Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Wakuu ebay ni sehemu ambayo wauzaji(Seller) na wanunuaji(Buyer) wanakutana
Muuzaji(Seller) anajiunga kwa kufungua Account ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa popote pale Duniani
Mnunuzi(Buyer) anajiunga kwa kufungua Account ebay popote alipo Duniani kisha anachagua bidhaa nayoitaka iliyotangazwa na Muuzaji(Seller) ana inunua online.

Ili kukamilisha zoezi la malipo na kuuziana bila kuibiana ndio sasa anaingia Pay pal
Pay Pal
ni njia ya malipo ambapo mtu yeyote anajiunga ili mradi awe ni mteja wa Bank inayotoa Card za Master au Visa Card
Kibongo Bongo CRDB wapo vizuri, baada ya kufungua Acc na kupewa Master/Visa Card yako unarudi tena CRDB kuomba wai link Master/Visa Card yako iweze kufanya online Transaction kwa kujaza form maalumu then you're done

Baada ya kadi yako kuwa Linked unajiunga kwa kufungua Acc Pay Pal kwa maana ya kwamba unawapa details za Account yako na kuwapa ruhusa kutoa pesa kwenye account unapo waomba kufanya hivyo

Jinsi ebay na Pay Pal wanavyofanya kukamilisha mpango mzima
ebay
ni kama soko ambalo watu hawaonani, mmoja yupo Hong Kong anauza iphone mwaingine Yupo Manzese Tz anataka kuinunua lakini wanakuta online through ebay. so huwezi ukamtumia tu mtu hela kwenye acc ya bank maana anaweza kuingia mitini na asiwepo wa kufuatilia
Sasa wanapotaka kulipana Pay Pal anaingia katikati kama bima wa malipo kwa kuhakikisha anamjua vyema Muuzaji(Seller) ambaye ndio mlipwaji

Mlipaji aka Mnunuzi(Buyer) aliyeko Manzese hamlipi direct mlipwaji aka Muuzaji(Seller) aliyeko Hong Kong,
Anachofanya Mnunuzi(Buyer) anampa ruhusa Pay Pal atoe pesa kwenye Acc yake ya bank kutumia Master/Visa kisha amlipe Muuzaji(Seller)
Kwakuwa Pay Pal anakuwa amechukua dhamana ya malipo ya mauziano yenu anawajibika kuhakikisha Muuzaji(Seller) ana bidhaa kweli anayouza na anaaminika atatuma kwa Mnunuzi(Buyer) kile alicho tangaza,....Fail to do so basi Pay Pal atawajibika kumrudishia Mnunuzi(Buyer) pesa yake, na baada ya hapo Pay Pal kushirikiana na ebay ndio watao mtafuta na kumbana Muuzaji(Seller) kwa utapeli alioufanya lakini wewe utakuwa tayari umerudishiwa pesa yako iwapo watajiridhisha kuna uvunjifu wa makubaliano.

CHANGAMOTO

Mara chache sana inaweza kutoke Muuzaji(Seller) akawa tapeli maana ili uwe Muuzaji ni lazima lazima ebay na Pay Pal watataka kujirisha lakini changamoto ipo baada ya kurudishiwa pesa zako
Mifumo ya Pay Pal yetu wanasema hairuhusu kupokea Pesa maana mabank nasikia sijui hayajaingia mikataba gani I dont know, so kibongo bongo acc zetu za pay pal ni kwa kulipia tu na si kupokea pesa(wataalamu watatusaidia katika hili)

Jambo lingine ni wizi wa mizigo Posta, binafsi ni muhanga wa hili.
Mwaka juzi niliagiza BlackBerry yangu lakini ilipotelea Posta na sijaipata hadi leo, nilianza kumsumbua Buyer lakini alinithibitishi mzigo umetumwa na hadi tarehe ulipopekelewa Bongo, nilipo wabana Posta wakaanza kunizungusha tu.
Na hii ndio maana Buyer wengi hawatumi(ship) mizigo Africa maana Posta za kiafrica ni majanga kwa wizi na hasa ukituma vitu vidogodogo vya thamani ya kuonekana kama Simu kamera nk, mara nyingi wana iba

