA WA MAANDALIZI
Muda wa kuandaa : Dakika 30
Muda wa kupika : Dakika 30
Idadi ya walaji : Watu 2

JINSI YA KUANDAA
Osha, safisha kisha kausha bamia zako. Kisha kata ncha za mwisho na ukate tena kugawanyisha mara 2 kama uonavyo katika picha.
Katika kikaango cha moto weka 1/2 kijiko kidogoc ha chai mafuta ya kupikia, kisha ongezea binzali nyembamba. ikishakua ya brown, ongezea kitunguu maji kilichokatwa, pamoja na tangawizi na kitunguu swawumu cha kusagwa pamoja na chumvi. Endelea kukaanga mpaka vitainike.
Kisha weka bamia, hakikaisha hapa unaongeza moto uwe mkali kabisa na kaanga haraka ili bamia ichanganyike na viungo na kitunguu. Kisha punguza moto na acha bamia ichemke kwa dakika 5.
Chakula hiki kinakua tayari tu pale bamia zinapokua laini baada ya kupikwa kwa dakia 15 hadi 20..
HAzitakua rojo rojo zitakua na ugumu wa wastani (crunchy) na ni laini kwa mlaji. Just the right bite to it. Kabla ya kutoa unaweza ongeza moto na ukamalizia kiungo cha mwisho juisi ya limao na garam masala, koroga vizuri na kisha mpatie mlaji na Chapati pamoja na wali.


 
Da bamia lilinisaidia sana enzi hizo naanza maisha mitaa ya Magomeni,mambo yalikuwa magumu kwa hiyo ukiwa na bamia pamoja na nyanya shughuli kwishney ni mlo wa chapchap hapo ukiwa na sembe na samaki wa kulumangia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom