Jifunze hivi, ukitaka kufanya biashara kipindi cha Corona

Nov 26, 2018
14
38
Habari za Kwako Mwana Jamii Mwenzangu!

Natumaini upo poa na unaendelea kujikinga na Corona iliyokuja kwa kasi 2020, Natumaini Mungu atatuvusha!

Wakati China wakiwa wamefunga milango yao na wamerudi makazini na shughuli zikiwa zinaendelea kama kawaida ( masks, sanitizers, kupimwa joto la mwili kila sehemu waendapo) huku biashara zitaendelea japokua tunalazimika kutumia mtandao kwa kufanya manunuzi maana hakuna namna nyingine.

Mambo ya msingi sana ya kuzingatia unapokua unaingia kwenye mtandao wa Alibaba ( mtandao mkubwa na uliozoeleka wa kununua vitu China kwa watu walio mataifa mengine nje ya China) ambapo kwa takwimu za ndani China ju ya hii platform ( mtandao) zinasema asilimia 25% ya "viwanda linavyoonekana" ndiyo viwanda (manufactures/factories) na asilimia 75% ni makampuni ya biashara ( trading companies) ambayo yananunua kutoka kwenye viwanda na kuorothesha bidhaa zao mtandaoni.

Hebu leo tuongelee vitu vya msingi vya kuangalia unapotaka kufanya order yako

1. FAHAMU NJIA ZA KUTAFUTA SUPPLIERS

A. Njia ya Moja kwa moja ( Direct Search )

Hii ni njia nzuri ya kumtafuta supplier wa kichina kwa kuandika moja kwa moja bidhaa au product unayoitaka kwenye sehemu ya kutafuta ( search bar kama inavyoonekana hapa kwa picha .

1. Ingia mtandao wa www.alibaba.com au app kwenye simu ( Ninashauri kutumia PC kuona vitu ving zaidi)
2. Tafuta supplier wazuri hasa wenye medali ya Dhahabu " Gold Suppliers" mara nyingi wanakua na uwezo wa kufanya kazi vizuri watakayopewa
3. Mtafute na anza maongezi nae.


2357466_how-to-buy-from-alibaba.jpg



Katika Njia hii ni vizuri kufahamu na kuangalia sana vitu hivi hapa Chini
1. Supplier ni Verified ( amethibitishwa), Ni Gold Supplier ( Ana medali ya Dhahabu kuonesha watu wa Alibaba wamefika kiwandani kukagua au ofisini na wameonesha kila makaratasi/ documents kwa alibaba), Trade Assurance ( anauwezo wa kulipa kukiwa kuna upungufu wa bidhaa au ubora)


2357479_types-of-suppliers.jpg



Baada ya kuona hivi vigezo vimetimia unaweza endelea kutafuta mawasiliano na wahusika
tafadhali angalia picha hapa Chini.

2357492_wine-tumbler-search.jpg




B. Njia ya Pili ni Kutuma Maombi ya Quotation kutoka kwa Suppliers ( Request for Quotation/ RFQ)

Hii njia wakati mwingine ninaiita njia ya JUMLA, haha, Maana yangu ni kua wewe unatuma maombi ya bidhaa yako unayoihitaji na kutoa maelezo yalio nyooka ( Kama hukuangalia makala yangu "UFANYE NINI UNAPONUNUA KUTOKA CHINA" ) baada ya muda hawa suppliers wataanza kukutumia message na quotation. Hapa utahitaji kusoma mmoja baada ya mwingine ili kujua nani anafaaa.

1. Ingia kwenye mtandao RFP & RFQ Trading Platform | Alibaba.com’s Global Sourcing Marketplace
2. Jaza form yao kama inavyoonesha kwenye picha hapa Chini


2357505_RFQ-sample-1-modified-2.jpg



3. Wasilisha ( Submit )
4. Angalia messages watakazokutumia kwenye message center
5.Tafuta supplier 2-3 wakuongea nao mpaka unampata unaemtaka

ANGALIZO LANGU, Njia zote ni nzuri kutumia pale unapotafuta supplier wa bidhaa zako JAPOKUA KAMA NI MGENI KWENYE HILI ENEO NA UNATAKA KUFAHAMU SUPPLIER WAZURI NINASHAURI UTUMIE NJIA YA PILI (RFQ ) utafanya haraka na pia utapata watu ambao wanataka kufanya kazi na wewe, na ukiweza wachuja vizuri unaweza pata supplier mzuri wa kufanya nae kazi vizuri ( NITAONGEA VIZURI SIKU NYINGINE KIREFU JUU YA RFQ)


2. WEKA VIGEZO VYA KUCHUJA SUPPLIER

a. Angalia Portfolio/ Profile Zao kuona kama hizo bidhaa unazotafuta wanatengeneza

Baada ya supplier wamekwisha kutafuta au umeshawatafuta angalia profile zao na kuona hizo bidhaa wameorodhesha kama bidhaa zao wanazotengeneza.
Kwa uzoefu wangu mara nyingi sana Kama profile/ portfolio haijaonesha bidhaa unazotafuta mara nyingi wanakua wanataka kupokea order na kuwapa kazi watu wengine ( udalali) au wanaweza kushindwa kufanya kama wewe unavyotaka.

Mara nyingi sana ni muhimu ufanye kazi na mtu anaejua nini anafanya

Cheki huu mfano hapa Chini, Mimi nilikua natafuta "wine tumbler" lakini kuangalia profile ya supplier hajaorodhesha kama ni bidhaa yake muhimu!

2357517_product-category_1.jpg



Swali kwanini hajaorodhesha? Nadhani jibu nimesema hapo juu. Hii ni sign kubwa kua anaweza asifanye kile unachotaka vizuri


B. Angalia Mawasilinao Mazuri na Mawasiliano Mabaya.

Ni rahisi sana kujua mtu mwenye uweledi na uzoefu wa kazi yake kwa maelezo anayokupa.
Mara nyingi supplier anafanya vizuri ataeleza maelezo mengi ambayo ni ya muhimu kwenye quotation yake na atakuuliza maswali mengi ya msingi. Tofauti sana na Supplier ambaye hana uzoefu

Njia za mawasiliano unaweza tumia ni hizi hapa Chini. Email, WeChat ( Chinese WhatsApp), WhatsApp na Skype.


2357518_5-channels.jpg




C. Uzoefu wa Biashara

Hii ni muhimu sana Mara nyingi sana watu wanafikiri bei ndiyo kitu pekee cha kuangalia wakati wa kutafuta suppllier ( BADIRISHA MTAZAMO) ni bora ukawa na faida ya kawaida na ukafanya kazi na mtu mwenye bei kubwa lakini ukawa na usingizi kila siku kuliko kufanya kazi na Supplier bei ndogo, ukawa na faida kubwa kwenye margin lakini ukafanya kazi katika mazingira ya kutokua na amani.


Baada ya kutafuta supplier na kufanya kuchagua na kuongea nae natumaini utaingia kwenye maridhiano ya bei ( negotiation), utaomba sample PP ( pre-production sample), utakagua kabla ya mzigo haujafika huku ( pre shipment inspection) utafuta usafirisha ( freight forwarder ) na kupokea mzigo wako ukiwa Tanzania.


Natumaini umejifunza kitu fulani na hii makala.

Tutaendelea kujuzana.

Kama unahitaji mizigo kutoka China, Unataka kukagua mizigo kabla hujatuma, unaweza wasiliana nami kwa simu

+255627637767 , Unaweza pia fika ofisini Mikocheni Hekima Garden, Mikocheni kwa Mawaziri Tukasaidiana.

Uwe na siku njema, Stay home, Stay Safe!
 
Back
Top Bottom