Kuna baadhi ya items ukiagiza utakutana na mkono wa TRA, hawa jamaa ni wasumbufu balaa ukiingia kwenye kumi nanane zao, watakutwanga makodi hadi uchanganyike au la sivyo ukate "kitu kidogo"

Hakikisha unaangalia Feed back na Reputation ya Muuzaji(Seller)
Hakikisha unasoma kwa makini na kuelewa discription ya item, ikiwezekana muulize Buyer kama hujaelewa.
Epuka kutumia njia zingine zaidi ya Pay Pal kama means ya malipo.Unaweza ku bid item alafu ukashangaa unapoke email ianakuambia ipo items kama hiyo kwa bei ndogo......usi jaribu

Shipping nayo ni topic ndefu kidogo natumai wapo wadau wataifafanua vizuri
Mkuu Paul, kwa hakika unastahili pongezi kwa kutumia muda wako wa thamani kutusaidia wanaJF wenzako kwenye jambo hili. Ahsante sana, you have my salute.
 
Hawa bancabc Mbona hawaeleweki nimeweka salio la tsh 397,000
nikanunua xiaomi redmi pro kwa dola 164.14 pamoja na shipping fee.
Nilitegeme itabaki ninunue case ila nashangaa imebaki 3758.20 kwa maana kwamba Jamaa wamefyeka buku 33 hivi.
Sielewi wametumia njia gani kucalculate?
Maana kule aliexpress thamani ni sawa na tsh 359,998
Sijaelewa huu mchezo ni kwangu tu au wote tunakumbana na jambo kama hili?
IMG_20180826_154530.png
 
View attachment 847511
Nenda bank print statement utaona hiyo hela imetumika vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mtandao gani wa gharama nafuu kuanzia bei na gharama za usafirishaji,kwa mtu anayetaka kununua mzigo wa jumla kama USB Flash,memory cards,charger kwa ajili ya kusambaza kwa wateja
 
Hawa bancabc Mbona hawaeleweki nimeweka salio la tsh 397,000
nikanunua xiaomi redmi pro kwa dola 164.14 pamoja na shipping fee.
Nilitegeme itabaki ninunue case ila nashangaa imebaki 3758.20 kwa maana kwamba Jamaa wamefyeka buku 33 hivi.
Sielewi wametumia njia gani kucalculate?
Maana kule aliexpress thamani ni sawa na tsh 359,998
Sijaelewa huu mchezo ni kwangu tu au wote tunakumbana na jambo kama hili?
View attachment 847511
Hiyo ni kawaida kabisaa! Online rates zipo juu ukilinganisha na za banks. Na bei inayoandikwa kwa TZS kwenye hii page ya aliexpress ni Approximate tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa bancabc Mbona hawaeleweki nimeweka salio la tsh 397,000
nikanunua xiaomi redmi pro kwa dola 164.14 pamoja na shipping fee.
Nilitegeme itabaki ninunue case ila nashangaa imebaki 3758.20 kwa maana kwamba Jamaa wamefyeka buku 33 hivi.
Sielewi wametumia njia gani kucalculate?
Maana kule aliexpress thamani ni sawa na tsh 359,998
Sijaelewa huu mchezo ni kwangu tu au wote tunakumbana na jambo kama hili?
View attachment 847511
Hiyo USD 164.14 = TZS 373,992.9851

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo USD 164.14 = TZS 373,992.9851
Bank rate tena iliyotumika hapa ni ndogo: 1usd = TZS. 2,278.500060923602

Muda mwingi huwa iko hivi
1usd = TZS 2,382 ( kwa paypal)

1usd = TZS 2422 ( iwapo utatumia amazon pay)

SPYMATE haujaibiwa rate iko sawa, Exchange rate ni moja ya changamoto kwa wanaofanya manunuzi mara kwa mara online.
 
Kwenye AliPay rates zao kweli ni changamoto, but kwenye PayPal na Amazon Pay wameweka bayana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom