Jifunze hili kwenye hili sakata la ndoa ya Dr. Mwaka na Bakwata

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,513
Salamu zenu...

Dini ya kiislaam ni dini ambayo hakuna kitu kuhusu maisha ya mwanadam hakijawekwa wazi utaratibu wake...

KILA KITU KATIKA MAISHA YA MWANADAM KIMEWEKEWA UTARATIBU KATIKA UISLAAM...KUANZIA KWENYE QUR-AN HADI HADITH ZA MTUME MUHAMMAD صلى الله عليه وسلم.

NDOA, TALAKA, NA MIRATHI NI KATIKA MAMBO HAYO.

Sheria ya kiislaam inaitambua NDOA ni kama agano zito ambalo watu wawili wa jinsia mbili tofauti walioridhiana kihisia,katikati yao YAKAZALIWA MAPENZI NA KUHURUMIANA, Agano hilo huliingia mbele ya Allaah kwa mujibu wa taratibu alizo ziweka Allaah Mtukufu.

QUR-AN 4:21
"mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti(Agano zito)?"

Taratibu hizo tunaita NGUZO ZA NDOA...tunaita nguzo kwa sababu nguzo ndizo husimamisha jengo...na bila nguzo hizo jengo halitosimama tena...hivyo basi...NGUZO ZA NDOA YA KIISLAAM NI HIZI ZIFUATAZO(Bila nguzo hizo HAKUNA NDOA HAPO):-

1. UWEPO WA MKE NA MUME, UWEPO WA MARIDHIANO BAINA YAO, UWEPO WA MAPENZI BAINA YAO.
* Kwenye nguzo hii...tunamaanisha katika UISLAAM HAKUNA NDOA YA KULAZIMISHANA...Kuna ile ada mitaani wanasema eti NDOA YA MKEKA...huu utaratibu kwenye uislaam haupo...ni uhuni tu uliosambaa.
* Lazima MKE aulizwe ni kweli amemridhia na amempenda MUME anayetajwa kuolewa nae...? Na lazima majibu yake LAZIMA YAZINGATIWE. Hali kadhalika kwa MUME. Kinyume chake hakuna ndoa.
*Hivyo basi uislaam umekataza kabisa MZAZI, MLEZI, KIONGOZI au mtu yeyote yule kumlazimisha mtu kuingia katika ndoa asiyoitaka.

Ushahidi ni hoja hizi katika hadith za Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم:
Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Bikira haozeshwi mpaka atakiwe idhini”. Akaulizwa: “Ewe Mtume wa Allaah! Idhini yake ni vipi?” Akajibu: “Kunyamaza kwake” (al-Bukhaariy na Muslim).

Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa msichana mmoja bikira alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuarifu kuwa babake amemuozesha naye anachukia hilo. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akampa hiari (yaani baina kukubali na kukataa) {Abu Daawuud, Ibn Maajah, ad-Daraqutwniy na al-Bayhaqiy}.

Na mfano wake ni ile Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma), ambayo ndani yake ipo ibara: “…akawatenganisha” (an-Nasaa’iy).

Hapa tunajifunza kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم kuwa aliivunja ndoa ambayo BINTI ALIOZESHWA KWA KULAZIMISHWA.

Inaendelea...
 
Salamu zenu...

Dini ya kiislaam ni dini ambayo hakuna kitu kuhusu maisha ya mwanadam hakijawekwa wazi utaratibu wake...

KILA KITU KATIKA MAISHA YA MWANADAM KIMEWEKEWA UTARATIBU KATIKA UISLAAM...KUANZIA KWENYE QUR-AN HADI HADITH ZA MTUME MUHAMMAD صلى الله عليه وسلم.

NDOA, TALAKA, NA MIRATHI NI KATIKA MAMBO HAYO.

Sheria ya kiislaam inaitambua NDOA ni kama agano zito ambalo watu wawili wa jinsia mbili tofauti walioridhiana kihisia,katikati yao YAKAZALIWA MAPENZI NA KUHURUMIANA, Agano hilo huliingia mbele ya Allaah kwa mujibu wa taratibu alizo ziweka Allaah Mtukufu.

QUR-AN 4:21
"mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti(Agano zito)?"

Taratibu hizo tunaita NGUZO ZA NDOA...tunaita nguzo kwa sababu nguzo ndizo husimamisha jengo...na bila nguzo hizo jengo halitosimama tena...hivyo basi...NGUZO ZA NDOA YA KIISLAAM NI HIZI ZIFUATAZO(Bila nguzo hizo HAKUNA NDOA HAPO):-

1. UWEPO WA MKE NA MUME, UWEPO WA MARIDHIANO BAINA YAO, UWEPO WA MAPENZI BAINA YAO.
  • Kwenye nguzo hii...tunamaanisha katika UISLAAM HAKUNA NDOA YA KULAZIMISHANA...Kuna ile ada mitaani wanasema eti NDOA YA MKEKA...huu utaratibu kwenye uislaam haupo...ni uhuni tu uliosambaa.
  • Lazima MKE aulizwe ni kweli amemridhia na amempenda MUME anayetajwa kuolewa nae...? Na lazima majibu yake LAZIMA YAZINGATIWE. Hali kadhalika kwa MUME. Kinyume chake hakuna ndoa.
*Hivyo basi uislaam umekataza kabisa MZAZI, MLEZI, KIONGOZI au mtu yeyote yule kumlazimisha mtu kuingia katika ndoa asiyoitaka.

Ushahidi ni hoja hizi katika hadith za Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم:
Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Bikira haozeshwi mpaka atakiwe idhini”. Akaulizwa: “Ewe Mtume wa Allaah! Idhini yake ni vipi?” Akajibu: “Kunyamaza kwake” (al-Bukhaariy na Muslim).

Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa msichana mmoja bikira alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuarifu kuwa babake amemuozesha naye anachukia hilo. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akampa hiari (yaani baina kukubali na kukataa) {Abu Daawuud, Ibn Maajah, ad-Daraqutwniy na al-Bayhaqiy}.

Na mfano wake ni ile Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma), ambayo ndani yake ipo ibara: “…akawatenganisha” (an-Nasaa’iy).

Hapa tunajifunza kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم kuwa aliivunja ndoa ambayo BINTI ALIOZESHWA KWA KULAZIMISHWA.

Inaendelea...
Uislamu ni mfumo mzima wa maishà wa binaadamu, kila jambo limefafanuliwa, ila kuna wa huni wasio kubari amri za Mungu makusudi.
 
2. UWEPO WA WALII WA MWANAMKE ANAYEOLEWA.
- Katika Uislaam hakuna MWANAMKE KUJIOZESHA MWENYEWE, Yaani hakuna mwanamke kujipeleka kwa mwanaume alafu aseme tayari ameolewa, ni lazima awepo WALII.

WALII ni nani? Walii ni MSIMAMIZI WA YULE MWANAMKE KWENYE MAMBO YAKE...katika Uislaam mwanamke yeyote yule lazima awe katika uangalizi wa WALII wake... Hakuna mwanamke anayejisimamia mambo yake mwenyewe...HAKUNA. na walii huyu ndiye ATAKAYEMUOZESHA BINT NA KUMKABIDHI KWA MUMEWE.

NA Mawalii wa mwanamke wapo katika mtiririko maalum uliopangwa na sheria ya kiislaam...kuna wa kwanza mpaka wa mwisho kabisa...HUWEZI KWENDA KWA WALII WA PILI au WATATU katika MTIRIRIKO wakati WALII WA KWANZA YUPO NA HAJUI KINACHOENDELEA...na wala HAJATOA RUHUSA au KUOMBA KUWAKILISHWA...NDOA HIYO HAITOKUBALIKA KISHERIA.

Na katika suala la ndoa, kuna vigezo mtu awe navyo ili awe WALII ANAYEKUBALIKA, Vigezo hivyo ni:-
1. Awe muislaam.
2. Awe Hai.
3. Awe na akili timamu.
4. Awe amefikia Baalegh.
5. Awe Walii pamoja na bint husika katikati yao kuwe na ndoa sahihi. NDOA NI KIGEZO MUHIMU SANA CHA KUKUBALIKA KWA WALII.
6. Awe anaswali swala 5 zote kwa wakati na kwa JAMAA MSIKITINI NA WAUMINI WENGINE.
7. Awe Muadilifu, maana yake awe mtu ambaye anavyojulikana na kuonekana katika jamii MEMA/MAZURI YAKE NI MENGI kuliko MAOVU YAKE.

* Mtu anapokosa vigezo hivyo hasa cha kwanza, cha pili, cha tatu, na cha nne, na cha tano basi anapoteza sifa ya kuwa Walii...na UWALII UNAHAMIA KWA MWINGINE ANAYEFUATA KATIKA MTIRIRIKO.

Mfano:- Walii akiwa sio Muislaam haozeshi, walii akiwa ameshakufa tunaangalia anayemfuata, walii akiwa MWENDAWAZIMU au akili nusu haozeshi, walii akiwa mlevi, mvuta bangi haozeshi...walii AKIWA HASWALI SWALA 5 HATAKIWI KUOZESHA ABADANI. Bint akiwa amepatikana nje ya ndoa, basi huyo hana Walii...walii wake ni kiongozi wa nchi.

MTIRIRIKO WA MAWALII KAMA ULIVYOELEKEZWA KATIKA SHERIA. Mawalii wa mwanamke wote, Wanatokea upande wa BABA YAKE. Mawalii hawatoki upande wa mama ASILANI.
Na mtiririko huu utazingatia KUTIMIA KWA VIGEZO TAJWA HAPO JUU Hasa kigezo namba 1 mpaka 6, vilevile ZINGATIA HAKUNA KURUKA WALII BILA IDHINI YA MUHUSIKA;-
1. BABA MZAZI wa Binti
, akiwa hayupo au hajakidhi vigezo ataangaliwa
2. BABU MZAA BABA MZAZI wa Binti, akiwa hayupo au hajakidhi vigezo ataangaliwa
3. KAKA wa BINT BABA MMOJA MAMA MMOJA, Akiwa hayupo au hajakidhi vigezo, ataangaliwa
4. KAKA wa BINT BABA MMOJA, Akiwa hayupo au hajakidhi vigezo, ataangaliwa
5. MTOTO wa kiume WA KAKA(yule wa baba mmoja mama mmoja) WA BINT(Yaani shangazi mtu),
6. MTOTO WA KIUME WA KAKA(Yule wa BABA MMOJA TU) Wa BINT(Yaani shangazi mtu).
Wakiwa hawapo hao au hawajakidhi vigezo, ataangaliwa,
7. BABA MDOGO AU BABA MKUBWA( Tunaanza na yule wa BABA MMOJA MAMA MMOJA NA BABA WA BINT...Kisha yule wa BABA MMOJA TU).

SASA IKIWA WOTE HAO HAWAPO AU HAWAJAKIDHI VIGEZO, Mfano:- Bint amesilimu yeye pekee yake kwao, au Bint amezaliwa NJE YA NDOA,
BASI HUYU BINT WALII WAKE NI;-
8. KIONGOZI WA NCHI - Kama kiongozi wa nchi atakuwa na mambo mengi mfano katika nchi yetu ya Tanzania, basi mamlaka haya ya Uwalii ameyakasimisha kwa:-
9. IMAMU WA MSIKITI AMBAO HUSWALIWA SWALA YA IJUMAA...NA WATU WAMEMKUBALI NA WANAMRIDHIA HUYO KAMA IMAMU WAO.
(Japo Bakwata wanalazimisha na hili liwe kwao). Lakini IMAM YEYOTE YULE AMBAYE ANASWALISHA SWALA YA IJUMAA NA ANATOA KHUTBA AU AMETEULIWA NA MAMLAKA ZA KUTEUA IMAM ATAKUWA WALII WA BINT...ATAMUOZESHA BINT.

Hivyo basi mpaka hapa tumeshaona, wenye haki ya kuozesha ni akina nani, kwahiyo unaweza ukaoa bila ya uwepo wa Sheikh, na wala WAJOMBA WA BINT HAWANA LOLOTE KATIKA HATUA HII...NI UJINGA TU NA UJANJA UJANJA.

Ushahidi:
Katika Qur-an 4:25
"فَانكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ" "NA WAOENI WANAWAKE KWA IDHNI YA WATU WAO"

Katika hadith, Amesema Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم،
"
لَاا تُزَوِّجِ الْمَرْأَةُ الْمَرْأَةَ وَلَاا الْمَرْأَةُ نَفْسَهَا فَإِنَّ الزَّانِيَة هِيَ الَّتِي تُزَوِّجُ نَفْسَهَا

"HAJIOZESHI MWANAMKE MWENYEWE AKAJIOZESHA KWA MWANAUME YEYE MWENYEWE AKAJIOZESHA ILA HUYO NI SAWA NA KAHABA, KWA SABABU MAKAHABA WANAOJIUZA NDIO WANAOJITOA WENYEWE KWA WANAUME BILA IDHNI YA WATU WAO."

Inaendelea...Nguzo ya tatu.
 
3. MAHARI.
- Katika uislaam MAHARI NI LAZIMA, NI LAZIMA...LAZIMA...Hili halina hiari wala mjadala kwa upande wa mwanamke wala si kwa upande wa mwanaume...lazima MWANAMKE ANAYEOLEWA APEWE MAHARI YAKE...NA NDOA BILA YA MAHARI HIYO NDOA NI BATILI.

- IZINGATIWE MAHARI NI HAKI YA MWANAMKE ANAYEOLEWA SIO WAZAZI AU YEYOTE YULE...

- Yeye mwanamke anayeolewa ndiye atakayechagua aolewe na MAHARI GANI...NA SHERIA HAIJAMUWEKEA VIDHIBITI VYA KIWANGO CHA MAHARI YAKE...ANAWEZA AKADAI MAHARI YOYOTE KIASI CHOCHOTE ATAKACHO BILA KUBANWA NA SHERIA. ifahamike hivyo kwanza. Hivyo mwanamke hata akisema anataka DUNIA NZIMA iwe mahari yake...kama una uwezo nayo MPE ndiyo haqq yake hiyo.

- Mahari inaweza ikawa yoyote ile, ikawa:
1. Pesa - kiasi cha shilingi kadhaa wa kadhaa inaweza ikawa mahari ya bint, kile atakachotaja bint.
2. Huduma - Bint anaweza akasema nifundishe Quran mpaka sura fulani, hiyo ndio mahari yangu...na itahesabiwa kuwa ni mahari yake.
3. Kitu kizuri atakachotaja mwanamke, mfano KABATI, KITENGE, KITANDA, GAUNI, MKUFU na mfano wake. Vyote hivyo vinaweza kuwa ni mahari.

PAMOJA NA KUACHIWA UWANJA MWANAMKE ANAYEOLEWA KUCHAGUA MAHARI ANAYOTAKA lakini KUNA MAPENDEKEZO KUTOKA KWA MTUME MUHAMMADصلى الله عليه وسلم... MAHARI YENYE UNAFUU ZAIDI NDIO YENYE BARAKA KWENYE NDOA.

Kuna dhana ipo kuwa, ukiolewa kwa msahafu basi ndio ndoa itakuwa na baraka...wengi hata huo msahafu wenyewe hawaufanyii kazi...hapa hakuna kitu... Wengi ni kutaka kujionesha mbele za jamii.

Mtume ameelekeza WANAWAKE TAJENI MAHARI NYEPESI ILI NDOA ZENU ZIWE ZENYE KUBARIKIWA ..lakini si kwamba ukitaja mahari kubwa hautakuwa na baraka...ila ndogo na nyepesi itakuwa na baraka zaidi.

Hamna mtu anaruhusiwa kutumia MAHARI YA BINT BILA IDHNI YAKE BINT MWENYEWE...HAPA WAZAZI WENGI NA WALEZI WANAINGIA KWENYE MAKOSA...WANAKULA MAHARI ZA BINT ZAO KWA DHULMA...

BINT anayeolewa atataja mahari iwe ina thamani ndogo iliyoje au kubwa iliyoje...hiyo ni mahari yake...na atatumia apendavyo...na wala hapangiwi na mtu atumieje, wala asilazimishwe atumie wanavyotaka wazazi.

MAHARI NI KILE ATAKACHOTAJA BINT NA SI WAZAZI AU WALEZI...KILE KINACHOORODHESHWA NA WAZAZI SIO MAHARI...NI NJIA ZA UPIGAJI TU KAMA UPIGAJI MWINGINE TU. NA NI DHULMA. UISLAAM HAUTAMBUI HAYO.

Hapa ndipo linapokuja swali la wanawake wengi ambao wameolewa kwa ahadi ya kupewa mahari baadae... alafu baadae mwanaume akagoma kutoa mahari...hiyo ndoa imevunjika automatically...kwa sababu hakuna ndoa bila ya mahari...ni binti tu ataondoka kama hajapewa mahari yake hata kidogo...kama alitanguliziwa kidogo...hilo ni deni ambalo mume akifa ...lazima likatwe katika mirathi yake apewe mke mahari iliyobaki...HAKUNA MWANAMKE KUDHULUMIWA MAHARI.

NA INAPENDEKEZWA KATIKA TUKIO LA UFUNGISHAJI WA NDOA...MAHARI ITAJWE ILI KILA MTU ASIKIE ILI IJULIKANE NA ISHUHUDIWE NA KILA MTU KUWA HUYU KAOLEWA NA KIASI KADHAA...NA KIMEBAKI KADHAA...ILI SIKU YA SIKU UKIJA KUSEMA HUJALIPWA KILA MTU ATAKUWA ANA UHAKIKA NI KWELI.

LAKINI HIVI SASA WATU WENGI WANAONA HAAYA KUDHIHIRISHA MAHARI WALIYOOLEA ...KWA KUONA AIBU...WANAFUNGA NDOA KWA "MAHARI TULIYOKUBALIANA"...IPI? LAZMA ITAJWE...KUNA LEO NA KESHO.

TAJENI MAHARI ZENU WALA MSIONE AIBU...IKIWA NI CHACHE NI HESHIMA...NA IKIWA NI NYINGI NI HESHIMA ..NI YAKO TU...AIBU YA NINI...ILA MASLAHI YA BAADAE LAZIMA YACHUNGWE...

MAHARI NI DENI KAMA LILIVYO DENI JINGINE...ISIPOLIPWA KWA WAKATI HAPA DUNIANI ..UTAILIPA AKHERA SIKU YA QIYAAMA... ZITACHUKULIWA SEHEMU YA SWALA ZAKO, SWAUMU ZAKO, SWADAKA ULIZOTOA ATAPEWA MKEO ANAYEKUDAI MAHARI...

LIPENI MAHARI MNAZODAIWA NA WAKE ZENU HAPA DUNIANI KABLA HAMJAFA
...NA MKIFA KATENI KATIKA MIRATHI ALIYOACHA MAITI LILIPWE KWANZA DENI LA MAHARI...NDIO MIRATHI IGAIWE...

DENI LA MAHARI HALIFI LABDA MKE ALISAMEHE TU.

USHAHIDI:
Katika Quran 4:4 ALLAAH ANASEMA,
وَءَاتُواْ ٱلنِّسَآءَ صَدُقَٰتِهِنَّ نِحۡلَةًۚ
"NA WAPENI WANAWAKE MAHARI ZAO, HALI YA KUWA NI HAKI YA LAZIMA KWAO".
 
Back
Top Bottom