Jifunze kuhusu Biashara ya KEYWORD

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,226
0
Kumekuwa na mifumo mbalimbali ya Biashara kwa njia ya mtandao ambayo watu wanaweza kufanya bila kuwekeza pesa nyingi zaidi ya muda na ujuzi kidogo wa baadhi ya vitu vidogo vidogo .
Kuna Adsense huu ni mfumo wa Biashara ya matangazo kwenye tovuti na blogu na mitandao mengine inayotolewa na google kwa uzoefu wangu ukiweka adsense kwenye tovuti au blogu yako aina nyingine ya matangazo kwa mfumo wa clicks unaweza usifanye kazi vizuri au inaweza kukufukuzia wateja wako wa blogu au tovuti kwa sababu Fulani fulani .
Kuna Infolinks huu ni mfumo wa Biashara pia wa matangazo tofauti na adsense ambapo unaona picha na maneno kwenye infolinks utaona maneno ambayo yamewekewa alama Fulani kukujulisha kwamba neno hilo linashabihiana na kitu Fulani kwenye mtandao kwahiyo ukigonga neno hilo ambalo linakuwa ni kiunganishi tayari utapelekwa kwenye linki husika ambayo imetangazwa .
Watu wengi wakiona infolinks bila kujua huhisi kurasa za tovuti wanazotembelea zimevamiwa au kuna shida Fulani kwenye komputa hiyo kumbe ni aina ya matangazo athari zake ni kwamba unaweza kupeperusha wateja yaani watembeleaji wa kurasa hizo kwa kiasi kikubwa usipokuwa makini .
Tofauti kubwa wa kimatangazo kati ya adsense na infolinks ni kwamba adsense inaweza kutumika katika lugha karibu zote ulimwenguni na kupata mapato lakini infolinks ni lugha chache mfano ukiweka infolinks kwenye kurasa za Kiswahili hazitambuliki labda kuwe na maneno ambayo yana maana Fulani kwenye lugha ya kiingereza au kifaransa .
Lakini watu wanatakiwa kuwa makini sana na templates wanazoshusha kwenye mitandao kwa ajili ya kuweka kwenye blogu au tovuti zao na kuingiza adsense na aina nyingine ya matangazo mara nyingi template hizi huwa na code zenye matangazo ya Yule ambaye aliweka template hiyo kwenye tovuti husika matokeo yake mapato mengi yataenda kwake - ingawa suala hili limeanza kupatiwa ufumbuzi na baadhi ya kampuni baada ya kushtukia haswa wakati wa malipo na sehemu haswa ya mtu alipokuwa .
Sasa leo ningependa kuongelea kidogo kuhusu hii Biashara ya KEYWORD kuna watu wengi ambao wanatumia adsense na infolinks bila kujaribu KEYWORD kama njia moja wapo ya kuweza kujua masoko yao yapo wapi haswa na jinsi wanavyoweza kutumia maneno kadhaa kwenye blogu zao au tovuti zao kuvuta wateja kwenye tovuti hizo ili aweze kutengeneza kiasa kikubwa cha pesa .
Kama unasoma hii unatakia uangalie kwenye mtandao kujua maana halisi ya keyword linapokuja kwenye suala la Biashara mtandao , kwa ufupi keyword ni maneno makuu mtu anayotumia kutafuta kitu kwenye mtandao kutumia search engine au aina nyingine ya utafutaji .
Mfano wakati wa uchaguzi watu wengi walikuwa wanatafuta neno kama JAKAYA KIKWETE 2010 na DR W P SLAA , ina maana blogu na tovuti zenye maneno hayo zilitembelewa sana na watu waliokuwa wanatafuta taarifa na mambo mengine kuhusu watu hao wawili na wengine wamejitengenezea vipato Fulani kwa njia ya keyword .
Ukija kwenye suala suala lingine sasa mfano kuna tovuti inaitwa NAOMBAKAZI.COM hii ni kwa ajili ya nafasi za kazi ulimwenguni , ukienda hapo utaona kuna vichwa vya habari kama International Jobs in Tanzania , Mining Jobs In Africa , Jobs in Kenya na mengine mengi sana ina maana mtu akitafuta Jobs in Kenya kwenye search engine kwa mtandao inaweza kukutana na tovuti naombakazi.com ambayo itakuwa na neno JOBS IN KENYA , ukitaka kujua Keywords au maneno ambayo watu hutumia kutafuta mpaka kufika kwenye tovuti au blogu yako nenda kwenye stats au tembelea keywordspy.com utaweza kujua hilo na utaweza kutumia maneno hayo KEYWORDS kwa ajili ya kuboresha zaidi tovuti au blogu yako kwa ajili ya kuvutia zaidi watu watembelee kwa huduma mbalimbali za kimtandao kama nafasi za kazi , majadiliano na mengine mengi sana .
Kwahiyo hiyo ni Biashara ya KEYWORD kwa ufupi tu unaweza kujifunza zaidi kutumia mafunzo mbalimbali kwa njia ya mtandao na utaweza kujitengenezea kipato kwa njia ya mtandao .
YONA F MARO
WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom