Jifunze kitu hapa: Hii hapa Taarifa ya mwanaume aliechomwa moto na mwanamke wake (mchepuko)

Ramon Abbas

JF-Expert Member
May 4, 2021
1,964
3,900
Jamaa huyo maarufu kwa jina la Zungu ameuliwa kwa kuchomwa moto na mpenzi wake huyo kwa jina la Neema. Tukio limetajwa kutokea huko Mbezi Makabe, Dar jana usiku.

Sababu inadaiwa ni jamaa kutokuwa mwaminifu katika mapenzi yao ndipo mdada anadaiwa kumfungia ndani jamaa kisha kumwaga petrol na kuunguza nyumba inayodaiwa kuwa ya baba wa mdada huyo.

Kabla ya tukio hilo jana, inadaiwa Neema aliweka status mtandaoni kuashiria atafanya tukio baya huku katika status hizo akisema mtanisamehe

Zungu ambaye ametajwa kuwa kinyozi huko Mbezi, kwa upande mwingine anadaiwa alikuwa na mke na watoto wawili hivyo Neema alikuwa mpenzi wake mwingine. Kwa mujibu wa walioshuhudia nyumba ikiungua wamesema walikuwa wakisikia sauti ya Zungu akimuomba Neema amsamehe na amfungulie mlango asifariki lakini moto uliochagizwa kwa petrol unadaiwa ulikuwa mkubwa

Neema tayari inadaiwa amedakwa yupo polisi.

Je, kitendo alichofanya Neema ni sahihi?

Nini maoni yako?

FB_IMG_1626501750115.jpg
 
Uzinzi mbaya sana. Kweli mshahara wa dhambi ni mauti jamaa kapokea mshahara wake. Tamaa siku zote huzaa dhambi jamani tuziongeleshe tamaa zetu. Tuzikemee kwa capital letters.

Leo hii jamaa kaacha familia nyuma sikitiko. Semesha moyo wako kuridhika. Tujifunze kutosheka la sivyo kizazi kitateketea. Wanaokufa ni wanaume, nguvu kazi ya taifa...adui atapita kirahisi kwenye taifa ikiwa population ya wanaume ni ndogo. Tamaa tamaa tamaa si nzuri.

#mwenyekusikianaasikie#
 
Hamna kitu kizuri kama uwazi kwenye mapenzi...

hata wanaume wenye Mke na una mchepuko....tafuta njia ya kumpooza mkeo na kumpunguzia mshtuko....asidhani yuko peke yake!!!

kila mtu anapokea jambo tofauti.,
 
Nikianza ku imagine kwa circumstances ya tukio naona kama hata mchizi kafa kizembe

Yani demu anawasha moto we uko ndani baada ya ku fight utoke unaanza kumuomba afungue mlango?

Hapo ningekua mimi vyombo vya habari headlines zingeandika the return of koyla.

Yani ningepita na mlango huku nawaka kama sharukan
 
Nikianza ku imagine kwa circumstances ya tukio naona kama hata mchizi kafa kizembe

Yani demu anawasha moto we uko ndani baada ya ku fight utoke unaanza kumuomba afungue mlango?

Hapo ningekua mimi vyomba vya habari headlines zingeandika the return of koyla.

Yani ningepita na mlango huku nawaka kama sharukan
Wanaume wa chipsi mayai nguvu wanatoa wapi? Amevuna alichopanda
 
Back
Top Bottom