Jifunze baadhi ya Application zitakazokusaidia kuwa salama katika simu yako

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Cerberus Program: Hii ni Programu Tumishi (Application) itakayokusaidia pale simu yako inapoibwa. Kupitia Cerberus utaweza kufunga simu yako na kufuta taarifa zako endapo simu yako itakuwa imechukuliwa na wahalifu au watu wasio sahihi

X-Privacy: Hii itakusaidia kuzuia taarifa zako zisivuje au kuchukuliwa na watu wengine kupitia mtandao. Zipo 'application' ambazo kukusanya namba za simu na Email za watu bila ya wao kijua basi X-privacy itakusaidia kuzuia (ipo ya bure na ya kulipia)

Cryptonite: 'Application' hii itakusaidia kutengeneza 'file' lenye ulinzi ndani ya simu yako ambalo utalitumia kuhifadhia taarifa zako nyeti

Surespot: Hii ni 'application' kwa ajili ya kutuma jumbe. Inakuruhusu uwasiliane na Mtu bila ya kuhusisha namba yako wala Email yako. Inatumia 'Internet'

Spideroak: Pia, kwa kutumia 'application' hii itaweza kuhamisha taarifa zako kutoka kwenye simu kwenda kwenye kompyuta kwa usalama zaidi. Application hii inahakikisha mchakato mzima unakuwa salama

Panic Button: Hii itakuwezesha kutuma ujumbe wa SMS kwa siri na haraka kwenda kwa watu wako wa karibu uliowachagua pale unapokuwa kwenye mazingira hatarishi au unakaribia kuwa mikononi mwa watu wasiojulikana

Moja ya taarifa itakazozituma ni pamoja na sehemu uliyopo kwa wakati huo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom