Jifunze Digital Marketing in Swahili Series (Season 2)

Aug 22, 2022
9
8
Habari wakuu,

Ninayo furaha kutangaza kurejea kwa series yetu pendwa ya mafunzo ya Digital marketing kwa lugha ya Kiswahili.

Nilikuwa active sana humu mwaka 2020 na mwaka jana mwanzoni...

Nikapotea kutokana na Majukumu ya kazi na projects nilizopata

Lakini nna furaha kuona watu walijifunza, na kuna baadhi nimefanya nao kazi since 2020 mpaka Leo

Plus wale ambao wamesoma thread ile ya kwanza ya Digital marketing,na kunitafuta mwaka huu

Nina habari njema kwa wote

Nimerudi kwa ajili ya kuendelea pale tulipoishia,

Karibu katika Season 2 ya Digital Marketing in Swahili

Nitakuwa hapa kushea nanyi maarifa,ujuzi na mbinu zinazotumika kufanya Matangazo ya biashara Mtandaoni

Ukweli usiopingika ni kwamba Biashara mpya zinafunguliwa kila siku,

Wafanyabiashara wanatafuta wateja,Kila mtu anataka kuuza..

Kama wewe ni Mfanyabiashara..

Niko hapa kwa ajili ya kushea na wewe yale Nnayofahamu katika Social media marketing, Sponsored Ads na Digital marketing kwa ujumla

Naamni ukijifunza mbinu za uhakika za kufanya Matangazo,utakuwa na uwezo mkubwa wa kujitofautisha sokoni,

Utafanya Matangazo ya uhakika, sio kubahatisha tena, na utaweza kuongeza mauzo yako kwa kuvutia wateja zaidi.

Karibun sana and stay tuned kwa Threads zinazokuja

PS: Kama una swali lolote au Changamoto kuhusu Sponsored Ads, uliza hapa nitakujibu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom