Jifunze English tenses kwa Kiswahili

CHUO CHA UFUNDI JITA

Senior Member
Feb 8, 2013
116
23
Heshima yenu wakuu, mara nyingi mtu unaweza kuwa mzuri sana kwa grammar lakini tense zikakuumbua. Mathalani;
>She love her dady very much badala ya >she loves her dady very much.

PRESENT SIMPLE TENSE
Pia hujulikana kama everyday tense ikiwa na maana kuwa kitendo hufanyika kila siku.
SHERIA 1
>< Uongezaji wa -s, -es au -ies mwishoni mwa kitenzi (verb) ikiwa imetanguliwa au imetumika noun au pronoun iliyo ktk nafsi ya tatu umoja (he, she, it) au jina kama Daud nk na mara nyingi utakuta maneno kama usually, daily, every....
mfano:
<> She cries everymorning
<> He plays football daily
<> Japhet goes to the market every month
SHERIA 2
Kutoongeza chochote kwenye verb (kitenzi) pale unapokuwa umetumia pronoun au noun za wingi na I kama they, we, you au Amina and Tedy
Mfano;
>< We normally chat
>< our sisters cook food daily
>< I go to the shop usually
>< Juma and Glad play volleyball every sunday

PENYE MAREKEBISHO, MASWALI... KARIBUNI, LENGO TUELEKEZANE PENYE UTATA
 
Pia tunatumiaga "do" na "does" plus verb kama inakuletea shida especially kwenye irregular verbs
 
Heshima yenu wakuu, mara nyingi mtu unaweza kuwa mzuri sana kwa grammar lakini tense zikakuumbua. Mathalani;
>She love her dady very much badala ya >she loves her dady very much.

PRESENT SIMPLE TENSE
Pia hujulikana kama everyday tense ikiwa na maana kuwa kitendo hufanyika kila siku.
SHERIA 1
>< Uongezaji wa -s, -es au -ies mwishoni mwa kitenzi (verb) ikiwa imetanguliwa au imetumika noun au pronoun iliyo ktk nafsi ya tatu umoja (he, she, it) au jina kama Daud nk na mara nyingi utakuta maneno kama usually, daily, every....
mfano:
<> She cries everymorning
<> He plays football daily
<> Japhet goes to the market every month
SHERIA 2
Kutoongeza chochote kwenye verb (kitenzi) pale unapokuwa umetumia pronoun au noun za wingi na I kama they, we, you au Amina and Tedy
Mfano;
>< We normally chart
>< our sisters cook food daily
>< I go to the shop usually
>< Juma and Glad play volleyball every sunday

PENYE MAREKEBISHO, MASWALI... KARIBUNI, LENGO TUELEKEZANE PENYE UTATA

Chart au chat...me najua hyo chart ni ya kwenye majedwari...
 
Uzi mzuri sana. Lakini mkuu Kiingereza hakisomwi kwa kukariri kama hivi. Ukisoma a lot of story books and novels, kiingereza kitakuja chenyewe automatically. Mimi sikuwahi kujifunza english structure zaidi ya kusoma vitabu vingi na kiingereza ndilo somo pekee nililopata A, pamoja na kwamba nilikuwa nachukua sciences.
 
Sentensi hii inaendaje kwa kiingereza? "baba mimi mwanao wa ngapi?"
 
PRESENT PERFECT TENSE

(WAKATI ULIOPO HALI TIMILIFU)
Hii ni tense inayohusisha kitendo kilichofanyika na tayari kimetimia.

SHERIA kuu katika Tense hii ni matumizi ya HAS na HAVE pamoja na matumizi ya PAST PARTICIPLE ambapo verb huongezewa &#8211;ed au &#8211;en na zingine hubadilika kabisa au hazibadiliki kabisa. HAS; hutumika kwa Pronouns au nouns zilizo katika Umoja kama (he, she, it, Juma)
HAVE; hutumika kwa Pronoun au Noun zilizo katika Wingi kama (you, we, they, Juma and Asha na I.) Unapotumia HAS au HAVE kwenye sentensi ni lazima Verb ibadilike na kuwa katika mfumo past participle.

MIFANO
<>We have seen them passing
<>They have written their letters
<>He has eaten all the food

NB: MASWALI YANAYOENDANA NA MADA HUSIKA NDO YATAJIBIWA
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom