Jifunze kusimama peke yako, wewe ni Mshindi

ShalomP

Member
Jun 14, 2019
97
154
Kuna wakati unaweza jikuta upo pekee Hakuna msaada wa ndugu,jamaa Wala rafiki hapo ndipo unahitaji ujitetee.

Kuna vitu vingine huwezi hata kuelezea mtu akakuelewa mzigo ulio nao ni Siri yako.Pambana wewe ni shujaa usimsimulie Kila mtu mipango yako au matatizo yako wengine ukiwasimulia ugeuka mwiba,wengine wanaweza kukutangaza madhaifu yako.

Usitoe Siri za mipango yako Bali washuhudie matokeo,wakikusema wewe wajibu kwa kufanya maendeleo.wakikupiga majungu wewe fanya kazi kwa bidii sana na uwe bize wanadamu hawaishiwi maneno.

Chunga Sana kinywa chako kabla ya kutamka neno lolote tafakari kwanza.kuna maneno mengine hujeruhi mioyo ya watu.mfano mtu hajaajiliwa hujamsaidia mtaji unaanza kusema mvivu,ajiajili je unayajua maisha yake au mapito yake? Msaidie mtaji uone Kama mvivu mwengine amechelewa kuoa au kuolewa unaanza kumjeruhi kwa maneno makali labda amechelewa sababu Hana mahali na kwao ni maskini msaidie mahali uone Kama hajaoa haraka.

Una uhakika wa kula Milo mitatu kulala pazuri unadhani wote tuko sawa tembea ujionee,una uhakika Kila mwisho wa mwezi ndio Mana unarahis sha usiwe muongeaji Sana Mana unaweza jikuta unakosea jifunze kukaa kimya na kuwa na maneno machache Kama ndiyo iwe ndiyo Kama hapana iwe hapana.

Jambo usilopenda kutendewa usiwatendee wengine.kama unapenda kupendwa Basi Anza Kwanza kujari na kupenda,Kama unapenda kusamehewa Anza Kwanza kusamehe,Kama hupendi kuumizwa Basi usiwaumize wengine.ukijua kupokea jua na kutoa na ukipenda kuheshimiwa Basi usiwadharau wengine.

Sio kwamba hawapo marafik i wenye upendo wapo wengi Kila mtu ana rafiki ,ndugu au jamaa yake msiri wake ambaye ndiyo huwa mshauri wake kwa Mambo ya kimwili au kiroho.

Sio marafiki wote ni wabaya wapo wema wasiri. Usimuhukumu mtu kwa mtazamo wa nje au muonekano wake.

Kwa mfano: Watu wakimya na wapole huonekana Kama wanadharau kumbe ndivyo sivyo lakini wakikutana mtu ambaye ni mcheshi anajua kuishi na watu wenye tabia Kama hizi unaweza ukajifunza mengi. Kwanza wako makini Sana, wakalimu pia wana busara na hekima ni washauri wazuri Sana hawapendi kumkwaza mtu Wala kukwazwa ndio Mana ukiwakosea ni wagumu Sana kusamehe ila usiombe mtu mpole akasilike balaa lake ni kubwa.wapo wa aina mbili wengine usamehe haraka,Kama unaona Jambo ni gumu limekuzonga mshirikishe rafiki msiri unayemwamini ambaye unaona atakupa ushauri utakao kujenga na kukuinua angalizo sio Kila mtu anapaswa kumwambia Mambo yako.Kuna wakati uwa inahitajika kampani ya kusimama Ili safari iendelee.

Thamini kazi yako au shughuri unayoifanya usiidharau kikubwa ni halali na inakupa mkate wa Kila siku. Maisha ni haya haya Tuishi kwa Amani na upendo.

Katika haya yote Tumtangulize Mungu.

Jumapili njemaa. LUKA 18:1-14
 
Ahsante sana.
Ila suala la siri ni la mtu mmoja, ukishindwa kukaa na siri na ukamwambia mwingine hiyo siyo siri tena.
Kama wewe mwenyewe imekushinda kukaa nayo sembuse huyo unayemwambia!!!!!
Wahenga walisema "Hakuna siri ya watu wawili"
 
Back
Top Bottom