Jifunze kusamehe na kusahau-2010

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU
Tuna uhakika ya kwamba, Roho Mtakatifu anakuongoza kusoma somo hili kwa makusudi kamili.

Maneno yaliyomo humu ni ya kukusaidia wewe na Wakristo wote, ili tuweze kuishi maisha ya "amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao."(Waebrania 12:14).
Kusamehe na kusahau ni tatizo kubwa ambalo limewazuia wakristo wengi wasipokee majibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Ninaamini kuwa maneno yaliyomo humu yatakusaidia katika kupokea majibu ya maombi mengi ambayo hujayapokea.
Ni maombi yetu kwa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo ya kwamba, Roho Mtakatifu ayachukue mafundisho haya na kuyaandika katika moyo wako, na akusaidie kuyatenda.
Na unaposoma itakuwa ni vizuri ukiwa na Biblia yako karibu, ili usome mistari yote tuliyoiandika. Somo hili tutajifunza kwa wiki sita mfululizo. Somo la wiki inayofuata litakuwa linajenga juu ya somo la wiki linalotangulia hasa baada ya wiki ya kwanza.
Tutakuwekea mfululizo wa somo hili kama ifuatavyo:
Wiki ya Kwanza: Kutosamehe ni kikwazo
Wiki ya Pili: Tabia ya Mungu ya kusamehe ndani yako
Wiki ya Tatu: Hasara za kulipiza kisasi
Wiki ya Nne: Hatua Tano Muhimu katika kusamehe
Wiki ya Tano: Je! aliyekukosea asipokuomba msamaha ufanyeje?
Wiki ya Sita: Utajuaje kama bado hujasamehe?

Tunataraji ya kuwa utaungana pamoja nasi kila wiki katika kujifunza somo hili. Ni maombi yetu kwa Mungu ya kuwa somo hili litakusogeza hatua nyingine muhimu katika maisha yako.
 
Ni masomo mazuri sana ambayo yanakueleza hatua kwa hatua namna ya kusamehe na kusahau.
 
Back
Top Bottom