Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni


msauziy

msauziy

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Messages
386
Likes
313
Points
80
msauziy

msauziy

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2017
386 313 80
Bank rate tena iliyotumika hapa ni ndogo: 1usd = TZS. 2,278.500060923602

Muda mwingi huwa iko hivi
1usd = TZS 2,382 ( kwa paypal)

1usd = TZS 2422 ( iwapo utatumia amazon pay)

SPYMATE haujaibiwa rate iko sawa, Exchange rate ni moja ya changamoto kwa wanaofanya manunuzi mara kwa mara online.
Kwenye AliPay rates zao kweli ni changamoto, but kwenye PayPal na Amazon Pay wameweka bayana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mnyamamkalisana

mnyamamkalisana

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Messages
274
Likes
100
Points
60
mnyamamkalisana

mnyamamkalisana

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2018
274 100 60
chief pole na majukumu?nna samsang s5 screen ilivujia wino.siwezi pata cha kuliplace cha bei nafuu?
Mkuu, nshangua online purchase account ya CRDB nmedownload app ya PayPal but inaniomba zip code 1&2,nafanyaj hapo msaada Mkuu
 
mnyamamkalisana

mnyamamkalisana

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Messages
274
Likes
100
Points
60
mnyamamkalisana

mnyamamkalisana

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2018
274 100 60
Naskia muuzaJ anapokea Pesa zake pind iwapo utapokea mzgo wako, je atajuaje kama umepata?
 
mnyamamkalisana

mnyamamkalisana

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Messages
274
Likes
100
Points
60
mnyamamkalisana

mnyamamkalisana

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2018
274 100 60
BID
Ni kwa bidhaa zilizo kwenye mnada

Utaratibu wa mnada nadhani unafahamu.

Mwenye dau kubwa hadi muda wa mnada kuisha ndiye inatakiwa alipie bidhaa husika.
Duh! Mbna karbin zote huandkwa hvo nafanyaj kupata cheap ili na mm niuze npate faida?
 
Edward Mangapi

Edward Mangapi

Member
Joined
Jul 29, 2018
Messages
91
Likes
40
Points
25
Edward Mangapi

Edward Mangapi

Member
Joined Jul 29, 2018
91 40 25
1. nenda ebay.com kisha register chagua customer au kama wewe ni muuzaji chagua akaunti ya merchant.

2. kujiunga inabidi kadi yako ya benki (visa/mastercard) iwe imesajiliwa kwanza kununua mtandaoni, kisha nenda paypal.com weka details zako na za kadi yako kisha watakutumia verification code (yangu nilichukua crdb) hapo kadi yako itakuwa verified tayari na paypal.

3. nenda sehemu yoyote. wanayokubali paypal nunua chochote, ingiza. detail za paypal, watakata gharama za icho kitu basi umemaliza

very easy
Ok
 
Edward Mangapi

Edward Mangapi

Member
Joined
Jul 29, 2018
Messages
91
Likes
40
Points
25
Edward Mangapi

Edward Mangapi

Member
Joined Jul 29, 2018
91 40 25
Kama ni free Standard Int,l shipping au free Economy Int,l shipping kwa kitu kama laptop, kwa ujumla haitafika, ila itaishia mikononi kwa wenye njaa (wafanyakazi mafisadi wa posta). Labda ujaribu EMS(nasikia na yenyewe bidhaa zinaibwa,ni kubahatisha pamoja na kuwa na tracking number), kama hauwezi, wasiliana na seller angalau atume kwa Registered Int,l Airmail ikiwa na tracking number kwa gharama ya ziada US $2 - 4. Ukibahatika, mzigo utafika, la sivyo umelia. DHL,pia EMS na Registered Int,l Airmail za posta zinakuwa na tracking number inayokuwezesha kujua sehemu mzigo ulipofika, muda gani na unafanyiwa nini, pia wakati wa kupokea lazima kusaini ili mtumaji ajue kuwa mzigo umepokelewa. Kwa Posta, pamoja kuwa na gharama nafuu za usafirishaji, mzigo wako ukijulikana matumizi yake au ukawa na thamani kwa aliyeuona, mara nyingi unapotea na hutoupata.
UKitaka uhakika zaidi wa kupata mzigo wako, uwekee bima(mwambie seller awekee bima kwa gharama zako). Ukipotea unalipwa na kampuni ya usafirishaji iliyopoteza mzigo. Ila nao ni wajanja maana wameweka viwango vidogo vya bima wanayoweza kulipa.
Kitu cha kutia moyo na ambacho kinaweza kukufanya uthubutu kununua bidhaa online, iwe eBay, Amazon au popote na ukafanya malipo kupitia wakala wa malipo kama Paypal etc, bila kujali kuwa utapokea mzigo wako au la, ni kuwa, usipopokea mzigo wako au ukiwa tofauti na jinsi ulivotangazwa wakati wa mnada, unarudishiwa pesa yako.
Angalizo:
Ukirudishiwa pesa yako toka Paypal, inabidi usubiri kama mwezi mmoja, ndipo ufuatilie benki iliyokupa Debt card, maana pesa inaporudishwa, inaingia kwenye benki yako (ina-float) na haiwezi kuingia kwenye akaunti yako hadi uende benki ukiwa na vielelezo vya muamala wa pesa iliyorudishwa na Paypal na uandike barua kuomba iingizwe kwenye acc yako au utume email pamoja na vielelezo vya muamala wa mrejesho wa pesa toka Paypal kwenda Huduma kwa wateja wa Debt card husika. Pia itabibdi uwakumbushe mara kwa mara kwa simu. Hakika pesa yako haipotei. Namba za simu za huduma kwa wateja zinakuwa kwenye Debt Card yako. Debt Card namaanisha MasterCard, Visa etc. Kwa upande wa pesa iliyorudishwa toka Paypal kutoingia kwenye Acc yako ni kuwa TZ haiko kwenye orodha ya nchi zinazopokea pesa toka Paypal bali sisi tuaruhusiwa kutuma tu wala si kupokea. Kwa hali hii, si rahisi M-Tz kuuza bidhaa online kwa kuwa hatapata malipo ya mauzo ya bidhaa zake, mpaka apige jalamba muda mrefu. jirani zetu Kenya wao wamo kwenye orodha ya kutuma na kupokea pesa toka Paypal.
Pia unapotaka kununua bidhaa, ni muhimu kuangalia Item condition: New, New Other(see details), Used, Manufacturer Refurbished, Seller Refurbished au For parts or not working. Hii inasaidia kuondoa usumbufu wa kununua kitu ambacho hukutegemea, na baadae kusumbuana na muuzaji kuwa kakuuzia kitu ambacho sicho kumbe wewe ndo hukuangalia vizuri condition ya kitu. Mfano: Umeona laptop imetangazwa New Other(see details) na ina bei ndogo sana kulinganisha na iliyotangazwa New,wewe ukakurupuka ukadhani ni mpya kwa kuona neno New, ukanunua. Imekula kwako, maana imetangazwa ni mpya lakini inaweza kuwa na michubuko, au ni mpya toka kiwandani lakini ni mbovu.
Conditions
New

A brand-new, unused, unopened, undamaged item in its original packaging (where packaging is applicable). Packaging should be the same as what is found in a retail store, unless the item is handmade or was packaged by the manufacturer in non-retail packaging, such as an unprinted box or plastic bag. See the seller's listing for full details.

New other (see details)

A new, unused item with absolutely no signs of wear. The item may be missing the original packaging, or in the original packaging but not sealed. The item may be a factory second or a new, unused item with defects. See the seller's listing for full details and description of any imperfections.

Manufacturer refurbished
An item that has been professionally restored to working order by a manufacturer or manufacturer-approved vendor. This means the product has been inspected, cleaned, and repaired to meet manufacturer specifications and is in excellent condition. This item may or may not be in the original packaging. See the seller's listing for full details.

Seller refurbished
An item that has been restored to working order by the eBay seller or a third party not approved by the manufacturer. This means the item has been inspected, cleaned, and repaired to full working order and is in excellent condition. This item may or may not be in original packaging. See the seller's listing for full details.
Used
An item that has been used previously. The item may have some signs of cosmetic wear, but is fully operational and functions as intended. This item may be a floor model or store return that has been used. See the seller's listing for full details and description of any imperfections.

For parts or not working
An item that does not function as intended and is not fully operational. This includes items that are defective in ways that render them difficult to use, items that require service or repair, or items missing essential components. See the seller's listing for full details.
Ok
 
Edward Mangapi

Edward Mangapi

Member
Joined
Jul 29, 2018
Messages
91
Likes
40
Points
25
Edward Mangapi

Edward Mangapi

Member
Joined Jul 29, 2018
91 40 25
Habari ya Leo wanandugu, Naomba mnisaidie ushauri, Nilinunua calculator (CASIO FX-9750GII GRAPHING CALCULATOR) tarehe 3/1/2018 katika ebay, Ilikuwa inatoka Lithuania,Europe kuja Tanzania. Kutokana na tracking app ninayotumia (17track) Mzigo uliondoka tarehe 6/1/2018 kutoka ulaya. Tarehe 24/1/2018 mzigo ulifika Johanesburg International Mail Center, SouthAfrica (JIMC, ZAJNBA). Tangu siku hiyo mzigo haujatembea tena hadi leo (16/2/2018). Ila tarehe 6/2/2018 niliwasiliana na seller akaniambia kwamba nisubirie utafika tu. Nimesubiri wee nikaona hapana. Nikatuma email kwa JIMC hakuna majibu mpaka leo, Jana tar 15/2/2018 nikanunua kifurushi cha kimataifa niwapigie, nimepiga weee mpaka salio limeisha lakini hawakupokea. Inavyoonekana mzigo umetumwa kwa ems na Anwani ipo sahihi na destination inaonekana ni Tanzania. Naombeni ushauri nifanyaje?
Vp ulipata huo mzigo wako hadi sasa?
 
HansMapunda

HansMapunda

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Messages
400
Likes
176
Points
60
HansMapunda

HansMapunda

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2015
400 176 60
Habari ya Leo wadau,

Kuna changamoto nimeipata. Nilikuwa nikitumia kadi ya NMB Tanzanite kununua vitu ebay kwa kupitia paypal kwa muda wa miaka 3. Baada ya kadi kuexpire ile kadi nikapewa kadi nyingine ya Mastercard NMB. Lakini kadi ile inakataliwa kusajiliwa na paypal. Kila nikiingiza paypal inakataa. Niliwasiliana na paypal wakaniambia niwasiliane na bank. Nilivyokwenda benki wakaniambia sijajaza fomu ya kuweza kuruhusu kadi kufanya miamala ya mtandaoni. Nikajaza fomu lakini mpaka leo bado kadi inagoma kusajiliwa na paypal. Naombeni mnisaide kama kuna mtu ana uzoefu na utatuzi wa tatizo hili.
 

Forum statistics

Threads 1,238,893
Members 476,226
Posts 29,335,882