Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,401
- 21,907
Imegundulika kwamba zaidi ya virusi 100,000 na wengine wajulikanao kama "worms" na "Trojan horses"- ambao kwa ujumla wanaitwa kwa kiingereza "malware" wakati huu wanasambaa katika mtandao wa "internet" na namba yao inaongezeka kiasi cha 1000 kwa mwezi.
Moja ya kampuni za kuuza programs za kuzuia virusi hivi na wengine iitwayo Sophos ya Uingereza, imegundua vitisho vipya vya wadudu hawa zaidi ya 1,380 wengi wakielekezwa kwa computer za Windows.
Lakini habari nzuri zilizopo ni kwamba watu wanaotengeneza hizo "malware" wamekuwa wakikamatwa katika nchi za Belgium mpaka Taiwan likiwemo kundi la wezi wa kwenye mtandao wa internet lililoko nchini Brazil ambalo limekwiba kiasi cha paundi 17 millioni kutoka kwa wateja wa benki katika mtandao wa internet.
Vita hii dhidi ya wezi hawa inaendelea na inasaidiwa na tuzo ya fwedha kutoka Microsoft.
Lakini wataalam wote wanakubaliana kwamba ni yule mmiliki wa computer ndie mwenye jukumu la kuhakikisha kwamba chombo chake hicho kiko salama dhidi ya wezi na waharibifu wengine katika mtandao wa internet.
Kumbuka kuna njia kuu tatu unazoweza kuzichukua kulinda computer yako;
1. Hakikisha firewall ipo hai muda wote iwe ni ya Windows au package nzima ambayo labda umeitunuku na umeinunua.
2. Hakikisha OS(operating system) yako ipo up-to-date.
3. Hakikisha anti virus unayotumia ni original na ipo up-to-date.
Ifuatayo ni maelekezo ya namna ya kulinda computer yako kutoka kwa wasumbufu wa karne hii ya 21.
THE VIRUS WRITER-MTUNZI NA MWANDISHI
Virusi, worms na Trojan horses vyote ni programs za computer zilizobuniwa kuidhuru computer yako, lakini vinatofautiana kinamna. Kirusi kinasafiri kutoka katika computer moja kwenda ingine kupitia kitendo cha binadamu kama vile kufungua email zenye kiambatanisho (attachment.
Kirusi pia kinaweza kusafiri bila msaada wowote kwa mfano kinaweza kujituma chenyewe katika sanduku lenye orodha ya watu ambao wewe huwa unawatumia barua pepe (emails).
Kirusi cha Trojan horse hakiwezi kujirudufisha au kusafiri lakini huwa kinaingia katika HDD na kutulia na kusubiri aliekituma kuiongoza computer yako kwa mfano kwa kubadilisha sura ya desktop yako na zile icons zake.
DALILI:
Unaweza kushangaa kuona computer yako inazima mara tu baada ya kuwaka, kufanya kazi taratibu mno, kuonesha vitu kama matangazo (pop-ups). Trojan huwa haiachi dalili zozote kuonesha kwamba iliingizwa katika computer yako ila kuonekana kama kuna matumizi mengi katika muunganisho wa computer yako na internet.
JINSI YA KUTIBU
Weka OS up-to-date na hakikisha firewall na anti virus ziko hai. Kumbuka anti virus zilizopitwa na wakati ni bure kabisa lakini zile nzuri kama AVG ([B]www.grisoft.com[/B]) zina facility ya kufanya auto-update features.
Fanya online scan kama una shaka na mtandao wako wa internet- jaribu Panda katika website hii tinyurl.com/455j.
Weka anti-Trojan package nzuri kama Trojan Hunter ([B]www.misec.net/trojanhunter[/B]) .
THE ROGUE DIALLER
Hivi ni virusi ambavyo kwa siri vinaunganisha computer yako katika mtandao wa internet na kwa kupiga namba ambazo huitwa "Premium rate" (namba ambazo zikipigwa huambatana na huduma fulanifulani kama za mtangazo) au namba za kimataifa kupitia modem ya dial-up. mara nyingi husafirishwa kwa kutumia -emails.
Watu pia huweza ku-download bila kujua waningiza virusi hivi kwa kuangalia websites zenye mambo kama ngono na kamari. Kwa Tanzania TTCL wanaweza wakawa wanaelewa hivi na kusaidia wateja ambao huenda wamekuwa wanakumbwa na matatizo ya dial-up modem ambapo kama kirusi kimeingia huweza kubadilisha "settings" kutoka kwenye Never Dial up kwenda kwenye dia-up connection.
DALILI:
Bili kubwa ya simu na utaona kwamba computer computer inajiunga na line na kujitoa bila mpangilio na pia kutoa mlio mreefu wa kuunganisha simu ambao mara nyingi huwa ni simu ya mbali.
UTATUZI:
Ondoa "modem" kwenye "line" ya simu pale unapokuwa hautumii computer (hii inajumuisha pia wale ambao wana broadband ambayo ni stand-by dial-up) na ingiza software guard kama Reconnect Warning kutoka www.reconnectwarning.com.
THE PHISHER AU MVUVI
Wezi wa mtandaoni hutuma mamilioni ya e-mails wakizifanya kana kwamba zinatokea ama benki au ofisi zingine au watu fulani wenye shida fulani.
Watakuuliza ukong'oli katika katika link ya tovuti na uende na u-update taarifa zako za akaunti ambayo haipo. Ukiwa ndani ya tovuti hio wanakwambaia uingize taarifa za akaunti yako na uweke password. Ukifanya hivyo computer yako inakuwa inaitwa kwa kiingereza "toast".
DALILI
Barua pepe yenye ujumbe kwako kwamba uijibu. Lakini moja ya mashaka ya haraka ni kuona kwamba kiingereza kilichotumika kuandika e-mail hio ni kibovu, grammar mbovu na harufi zilizokosewa.
SULUHISHO
Hakuna benki yoyote itakutumia e-mail na kukwambia ubadilishe details zako online na usijaribu kujibu au kufungua e-mails ambazo unaona si za kawaida. Kumbuka kuna maeneo makuu matatu yanayoweza kutumika kukuharibia computer yako- email, web browsers na computer ports.
Kwa mfano port 80 ni kwa ajili ya https://www.jamiiforums.com na si vinginevyo ambayo huitwa "default" kwasababu huitaji kusema ni nini hasa unahitaji kutoka katika website hio kama ambavyo ungefanya kwa ULR ambayo unasema ni kitu gani unahitaji kwa mfano https://www.jamiiforums.com/images/meerkatofficers.jpeg.
THE PHARMER (MKULIMA)
Huu ni ushambulizi ulio makini dhidi ya computer yako ambao unatumia software iliotengenezwa ili ichukue taarifa za computer yako na kueleza huyo mr "Pharmer" kuhusu matumizi ya computer yako na unapenda kubarizi sehemu zipi. Inaitwa "spyware". Inaelezwa na wataalam wa computer kwamba kila computer ina vipande kati ya 80 na 90 vya codes ambazo huweza kutumika kuwasiliana na spyware. Programs hizi zinaingizwa katika computer pale mtu anapo-download software fulani au kubarizi tovuti zisizo na maana.
DALILI
Kwa kuwa zinafanya kazi kimyakimya na vigumu kugundua. Hata hivyo uwe mwangalifu pale unapoona browser yako inachukua muda kufunguka au IE kukatika bila ya kutarajia.
SULUHISHO
Ondokana na mambo ya freeware na free toolbars au search bars ambazo zinafadhiliwa na hawa watafutaji na ukae mbali nazo isipokuwa kama zinatoka katika kampuni za kuaminika kama Opera, Yahoo! au Google.
Ili utafute na kuondoa jaribu ku-download Ad-Aware kutoka www.lavasoftusa.com (kumbuka kuangalia anuani sahihi maana kuna zilizofanana na hii). Microsoft nao wana anti-spyware protection ambayo utaipata katika website yao na ukumbuke kuifanya iwe ina-scan automatically na kila mara.
Gharama za ulinzi ni kuwa macho saa zote.
Mwisho.