Jifunze kutafuta Fursa badala ya Kutafuta Ajira

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
647
1,000
Kwanza nianze kwa kusema kwamba kuajiriwa sio vibaya,kufanya kazi kuajiriwa sio kosa,wala kuishi kwa mshahara sio dhambi.Watu wengi huwa wanakuwa na tafsiri mbaya sana wanpoona watu tunahamasisha watu kujiajiri bila kufahamu kwamba jamii yetu ina uhitaji mkubwa sana wa Job creators so tunapohamasisha watu wajiajiri lengo sio kusema kwamba ajira na mbaya bali ni katika jitihada za kutaka kutatua tatizo la ukosefu wa ajira ambalo linatesa sana watu.

Tunataka kama jamii tubadili mindset yetu kutoka kuwa job seekers to Job creators.Tunataka jamii ya watu wanaozalisha fursa na sio kutafuta fursa.Tunataka kuondoa ila kasumba ya kwamba ni lazima mtu awe na ajiri ili awe kuishi maisha bora.

Leo nataka nizungumzie umuhimu wa watu kutafuta FURSA badala ya kutafuta AJIRA.Ninaposema fursa simaanisha kwamba AJIRA sio FURSA ila nataka tuitazame FURSA katika Mtazamo mpana na uliozama.Kwa muktadha huu nataka kuelezea fursa kama,jambo,hali,hitaji,suala lolote lile ambalo mtu anaweza kutumia uwezo wake alionao kwa wakti huo katika ama kulitatua,kujioongozea kipato au kutengeneza fursa zaidi.

Ili nieleweke vizuri nitoe mfano rahisi.Kuna tatizo la uchafu katika JIJI la Dar es Salaam,Ndani ya TATIZO hili kuna FURSA.Fursa iliyopo ni ya kulifanya Jiji liwe safi.Ndani ya Fursa hii kuna fursa ya kusafisha,kutoa elimu,kukamata wachafu na kuwatoza,kukusanya taka na kuzifanyia recycling.Kukusanya TAKA na kuzitumia kuzalisha bidhaa mbadala n.k.Hizo zote ni fursa ambazo katika kuzitatua kuna fursa nyingi zitazaliwa pamoja na ajira nnyingi.Kwa TAKWIMU Ndogo tu Kazi ya Kulifanya la Dar es Salaama ambalo lina wakazi TAKRIBANI Milioni 5+ ni kazi ambayo inathamani ya zaidi ya TZS Bilioni moja kwa Mwezi za moja kwa moja na Bilioni nyingine 2 ambazo sio za mojamoja.Hii ina maana kwamba kama mtu akiitazama fursa hii ya JIJI Chafu na kutaka kuitumia anaweza kutengeneza a 1 Bilion industry.

Katika kulifanya Jiji liwe safi atazalisha ajira nyingi,moja kwa moja na ambazo sio za moja kwa moja.Lengo langu sio kuzungumzia usafi wa JIJI la Dar es Salaam.Nafikiri hilo ni Jukumu la Kaka yangu Paul Makonda ila lengo langu ni kutaka kukuonesha kwamba kila tatizo ni fursa.

Hata nikitoa mfano wa TATIZO la AJIRA ambalo nalo ni kubwa,kwa Tanzania kuna fursa imo humo ndani.Wengi wa watafuta ajira wanakosa Taarifa sahihi,wanakosa connection,wanakosa,muongozo sahihi na msaada,wanakosa on demand skills ambazo waajiri wanazitafuta na hazifundishiwi shuleni wala chuoni.Hii nayo ni fursa ambayo nayo haijatumia ipasavyo.Hii ni sector ambayo ina thamani kubwa sana na kama ikitumika ipasavyo itazalisha fursa nyingine zaidi.

Sasa baada ya kutoa mifano ni kueleza ni vipi unaweza kutafuta fursa badala ya kutafuta Ajira.Wewe kama ni mhitimu Pembeni ya Kuwa na Wasifu mzuri(CV) ni muhimu ukawa na skills za ziada ambazo zinahitajika kwenye soko.Unapotembea mjini kutafuta kazi ukienda kwenye ofisi usiseme unatafuta kazi,nenda kama mteja anayehitaji huduma na hakikisha unapata zile key contacts za watu wanaofanya maamuzi.Kwa mfano,kama unatafuta kazi kwenye kiwanda cha saruji,basi nenda kama mtu anayetafuta fursa ya kuwa Super dealer wa Cement au kununua Cement in Bulk kwa ajili ya Project kubwa(Be creative) na hakikisha unapoondoka unapata Email,namba ya SIMU na hata ukiweza waambie wakupatie Pro Forma invoice hakuna ubaya kwa sababu lengo lako ni kujenga connection.Taarifa na connection kama hio inaweza kukusaidia mahali ambapo hujatarjia na ukajenga reputation nzuri sana.

Hivyo basi nasisitiza tena kwamba badala ya kusambaza CV tutafuta kuzielewa zile kampuni,kuelewa huduma zao,kuwaomba watupatie Quotation na Business profile na hata kuhudhuria maonesho yao ili kujenga network pamoja na kuongeza ufahamu kuhusu brands ambalimbali ambazo zinaweza kuja kukuajiri au hata kufanya nao biashara.

Nisisitize tu kwamba badala ya kutafuta Ajira tutafuta FURSA na AJIRA ZITAKUJA ZENYEWE
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
12,726
2,000
Kaka Yangu, Ndugu Yangu, Mdogo Wangu.

( Vijineno Vya Kinafiki Vinavyotumiwa Na Wanasiasa Uchwara Wa Africa Na Vijana Njaa Kujikomba Komba )
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom