Jifungie zako ndani, tazama filamu hizi

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,430
23,750
It's been a damn long time kiunga hiki, hope mko poa nyote, karibuni tena uwanjani hapa tupendekezeane filamu nzuri za kutazama katika kipindi hiki cha weekend, na hivi mvua inanyesha ukikaa zako ndani unafurahia muda wako to the maximum!


Tazama hapa ....


1. THE 8th NIGHT
dd133ffc3d2439016a128471721513c9.png


Miaka alfu mbili na mia tano ilopita palipata kutokea vita kali baina ya Buddha na shetani aliyetaka kuifungulia Jehanamu duniani ili watu wapate kuteseka, vita hiyo ikadumu kwa muda mfupi kwani Buddha alibaini chanzo cha nguvu kubwa ya shetani huyo kuwa ni macho yake mawili yalopamoja, moja jeusi na jingine jekundu, hivyo akayang'oa na kuyatenganisha kwa moja kulipeleka mashariki ya mbali na jingine kulipeleka magharibi ya mbali ili yasije kupatana kamwe!

Na huko akawapa watumishi wake wawili wapate kuyachunga. Amani ikarejea siku na siku, wiki na wiki, miezi na miezi na miaka na miaka mpaka mwaka wa sasa ambapo Profesa mmoja wa historia anakumbana na mkebe mmojawapo wenye jicho lililofichwa katikati ya jangwa. Haamini macho yake! Kumbe habari zile za kale ni kweli? Kila mtu alidhani ni hekaya tu!

Anahabarisha watu na wanataaluma wenzake lakini hakuna anayemwamini, hamna uthibitisho wa hayo anayoyasema, wanamwona ni mwehu anayesema porojo hivyo anapoteza hadhi na kazi yake, kitu hiki kinamuuma mno, anakumbwa na sonona, sasa anaadhimia kuuthibitishia ulimwengu kuwa maneno yake ni kweli kwa kuutoza gharama kubwa ... gharama ya maisha ... Anajitoa sadaka ili apate kuamsha jicho lililolala, baada ya hapo jicho hilo linakuwa likihama mwili kwa mwili kusaka jicho lingine la pili ili yapate kukamilika, na punde hayo yatakapotimia basi shughuli iliyomalizwa miaka alfu mbili ilopita inaanza upya! Tena hivi sasa Buddha mtetezi akiwa hayupo tena.

Sasa nani wa kuzuia hilo katika usiku wa nane wa kupata kwa mwezi ili haya yasipate kutimia? Ni binadamu gani ataweza kupambana na nguvu hii ya kifo kunusuru walimwengu?

Patashika.

f8a4f6a15b0693b2ba949a162f79f3c6.png

---
2. THE GROTESQUE MANSION or THE GHOST MANSION (2021)
d8a1c5def4b8fc0f2eb69f45ad519820.png


Msanii ambaye anahangaika kujenga hadhi yake katika uchoraji wa mtandaoni, haswa baada ya kazi yake ya kwanza kufeli vibaya, anajikuta akiangukia kwenye mikono ya bwana ambaye anahusika na kutunza jengo moja kubwa na kuukuu kwa lengo la kupata hadithi kali itakayoendana na mikono yake ya uchoraji.

Kilichomvutia mwandishi huyo kufika kwenye jengo hilo ni habari zake ya kwamba kuna watu kadha wa kadha wamepotea kimaajabu katika jengo hilo na hata wengine wamefia humo katika mazingira tatanishi.

Sasa huko anakutana na bwana mmoja mzee, yeye ni 'caretaker' wa jengo hili, na bwana huyu baada ya kushawishiwa na kijana huyu mchoraji, anaamua kufunguka juu ya yale yaliyotukia katika jengo hili, moja baada ya jingine, huku kijana akirekodi kuhakikisha hakuna kinachompita.

Ndo' mzee anasimulia mkasa kwa mkasa, chumba kwa chumba, akianza na chumba alichokaa mwandishi kisha chumba alichokaa muuza dawa (pharmacist) alafu akaja kwenye chumba alichokaa dalali wa majengo.

Kila chumba kina hadithi na mkasa wake, mikasa hiyo ndo' filamu yenyewe, mikasa ya kushangaza kabisa, mambo ya kuacha kinywa wazi, mwandishi anayanakili na kwenda zake akiwa amepata hadithi kabambe.

Anaifanyia kazi hadithi hiyo na kisha kuikabidhi kwa mchapaji, mchapaji naye anaipenda , anamuahidi pesa nzuri tu, lakini anamtaka bwana huyo airefushe hadithi yake kwani ni fupi sana, hivyo bwana mchoraji akalazimika kurudi tena kwa mzee yule ili aendelee kumhadithia mikasa ya vyumba vingine, mzee akawa mzito, mchoraji akamsihi akimuahidi yupo radhi hata kumlipa.

Lakini kurudi kwa bwana huyu hakukua na jema na hakutamuacha na jema ... Round hii, si tu kwamba anasimuliwa mkasa bali anapewa na ufunguo wa chumba aende kujionea kwa macho yake na kusikia kwa masikio yake ...

Kadiri alivyofukua mambo hayo ili apate hadithi, anajikuta naye anazamia humo, anazamia katika shimo ambalo hatoweza kutoka tena ... abadani.

Screenshot_20221126-154151.png

---

3. CHOOSE OR DIE (2022)
images.jpg

Kama uliwahi kutazama na kupenda mahadhi ya BLACK MIRROR, NO ESCAPE ROOM na JUMANJI, basi tenga tena muda wako kwaajli ya filamu hii ...

Kwasababu ya ukata wa familia yake, binti Kayla analazimika kuacha chuo ili atafute kipato kwa kufanya kazi ndogondogo za usafi, kazi ambazo bado hazimpatii kipato cha kueleweka kukimu mahitaji.

Huku mama yake akiwa ni mtumiaji sugu wa madawa ya kulevya na muda si mrefu ametoka kumpoteza mdogo wake wa kiume kwa kuzama kwenye bwawa la kuogelea kwasababu ya kutokuwa makini kumchunga na kama haitoshi mwenye nyumba amekuwa ni msumbufu sana, Kayla anajikuta akiingiwa na shauku ya kucheza game la CURS>R, game ambalo alilikuta katika ofisi ya rafiki yake (Isaac), baada ya kubaini game hilo lina zawadi nono ya pesa kwa atakayeshinda, pesa ambazo ni dhahiri zitatatua kila changamoto alokuwa nayo.

Lakini taratibu, katika mahangaiko hayo, Kayla anajikuta akizama katika mtego wa maisha yake kwani badala ya yeye kucheza game, hali inakuwa kinyume, game linamcheza yeye! Kila baada ya muda, anapata machaguo mawili magumu sana ambapo analazimika kuchagua mojawapo, na ni lazima achague la sivyo atakufa, na ajabu ni kwamba kila analolichagua linatokea dhahiri shahiri mbele ya macho yake ikiwemo watu kufa!

Kutoka hawezi, kila anavyosonga mbele hali inazidi kuwa tete. Ni wazi hana 'option' nyingine zaidi ya kupambana kujinasua, lakini kivipi?
images(1).jpg

---

4. BLOOD RED SKY.

3b84e5231409e249ae9a2edf6848c93b.png

Pale ndege inapogeuka kuwa jeneza.

Mwanamke mjane, Nadja, pamoja na mwanae mdogo wa kiume, Elias, wanajiandaa kupanda ndege inayoelekea jiji la New York, Marekani, kwaajili ya Nadja kuifuata tiba ya ugonjwa fulani unaomsumbua, anaongea na dokta kwenye simu na dokta anamhakikishia kuwa atapona kabisa punde tu atakapopata tiba kwahiyo kilichobakia ni yeye tu kuwasili hospitali.

Nadja anapanda ndege kwa matumaini lakini muda si mrefu matumaini yake yanaingia doa baada ya kubaini ndege imetekwa na magaidi wanaosisitiza kuwa hawatamwacha mtu yeyote hai mpaka pale kiasi fulani cha pesa kitakapotumwa kwenye accounts zao!

Kwa kuogopa, Elias anakimbia akajifiche sehemu salama, Mama yake (Nadja) anajaribu kumzuia lakini inakuwa 'too late', gaidi mmoja anamwona na kummiminia risasi zinazomlaza chini akimwaga damu pomoni!

Kwa majeraha hayo ni wazi Nadja amekufa, na ni kweli alikuwa amekufa lakini shida akaamka akiwa kiumbe kingine mbali na binadamu! Hapo ndo' upande wake wa wa pili wa ugonjwa unapoonekana, ugonjwa ambao kama magaidi wangeufahamu basi huenda wasingethubutu kumtupia risasi.

Muda si mrefu ndege inalowa damu, ugonjwa unasambaa kwa wengine na kufumba na kufumbua chombo hicho kinageuka kuwa ulingo wa kupambania maisha huko angani!
7efb191f3911bb0ec9cb1bc8c9c33814.png

---

5. MR HARRIGAN'S PHONE.
images(2).jpg

Popote pale utakapoona filamu imetokana na vitabu vya Stephen King, usijiulize mara mbili kuitazama. King ndiye mwandishi bora kuwahi kutokea duniani katika tanzu ya 'Horrors'. Filamu ya IT, IN THE TALL GRASS, PET CEMETARY, CARRIE, THE SHINING, FIRESTARTER na kadhalika na kadhalika ni kazi ya mikono yake. Humo ndani ni hatari sana.

Stephen King hakupi tu filamu ya kutisha bali anakupa filamu ya kutisha yenye hadithi tamu ndani yake, in-depth plot, tofauti na filamu nyingi za kutisha zenye visa dhaifu huku zikitegemea zaidi 'scenes' za vitisho vya hapa na pale.

Filamu hii ya Mr Harrigan's Phone inamhusu kijana aitwaye Craig ambaye anapata kutengeneza mahusiano ya karibu mno na tajiri mkubwa (bilionea) aitwaye Mr. Harrigan, tajiri ambaye yuko kingoni mwa maisha yake kwasababu umri umeshamtupa mkono.

Tajiri huyo kwasababu ya uhafifu wa macho yake ya kizee, alimuhitaji Craig nyumbani kwake ili awe anamsomea vitabu na kwasababu hiyo wakatengeneza ukaribu sana kiasi cha kijana Craig kuwa huru kumweleza Mr. Harrigan maisha yake binafsi, ikiwemo namna anavyoonewa shuleni, huku naye mzee huyo akimpa ushauri wa hapa na pale. Japo Craig alikuwa anafanya kazi hii ya kumsomea mzee kwa ajili ya malipo tu lakini baadae alijikuta kazi hii ndo' kampani yake kubwa maishani.

Mahusiano haya hayadumu muda mrefu, Mr. Harrigan anafariki. Craig anaumia sana kumpoteza rafiki wa karibu, kwa kuonyesha mapenzi yake kwa marehemu huyu basi anahakikisha zawadi yake ya simu alomnunulia anazikwa nayo.

Maisha yanabadilika kwa Craig, hana tena wa kumwambia mambo yake kama hapo awali. Mambo yanapomzidi kifuani, anaona atumie simu yake kuwasiliana na Mr Harrigan, si kwamba marehemu huyo atamsaidia kwasababu ni wazi tayari ameshakufa bali tu kijana huyu apate mahala pa kushushia mzigo wake.

Ajabu ni kwamba, Craig anapata majibu toka kwa marehemu Mr. Harrigan! Anastaajabu, anamwambia baba yake lakini hakuna anayemwelewa. Hata naye hakulipa uzito jambo hili.

Mambo yanakuja kuwa mazito zaidi pale Craig anapokuja kuongea na simu kuhusu uonevu anaofanyiwa shuleni, anachukulia swala la kawaida tu ila baadae anastaajabu kusikia bwana aliyemfanyia uonevu amepata ajali mbaya na kufariki!

Sasa Craig anaanza kuamini simu ya Mr. Harrigan si ya kawaida! Pia anapata hamu kali ya kujua zaidi maisha ya Mr. Harrigan alipokuwa hai, alikuwa ni mtu wa namna gani? Na je, waliowahi kumfanyia kazi wanamjua vipi bwana huyo?

Craig atafikia wapi kwenye hili?

Zama ndani!
images(4).jpg
 
Kaka, hakikisha, kwa namna yoyote ile, unaitazama hii! Imetoka kwa fundi aliyetengeneza US na GET OUT, bwana Jordan Peele.View attachment 2429223
Ok ngoja nijaribu kukuamini kwa hii tu nione kama kweli wanasayansi wamefanya yao...

Maana movie zinazohusu makosa ya kisayansi ni movie zangu pendwa haswa.......na kiuhalisi ni current issues (Scientific warfare)...kwa dunia ya sasa physical battle ni Africa tu
 
Back
Top Bottom