Jifunze kuchagua Marafiki Baada Ya Ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jifunze kuchagua Marafiki Baada Ya Ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Nov 22, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,610
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  MARAFIKI

  Je wewe ni rafiki mwema?

  je wamtakia nduguyo maisha ya amani kwenye ndoa yake?

  je utafaidika ni ni ukihusika katika kuvunja ndoa ya mwenzio??

  Ndugu wapendwa nimeona ni vyema leo tuongelee matatizo ya marafiki katika ndoa....marafiki ni watu wazuri sana..lakini marafiki hawa hawa ni watu wabaya sana sana katika kujenga Familia...tunajua watu wengi wanapotoka katika ubachela wanakuwa na marafiki wengi..wapo waliokuwa wanakunywa nao mpaka saa saba ya usiku..wapo uliokuwa nao mnaongozana pale Africasana kuchagua "TUNDA"...kuna wale ambao kweli wana upendo wa dhati...naomba nikujulishe baada ya kuwa na mahusiano ya ndoa una/utaitajika kuchagua marafiki ili NDOA yako iendelee...dear
  br n sis...nimeeona ndoa nyingi sana zikiterereka sababu ya marafiki..unakuta mtu alikuwa anakaa ROSEGARDEN mpaka saa saba usiku leo hii ameoa hajui pale ndani yuko mkewe na mtoto wanamsubiri...tusikubali kutokea yale yaliomtokea ndugu mtarajiwa masa@@@

  ni vyema tukajali familia zetu kabla ya marafiki..ukioa ama kuolewa jua unahitaji kubaki na wale marafiki unaowaona wanafaa na hawataweza kuyumbisha familia/Ndoa yako..usiogope kuachana na marafiki kama inafika wakati angalia lipi bora kuwa na amani na familia yako ama kuwa na marafiki watakaoyumbisha familia yako
  Kama umekuwa unayumbishwa anza sasa badilika...jali familia yako rudi nyumbani muda muafaka...

  Nawatakia NDOA ZENYE BARAKA
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Ukishaoa tafuta marafiki waliooa..
  Marafiki wasiooa usiwaache but usizungumze
  masuala yako na mkewe kwao.
  Hawawezi kukushauri vizuri.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,610
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280

  Good expirience..inabidi mkuu tutengeneze kataasisi chetu cha ushauri wa ndoa lakini kiwe ka NGO kwanza tujue pa kutokea kimaisha...
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  mie sitaki rafiki rafiki yangu ni mme wangu tu mwingine wa nini ??? simtaki nasema simtaki eeh ...
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Mh kwa hili nitapoteza marafiki wote wazuri.

  Vipi kama hujabahatika kupata mchumba na muda unasonga?
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  hahahaha ina maana huna ubavu wa ku approach or ???
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ninao ila picha yangu ile siuliiona na wewe ulikuwa wa kwanza kuniponda na hapo umeoolewa je ungekuwa single sindio ungeeuwa kbsa?
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama hili ni sahihi.Cha msingi ni uwe na rafiki mzuri tu kama umeoa/umeolewa au hujaoa/hujaolewa.kwani hakuna marafiki wabaya waliooa/kuolewa?
  Kuna watu wapo single lakini wana mapweinti makali kuliko waliooa/kuolewa..
  As long as una akili basi unaweza kupambanua jema na baya.Na ni rahisi kwako kujua kama huyu rafiki ni mbaya au mzuri.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mie pia nasema wake za watu tusiwe na mashoga...............manake hawana cha maana zaidi ya umbea na kukushawishi kuwa mume wako hakupendi
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  kwani sura mbaya ndo inasababisha usio jamani kila mtu ameandikiwa wa kwake
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Marafiki kwani unawapataje? Na unachaguaje jamani hebu tufafanulie
   
 12. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  A wapi ZD, aliyeolewa bora asiwe close na singles, wanaweza kuwa marafiki wa kawaida tuu, lakini close friends...nope!

  kwanza hata story zinaanza ku wa hazipandi kwa sababu mnajikuta kila mkiongea from heart mnaongea "lugha" tofauti
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  kweli Triples
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Usisahau na hii iko kwa madadas waliolewa pia. Anakuwa anamwonea mwenzake wivu kwa kuwa kampiku kimaisha -pesa kidogo , life style etc. then anatengeneza mazingira ya kumharibia mwenzake. Sometimes madadas wanadanganyana ile mbaya hasa wanapoanza topic za kuwakandia waume zao . mara anaingia mtegoni anamplekea mumewe waliyodanganyanyana ,kumbe anaharibu huku mwenzie anachekelea jino pembe.
   
 15. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,404
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Acha hasira mama,kama hutaki rafiki utajisikiaje huyo mume wako unayeamini kuwa ndio rafiki yako pekee,akawa hana urafiki wowote na wewe bali anatimiza ahadi tuu ya ndoa yenu,je,hujui kuwa ktk maisha ya kawaida marafiki wanaumuhimu sana,je,mume wako akiamua kufuta urafiki na wewe sababu ya maslahi yake utaficha wapi sura yako?Au wewe unajuaje kama na yeye anakuchukulia kama rafiki,think twice mama!!
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  mchajikobe yule niliyeamini ni rafiki yangu niliekuwa nikilia nae analia nikiumwa nae anaumwa kumbe anapretend sitaki tena
  labda baadae sana au wewe uwe rafiki yangu ama nipate kibibi cha 50-70 years nikipende kinipende nikitunze na kukieheshimu hahaha
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie kwa kweli ckubadili frnd kabisa, wale wale walio wema kwangu ndio nipo nao mpaka kesho na ni watu wangu wa karibu kwenye shida na raha, huo umbea wa kuanza kuongelea waume zenu kwa ma frnd ndio una cost...rafiki ni rafiki na ataendelea kuwa rafiki na mume ni mume kila mtu ana nafac yake.
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  ndio kama wewe mami, bado hujaingia ndani lakini ushauri umesimama kama hivi....well said ma.
   
 19. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,404
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Hivi hujui kuwa ndoa huvunjwa na wanandoa?Mara nyingi sana ukiwa na marafiki ambao ni wana ndoa watakuelezea matatizo ya ndoa zao na solutions walizo jaribu chukua,sasa hapa usipokuwa makini ndio utajikuta unaishia kwa waganga,sababu tuu ni rafiki unaye muamini,na ukiwa na marafiki wanandoa amini usiamini ktk kila ushauri atakao kupa kuhusu ndoa yako unaweza jikuta unakubali,kisa tuu ameishi muda mrefu ndoani,swala ni kwamba kuwa na marafiki wa aina tofauti ila unatakiwa kuchuja ushauri wao!!Marafiki ni watu wa kupokelewa,sio kukimbiwa!!
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kwanini lugha zitofautiane? kwani mkikaa c mnaongelea maendeleo na mambo mengine ya lyfe kusaidiana pale panapowezeana? walkuwa frnds zangu kabla cjaolewa, leo nimeolewa niwamwage eti kisa tutapishana lugha?...kabla cjaolewa nilikuwa na ma frnd walioolewa na nimeolewa nikaendelea kuwa na frnds ambao walikuwa bado hawajaolewa na hatukuwahi kuongea lugha tofauti kabisa....nadhani hapa kila mtu na msimamo wake.
   
Loading...