Wanawake muelewe, sio kila mwanaume anayekupa hela anakutaka kimapenzi

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233
Kuna mdada alikutana na mkaka wakati wako safarini yule kaka akamuomba mdada namba ya simu njiani akamnunulia kila kitu alichotaka, alipofika stand mkaka akamlipia usafiri mpaka home kwao. Basi wakawa wanawasiliana kila siku. Siku nyingine anamuita wanatoka wanakula na kunywa na hela anampa.

Yule dada akawaambia marafiki zake nimepata bonge la bwana jamani nitake nini mimi nisipewe? Mashoga wakamwambia we ebu jaribu yule dada akampigia yule jamaa akamwambia leo nipo nipo tu natamani kutoka ila sina hela ya saloon nimemisi sina kwenda club na marafiki zangu. Yule jamaa akamwambia ok akamtumia laki 3 ya saloon na kumwambia kama isipimtosha aseme.

Wenzie wakasema lol shoga bwana umempata ilipofika jioni yula mwanaume akapiga simu kwa yule binti akamuuliza club gani mnakwenda? Yule dada akataja club wanayotaka kwenda yule bwana akamwabia basi namtuma mtu aje awachukue mimi mtanikuta huko.

Baada ya muda yule dada akaenda yeye na jopo lake, walipofika wakanywa, wakala na kucheza. wakarudishwa home kama walivyoahidiwa siku ya pili yule bwana akamwambia yule dada nataka kuzungumza na wewe ila please njoo peke yako yule dada akajikoka akaenda alipofika kule yule kaka akamwambia nimempenda sana rafiki yako yule mweupe mweupe naomba ukamwambia hisia zangu hizi wala sina plan ya kumchezea nitamuoa kabisa.

Yule dada akamwambia mimi je? Yule kaka akamuuliza wewe nini? Yule dada akamjibu mimi utanipeleka wapi kwa hiyo mimi ndo unaniacha? Yule kaka akamwambia mimi sikuwahi kukupenda wewe kimapenzi, nilikuchukulia kama rafiki ndo maana sijawahi kuzungumza na wewe swala la mapenzi mimi huwa nikikipenda kitu sichukui muda ninasema hapo hapo.

Tangu nikufahamu wewe tuna miezi kama mitatu sijawahi hata kukushika nywele kama kunakitu nimekifanya kwako ni kukushika mkono tu kitu ambacho hata marafiki wanakifanya sikuwahi hata kukuleta kwangu kwa kuwa najua ni mke pekee ndie anaestahili kupajua nyumbani kwangu.

Dada huku akilia akamwambia mbona ulikua unanihonga? Yule kaka akacheka akasema sikuwahi kukuhonga mimi nilikua nakupa kama rafiki na sababu ya kukunyima angali ninacho sijafundishwa hivyo na usidhani kama nitamuoa rafiki yako alafu wewe ukiniomba nitakunyima hapana nitakupa kama ninacho ila katu sitokupa kipaumbele kuliko mke wangu. Mke wangu akiridhika kwa nilichompa basi nawe utapata, basi yule dada akamwambia siwezi kumwambia rafiki yangu watanicheka mno wote wanajua wewe ni bwana wangu siwezi naomba unipende mimi kaka yangu.

Yule kaka akamwambia siwezi kukupenda wewe kama mke wangu sina hisia hizo kwako na usiogope kumwambia ni bora ukaseme wajue wewe uliuelewa upendo wangu vibaya watakubembeleza na kukufariji, kuliko kukaa kimya maana mimi nitakapokutana na rafiki yako popote nitamwambia tija ya moyo wangu nae atakapo nikataa kwa kudhani mimi ni shemeji yake nitamuelewesha jins gani mimi tulivyo na ili kujitetea ili kumpata nimpendae nitaingia ndani zaidi na kumweleza kuwa nilikutuma wewe ujumbe huu na hukuufikisha.

Hapi ndipo rafiki zako watakudharau na kukukebehi watakuletea maringo ya waz iwazi na utajiona huna thaman. kuelewa vibaya sio tatizo ila tatzo linakuja pale ulipogundua kuwa ulichokielewa sicho nawe ukang'ang'ania.

Yule dada aksmjibu sasa kwanini hukunipenda mimi wakati ndo ulitangulia kuniona? Yule kaka akamjibu sio kila kilichopo mwanzo kinastahili kuna vingine vyenye kufaa vipo kati na hata mwisho kikubwa usiwe na haraka katika kufanya maamuzi nikuulize swali dada? Yule dada akamjibu ndio niulize, yule kaka akamwambia hapo ulipo unausichana wako? Yule dada akamjibu hapana, kaka akamuuliza ni nani alieutoa? Yule dada akamjibu mpenzi wangu wa kwanza, yule kaka akamuuliza yupo hai au amekufa? Yule dada akamwambia yupo hai na mpenzi wake mwingine.

Basi yule kaka akamwambia KWANINI HUKULAZIMISHA NDOA KWA MTU ALIYETANGULIA KUUJUA UNDANI WAKO NA UJE KULAZIMISHA NDOA KWANGU MIMI MTU NILIETANGULIA KUZIJUA TAMAA ZAKO?

Rafiki yako alikua mstaarabu sana kati ya marafiki zako wote, hakunywa pombe, hakuupenda mziki mlimlazimisha tu kuja mara nyingi alikua ni mtu wa kukaa chini, mara kwa mara alisisitiza tirudi nyumbani. Hata tulivyokua tukiondoka alinambia ni vema na wewe umeenda kupumzika maana umechoka pia sisi nyumbani tutakwenda wenyewe sio mbali na hapa tukichukua tax wote mlimbeza na kumwabia hebu huko hiyo ndo kazi ya mwanaume tupeleke utupe na hela ya supu kesho.

Hivi mlimpata wapi rafiki kama yule mbona haendani na ninyi? Yule msichana huku akilia akajibu yule ni house girl wetu huwa napenda kutoka nae ili baba na mama wasihisi nakwenda kufanya mabaya huko niendako.

Basi yule kaka akamwambia nenda kamwambie house girl wenu kuwa NAMPENDA SANA AJE KWANGU AFANYE KAZI YA KUNIPENDA KWA DHATI NAMI NITAMLIPA UPENDO.

#Js
 
Hakika nashindwa kuandika.

Huu uzi ni ujumbe kuntu.

Ila vijana , wala chips zege na kuku wa kichina hawataelewa kwa maana hata kama wakiambiwa maana huwa hawaelewi katu.
 
Kuna mdada alikutana na mkaka wakati wako safarini yule kaka akamuomba mdada namba ya simu njiani akamnunulia kila kitu alichotaka, alipofika stand mkaka akamlipia usafiri mpaka home kwao. Basi wakawa wanawasiliana kila siku. Siku nyingine anamuita wanatoka wanakula na kunywa na hela anampa.

Yule dada akawaambia marafiki zake nimepata bonge la bwana jamani nitake nini mimi nisipewe? Mashoga wakamwambia we ebu jaribu yule dada akampigia yule jamaa akamwambia leo nipo nipo tu natamani kutoka ila sina hela ya saloon nimemisi sina kwenda club na marafiki zangu. Yule jamaa akamwambia ok akamtumia laki 3 ya saloon na kumwambia kama isipimtosha aseme.

Wenzie wakasema lol shoga bwana umempata ilipofika jioni yula mwanaume akapiga simu kwa yule binti akamuuliza club gani mnakwenda? Yule dada akataja club wanayotaka kwenda yule bwana akamwabia basi namtuma mtu aje awachukue mimi mtanikuta huko.

Baada ya muda yule dada akaenda yeye na jopo lake, walipofika wakanywa, wakala na kucheza. wakarudishwa home kama walivyoahidiwa siku ya pili yule bwana akamwambia yule dada nataka kuzungumza na wewe ila please njoo peke yako yule dada akajikoka akaenda alipofika kule yule kaka akamwambia nimempenda sana rafiki yako yule mweupe mweupe naomba ukamwambia hisia zangu hizi wala sina plan ya kumchezea nitamuoa kabisa.

Yule dada akamwambia mimi je? Yule kaka akamuuliza wewe nini? Yule dada akamjibu mimi utanipeleka wapi kwa hiyo mimi ndo unaniacha? Yule kaka akamwambia mimi sikuwahi kukupenda wewe kimapenzi, nilikuchukulia kama rafiki ndo maana sijawahi kuzungumza na wewe swala la mapenzi mimi huwa nikikipenda kitu sichukui muda ninasema hapo hapo.

Tangu nikufahamu wewe tuna miezi kama mitatu sijawahi hata kukushika nywele kama kunakitu nimekifanya kwako ni kukushika mkono tu kitu ambacho hata marafiki wanakifanya sikuwahi hata kukuleta kwangu kwa kuwa najua ni mke pekee ndie anaestahili kupajua nyumbani kwangu.

Dada huku akilia akamwambia mbona ulikua unanihonga? Yule kaka akacheka akasema sikuwahi kukuhonga mimi nilikua nakupa kama rafiki na sababu ya kukunyima angali ninacho sijafundishwa hivyo na usidhani kama nitamuoa rafiki yako alafu wewe ukiniomba nitakunyima hapana nitakupa kama ninacho ila katu sitokupa kipaumbele kuliko mke wangu. Mke wangu akiridhika kwa nilichompa basi nawe utapata, basi yule dada akamwambia siwezi kumwambia rafiki yangu watanicheka mno wote wanajua wewe ni bwana wangu siwezi naomba unipende mimi kaka yangu.

Yule kaka akamwambia siwezi kukupenda wewe kama mke wangu sina hisia hizo kwako na usiogope kumwambia ni bora ukaseme wajue wewe uliuelewa upendo wangu vibaya watakubembeleza na kukufariji, kuliko kukaa kimya maana mimi nitakapokutana na rafiki yako popote nitamwambia tija ya moyo wangu nae atakapo nikataa kwa kudhani mimi ni shemeji yake nitamuelewesha jins gani mimi tulivyo na ili kujitetea ili kumpata nimpendae nitaingia ndani zaidi na kumweleza kuwa nilikutuma wewe ujumbe huu na hukuufikisha.

Hapi ndipo rafiki zako watakudharau na kukukebehi watakuletea maringo ya waz iwazi na utajiona huna thaman. kuelewa vibaya sio tatizo ila tatzo linakuja pale ulipogundua kuwa ulichokielewa sicho nawe ukang'ang'ania.

Yule dada aksmjibu sasa kwanini hukunipenda mimi wakati ndo ulitangulia kuniona? Yule kaka akamjibu sio kila kilichopo mwanzo kinastahili kuna vingine vyenye kufaa vipo kati na hata mwisho kikubwa usiwe na haraka katika kufanya maamuzi nikuulize swali dada? Yule dada akamjibu ndio niulize, yule kaka akamwambia hapo ulipo unausichana wako? Yule dada akamjibu hapana, kaka akamuuliza ni nani alieutoa? Yule dada akamjibu mpenzi wangu wa kwanza, yule kaka akamuuliza yupo hai au amekufa? Yule dada akamwambia yupo hai na mpenzi wake mwingine.

Basi yule kaka akamwambia KWANINI HUKULAZIMISHA NDOA KWA MTU ALIYETANGULIA KUUJUA UNDANI WAKO NA UJE KULAZIMISHA NDOA KWANGU MIMI MTU NILIETANGULIA KUZIJUA TAMAA ZAKO?

Rafiki yako alikua mstaarabu sana kati ya marafiki zako wote, hakunywa pombe, hakuupenda mziki mlimlazimisha tu kuja mara nyingi alikua ni mtu wa kukaa chini, mara kwa mara alisisitiza tirudi nyumbani. Hata tulivyokua tukiondoka alinambia ni vema na wewe umeenda kupumzika maana umechoka pia sisi nyumbani tutakwenda wenyewe sio mbali na hapa tukichukua tax wote mlimbeza na kumwabia hebu huko hiyo ndo kazi ya mwanaume tupeleke utupe na hela ya supu kesho.

Hivi mlimpata wapi rafiki kama yule mbona haendani na ninyi? Yule msichana huku akilia akajibu yule ni house girl wetu huwa napenda kutoka nae ili baba na mama wasihisi nakwenda kufanya mabaya huko niendako. Basi yule kaka akamwambia nenda kamwambie house girl wenu kuwa NAMPENDA SANA AJE KWANGU AFANYE KAZI YA KUNIPENDA KWA DHATI NAMI NITAMLIPA UPENDO.

#Js

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaa haaa Haaa teeeh teeeh teeeh , [HASHTAG]#Ushimen[/HASHTAG], unachekesha sana mkuu.

Haya, ngoja aje mrembo akuombe 500k ndipo tutajua kweli wewe au unatupa jiwe kwenye mzinga wa nyuki pasi na mbio ama mto wa kujizamisha.
Acha utani mkuu. 500k sio kitu cha kitoto
 
Back
Top Bottom