Jifunze kuelewa maana ya kuoa/kuolewa kabla ya kuingia huko

nebuchadnezzer

JF-Expert Member
May 10, 2013
245
341
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Kama wengi wetu tujuavyo, Ndoa ya kwanza ilifungishwa pale Edeni na Mungu mwenyewe. Na ilikuwa ndoa takatifu, iliyobeba msingi na dira ya ndoa nyingine zote zitakazofuata jinsi zinavyopaswa ziwe.

Katika ndoa ile ilihusisha Mtu mume mmoja (Adamu) na mtu mke mmoja (Hawa)..Kwa kupitia wazazi wetu hawa wawili ndio sisi sote tumetokea…ikiwa na maana kuwa ndoa kamili na takatifu inahusisha mume mmoja na mke mmoja…na si Zaidi. Hicho ni kigezo cha kwanza na cha muhimu.
kabla ya kuingia huko kabla ya kuingia huko

Pia kabla ya ndoa ile kufungishwa, Maisha yalianza na Adamu kwanza, Mungu alimpa Adamu mimea, mashamba ya kulima, makazi na kila kitu, hapo kabla Hawa hajatokea…na Adamu akaanza majukumu yake ya shughuli pale Edeni kabla ya Hawa kutokea…Na Hawa alipotokea alikuwa kama msaidizi tu wa kazi ambayo tayari ilikuwa imeshaanza. Ikiwa na maana kuwa Mwanamume yoyote kabla hajadhamiria kuoa ni lazima angalau awe na mahali pa kujishikiza ili aweze kumhudumia huyo mkewe anayekuja kumwoa…

Na kumbuka Mungu hakumleta Hawa kwaajili ya tamaa za mwili za Adamu, hapana bali alimleta ili awe msaidizi kwake, kwa namna zote, kifikra, na hata katika kazi zake za kimaendeleo Adamu alizokuwa anazifanya…Ikiwa na maana kuwa lengo la kwanza la ndoa sio kukutana kimwili kama inavyochukuliwa sasa na wachache wasio na maarifa ya kutosha.

Hivyo mwanamke jukumu lake kubwa katika ndoa ni kushirikiana na mume wake, na kuyafanya majukumu yote ambayo mume wake angepaswa ayafanye, ikiwemo ya kihuduma na ya kiuchumi, Hawa hakupelekwa kwa Adamu kumtoa Adamu pesa!..bali awe msaidizi….Maana yake kitu ambacho hakijakaa sawa au hakijakamilika mikononi mwa mwanaume, mwanamke anakiweka sawa na kukimalizia.

Na jukumu kubwa Zaidi mwanamume na mwanamke walilopewa ni kujiepusha na Uovu…Na shetani huwa anawatumia wanawake wengi kuharibu ndoa kuliko wanaume..Kama Hawa mzazi wetu wa kwanza angekaa katika nafasi yake na kujiepusha na uovu, leo hii duniani kungekuwa ni paradiso, lakini kwa kuacha majukumu yake ya USAIDIZI na kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu hakumwagiza matokeo yake ndio yakawa yale…Na hata sasa mwanamke akiacha majukumu yake na kujikita katika ulimwengu huu, katika usengenyaji, umbea, katika kutoa siri za mume wake nje, katika kutomheshimu mume wake, kumdharau, kumdhalilisha, kumwaibisha, kuvaa kikahaba, kuwa mhuni, mlevi,mtu mwenye mizaha na kila aina ya udunia, anajiharibia mwenyewe na anaibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe..

Na Ndoa takatifu ni lazima ihusishe watu wawili wenye Imani moja..Ni kinyume na maandiko kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini baada ya wewe kuamini, Kama umeshamwamini Yesu Kristo na uweza wake hupaswi hata kidogo kutafuta kuoa/kuolewa na mtu asiye mkristo. Na ndoa yoyote ya kikristo lazima iwasilishwe na kubarikiwa mbele ya kanisa la Kristo. Sio sahihi kabisa kufunga ndoa za kimila wala za kiserikali baada ya kumwamini Yesu Kristo.

Na ni lazima kulipa mahari kwa ndugu wa mwanamke kabla ya kumwoa, kama huo ndio utaratibu wa familia ya mwanamke, Adamu hakulipa mahari kwasababu mkewe Hawa ,chimbuko lake lilikuwa ubavuni mwake, hakuwa na wazazi wala ndugu…lakini sasa kila mwanamke anao wazazi/ndugu/walezi…Huko ndiko alikolelewa, hakulelewa ubavuni mwako,…kwahiyo ni wajibu kumtoa kwa wazazi wake kwa utaratibu huo maalumu wa kulipa mahari…

Hata Hawa alipotolewa ubavuni mwa Adamu, Bwana Mungu aliparudishia nyama pale palipotolewa ili Maisha ya Adamu yaweze kuendelea, hakuacha shimo pale wala kidonda!…Na hali kadhalika unapomtoa mwanamke kwa wazazi wake ni lazima uzibe pengo uliloliacha pale, na hilo unaliziba angalau kwa mahari, sio unamwiba na kuacha huzuni kule na malalamiko na laana na maumivu.

kama utashindwa kulipa mahari ya kiasi hicho kidogo cha fedha utawezaje kuitunza na kuihudumia familia yako inayokuja huko mbele, ambayo pengine itahitaji matunzo ya gharama nyingi kuliko hizo za mahari??…kama hutaki kutoa mahari, maana yake bado hujaelewa maana ya kuoa, hivyo unapaswa ungoje mpaka utakapoelewa vyema maana ya ndoa ndipo uoe.

Na mwisho biblia inatuambia kuwa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana…wale ambao wameoa na wawe kama hawajaoa…ili muda mwingi tuutumie katika kuutafuta Zaidi ufalme wake na haki yake kwasababu unyakuo upo karibuni, na mbinguni tuendako hakutakuwa na kuoa wala kuolewa, yatakuwa ni mambo mapya huko ambayo ni ya muhimu Zaidi kuliko haya.

1Wakorintho 7:28 “Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
29 Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;
30 na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu.
31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.
32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”

Maran atha!
 
Asante sana ndugu kwa bandiko lako hili, japo sijamaliza kusoma ila niweke sawa pale sehemu umesema ndoa ni ya mume na mke mmoja na si zaidi... hebu nipe rejea yenye kusema hayo.

Nikionacho mimi katika dhana yako ni kwa mujibu wa uumbaji wa Mungu, aliumba mtu mume na mke na kuwabariki wakazae waongezeke... hii haitoshi kujenga hoja ya mke mmoja.

Ikumbukwe baada ya watu wa Mungu kuongezeka walianza kujitwalia wake lukuki, tena ni wale watu wake watiifu kindakindaki na haikupata kukemewa... kama ipo rejea nitafurahi kujifunza.

Ngoja nirudi nikaendelee kusoma, nitarejea tuendelee kujifunza... heshima mbele.
 
Hii hoja yako ya wake wengi, waandishi na Mafarisayo walimtega nayo Yesu uli wapate kumkamata lakini aliwajibu vizuri na kuwaambia kuoa mke zaidi ya mmoja na kutoa talaka waliruhusiwa na Musa (siyo Mungu) kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao lakini Tangu mwanzo kusudi la Mungu ilikuwa mke / mume mmoja tuu
Kasome (Mathayo 19:3-12) au Marco 10:2-12)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafsiri nzuri ya ndoa ni kuoana hiyo ya kusema kuna muoaji na muolewaji haijakaa vizuri ndoa ni kuoana hiyo inaleta balance kwenye ndoa
 
Badilisha heading hiyo uliyoweka imekaa kimfumo dume unaojikweza badala ya kusomeka
JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO

Isomeke

JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOANA KABLA YA KUINGIA HUKO.
 
Hii hoja yako ya wake wengi, waandishi na Mafarisayo walimtega nayo Yesu uli wapate kumkamata lakini aliwajibu vizuri na kuwaambia kuoa mke zaidi ya mmoja na kutoa talaka waliruhusiwa na Musa (siyo Mungu) kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao lakini Tangu mwanzo kusudi la Mungu ilikuwa mke / mume mmoja tuu
Kasome (Mathayo 19:3-12) au Marco 10:2-12)

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante ndugu yangu, nimesoma rejea yako japo imejikita zaidi kwenye talaka na kujificha kuwa ile ilikuwa ruhusa ya Musa kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao... kitu kipya najifunza hapo ni uwezo wa Musa kupindisha (kupotosha) sheria kulingana na mazingira.

Kuhusu wake wengi haina maelezo, zaidi ya ile tu kuwa Mungu aliumba mume na mke na wakawa mwili mmoja.... inaweza kuwa inajitosheleza.

Sasa hapo baada ya vitisho vya ‘kuzini’ ikitokea mmeachana, wanafunzi wake wanasema basi kwa ugumu huo haifai kuoa... hii si kinyume na mpango wa Mungu.?
 
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Kama wengi wetu tujuavyo, Ndoa ya kwanza ilifungishwa pale Edeni na Mungu mwenyewe. Na ilikuwa ndoa takatifu, iliyobeba msingi na dira ya ndoa nyingine zote zitakazofuata jinsi zinavyopaswa ziwe.

Katika ndoa ile ilihusisha Mtu mume mmoja (Adamu) na mtu mke mmoja (Hawa)..Kwa kupitia wazazi wetu hawa wawili ndio sisi sote tumetokea…ikiwa na maana kuwa ndoa kamili na takatifu inahusisha mume mmoja na mke mmoja…na si Zaidi. Hicho ni kigezo cha kwanza na cha muhimu.
kabla ya kuingia huko kabla ya kuingia huko

Pia kabla ya ndoa ile kufungishwa, Maisha yalianza na Adamu kwanza, Mungu alimpa Adamu mimea, mashamba ya kulima, makazi na kila kitu, hapo kabla Hawa hajatokea…na Adamu akaanza majukumu yake ya shughuli pale Edeni kabla ya Hawa kutokea…Na Hawa alipotokea alikuwa kama msaidizi tu wa kazi ambayo tayari ilikuwa imeshaanza. Ikiwa na maana kuwa Mwanamume yoyote kabla hajadhamiria kuoa ni lazima angalau awe na mahali pa kujishikiza ili aweze kumhudumia huyo mkewe anayekuja kumwoa…

Na kumbuka Mungu hakumleta Hawa kwaajili ya tamaa za mwili za Adamu, hapana bali alimleta ili awe msaidizi kwake, kwa namna zote, kifikra, na hata katika kazi zake za kimaendeleo Adamu alizokuwa anazifanya…Ikiwa na maana kuwa lengo la kwanza la ndoa sio kukutana kimwili kama inavyochukuliwa sasa na wachache wasio na maarifa ya kutosha.

Hivyo mwanamke jukumu lake kubwa katika ndoa ni kushirikiana na mume wake, na kuyafanya majukumu yote ambayo mume wake angepaswa ayafanye, ikiwemo ya kihuduma na ya kiuchumi, Hawa hakupelekwa kwa Adamu kumtoa Adamu pesa!..bali awe msaidizi….Maana yake kitu ambacho hakijakaa sawa au hakijakamilika mikononi mwa mwanaume, mwanamke anakiweka sawa na kukimalizia.

Na jukumu kubwa Zaidi mwanamume na mwanamke walilopewa ni kujiepusha na Uovu…Na shetani huwa anawatumia wanawake wengi kuharibu ndoa kuliko wanaume..Kama Hawa mzazi wetu wa kwanza angekaa katika nafasi yake na kujiepusha na uovu, leo hii duniani kungekuwa ni paradiso, lakini kwa kuacha majukumu yake ya USAIDIZI na kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu hakumwagiza matokeo yake ndio yakawa yale…Na hata sasa mwanamke akiacha majukumu yake na kujikita katika ulimwengu huu, katika usengenyaji, umbea, katika kutoa siri za mume wake nje, katika kutomheshimu mume wake, kumdharau, kumdhalilisha, kumwaibisha, kuvaa kikahaba, kuwa mhuni, mlevi,mtu mwenye mizaha na kila aina ya udunia, anajiharibia mwenyewe na anaibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe..

Na Ndoa takatifu ni lazima ihusishe watu wawili wenye Imani moja..Ni kinyume na maandiko kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini baada ya wewe kuamini, Kama umeshamwamini Yesu Kristo na uweza wake hupaswi hata kidogo kutafuta kuoa/kuolewa na mtu asiye mkristo. Na ndoa yoyote ya kikristo lazima iwasilishwe na kubarikiwa mbele ya kanisa la Kristo. Sio sahihi kabisa kufunga ndoa za kimila wala za kiserikali baada ya kumwamini Yesu Kristo.

Na ni lazima kulipa mahari kwa ndugu wa mwanamke kabla ya kumwoa, kama huo ndio utaratibu wa familia ya mwanamke, Adamu hakulipa mahari kwasababu mkewe Hawa ,chimbuko lake lilikuwa ubavuni mwake, hakuwa na wazazi wala ndugu…lakini sasa kila mwanamke anao wazazi/ndugu/walezi…Huko ndiko alikolelewa, hakulelewa ubavuni mwako,…kwahiyo ni wajibu kumtoa kwa wazazi wake kwa utaratibu huo maalumu wa kulipa mahari…

Hata Hawa alipotolewa ubavuni mwa Adamu, Bwana Mungu aliparudishia nyama pale palipotolewa ili Maisha ya Adamu yaweze kuendelea, hakuacha shimo pale wala kidonda!…Na hali kadhalika unapomtoa mwanamke kwa wazazi wake ni lazima uzibe pengo uliloliacha pale, na hilo unaliziba angalau kwa mahari, sio unamwiba na kuacha huzuni kule na malalamiko na laana na maumivu.

kama utashindwa kulipa mahari ya kiasi hicho kidogo cha fedha utawezaje kuitunza na kuihudumia familia yako inayokuja huko mbele, ambayo pengine itahitaji matunzo ya gharama nyingi kuliko hizo za mahari??…kama hutaki kutoa mahari, maana yake bado hujaelewa maana ya kuoa, hivyo unapaswa ungoje mpaka utakapoelewa vyema maana ya ndoa ndipo uoe.

Na mwisho biblia inatuambia kuwa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana…wale ambao wameoa na wawe kama hawajaoa…ili muda mwingi tuutumie katika kuutafuta Zaidi ufalme wake na haki yake kwasababu unyakuo upo karibuni, na mbinguni tuendako hakutakuwa na kuoa wala kuolewa, yatakuwa ni mambo mapya huko ambayo ni ya muhimu Zaidi kuliko haya.

Maran atha!
sehemu ya mahari sijaelewa, ina maana wahindi mahari inavyolipwa na mwanamke ni kosa?
 
Tafsiri nzuri ya ndoa ni kuoana hiyo ya kusema kuna muoaji na muolewaji haijakaa vizuri ndoa ni kuoana hiyo inaleta balance kwenye ndoa
Hiyo ya kuoana ni maisha ya kisasa tu ila kuna kuoa na kuolewa.
 
sio kweli kila upande lazima urithie ndiko kunaitwa kuoana.Ndoa usipofunza maswala ya kuoana na misingi ya kuoana ndoa hazifiki mbali zitavunjika empasis iwe kufundisha jinsi watu waweza kuoana na jinsi waweza ishi pamoja kama community moja ,Wakifunzwa sheria za ushirika ndani ya community yao kama vile kila mtu ampende na kumheshimu mwenzie kutochokozana,kunyenyekeana kila mmoja amnyeyekee mwenzie nk nje ya hapo ni pata shika nguo kuchanika kwenye ndoa
 
Na Ndoa takatifu ni lazima ihusishe watu wawili wenye Imani moja..Ni kinyume na maandiko kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini baada ya wewe kuamini, Kama umeshamwamini Yesu Kristo na uweza wake hupaswi hata kidogo kutafuta kuoa/kuolewa na mtu asiye mkristo. Na ndoa yoyote ya kikristo lazima iwasilishwe na kubarikiwa mbele ya kanisa la Kristo. Sio sahihi kabisa kufunga ndoa za kimila wala za kiserikali baada ya kumwamini Yesu Kristo.

Kipande hiki nafikiri umeamua kuchagua upande na kuminya mjadala, ‘kanisa la Kristo’ ni nini na linahusikaje na uhalali wa ndoa.?
 
dhana ya mke moja na mume mmoja haijitoshelezi!!!Mungu aliumba kila kiumbe wawili wawili wa kiume na wakike kama kawaida tu!lakini hakuna sheria yj mke mmoja bali kila mtu na uwezo wake!!daudi hafanani na king solomon na n.k!!!Dhana ya kuwa mwili mmoja sio ya kimwili bali ya kiroho kama kristo alivyo mume wa kanisa japo kanisa lina watu wengi tena wa jinsia tofauti haimaanishi kristo kawaoa wote!!!!Dhana mke zaidi ya mmoja sio dhambi wala hakuna ole kwa wenye wake zaidi ya mmoja!!!HATA TAIFA LA ISRAEL AMBALO MNASEMA NI TAKATIFU LILIZALIWA NA WANAWAKE WANNE WALIOLALA NA YAKOBO NA HAIKUWA KOSA WALA HAWAKUZALIWA WATOTO HARAMU HAPO NDIO MANA TAIFA NI TAKATIFU!!Enyi wakristo! je nyie mu watakatifu kuliko yakobo?selemani?daudi ambao walioa zaidi mmoja?kwanini kujitungia sheria ambazo ni kitanzi kwenu???Hata paulo hakuwaambia?kuwa ni maaskofu na mashemasi pekee wanao paswa kuoa mke mmoja???Aliewadanganya ni nani?Basi mi nasema kila mtu na aoe kwa kadri ya uwezo wake kama Baba apendavyo na sio kwa sheri za uchumi za viwanda za 1800 za warumi zisemavyo kuwa eti muwe na mmoja na wengine wasioe kabisa isipokuwa Baba amesema nao!!!
 
Sheria za viwanda vya 1800 zilisisitiza nuclear family ya mume na mke na watoto wawili ili iwe rahisi kuwasafirisha kutoka kiwanda kimoja kwenda kingine!!!dhana ya uumbaji ni kwamba kila kiumbe aliumbwa wawili wawili kuendeleza kizazi na sio kuoana kama wanavodhani wengi!kuoana kuna kuja badae nyakati za musa na torati ndio taratibu za kuoana ndo mana hapo mwanzo kaka na dada waliingiliana na kuzaa hadi kizazi chetu !kulikuwa hakuna sheria za kuoana!!kuoana kumekuja badae sana kwenye nyakati za musa!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom