Jiepushe kurudiana na mpenzi wako zamani

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
I greet you all members in the name of JF,

Mapenzi/Mahusiano ni kama chuo/darasa, unapata mengi ya kujifunza toka
kwa mwenzako uliyenaye kwenye huo uhusiano. Mnaweza achana kwa makubaliano mazuri au kwa vurugu na dharau pamoja na kejeli kibao.

Hutokea mara nyingi mmoja wenu akarudi kama rafiki mwema aliyebadilika na kuhitaji nafasi ya pili ya mahusiano/mapenzi tafadhali usikurupuke kuingia katika mtego huo.

Unaweza kuhatarisha afya yako bila kujua.Baadhi ya wanaorejea na kuomba mrudiane wanakuwa na agenda za siri kama hizi.

1) Kule alikoenda aliyempata kashindwa kufikia vigezo vya ubora ulivyonavyo wewe ndo maana karudi mazingira yamemrudisha kwako vinginevyo asingerudi, sio upendo.

2) Anaweza kuwa na kinyongo moyoni nawewe kwa namna uliyomuacha sasa anataka kulipa kisasi kwa gharama yoyote,sio lazima atoe uhai wako katika hili.

3) Maisha yamemshinda yamekuwa ni kinyume na matarajio yake, angefanikiwa asingerudi, akirudi huyu lazima akufilisi akirudi kwako.

4) Wako wanaorudi kujaribu hana nia ya dhati,lolote litakalokuwa liwe,mtu wa aina hii, ataishia kukupotezea mda na raslimali zako.

5) Wako wanaorudi huku bado wanamahusiano waliyoyaanzisha baada ya kuachana nawewe awali utashangaa mwanamke/mwanaume ana stress za mapenzi mda mwingi chanzo kumbe ni kule alikotoka bado yuko naye.

Ni hayo kwa leo, bado maamuzi ni yako kwani maswala ya mapenzi ni vigumu kumwamulia mtu, unampa ushauri kutokana na uzoefu ambao nao hauna kanuni, unatofautiana baina ya mtu na mtu.
 
Umesema vema mkuu ila kuna usemi unasema huwezi jua thamani ya kitu ukiwa nacho mpaka kikutoke, kufuatia usemi huo yawezekana mpenzi wako ulikuwa nae akahisi akiachana na wewe ataienjoy akaachana na wewe akaenda huko nje akagundua alivyokuwa na wewe alikuwa paradiso ndogo mpenzi kama huyu akirudi atakuwa ameshapata fundisho na atakuheshimu mpaka mwisho wa maisha.
 
Kuna demu nisharudiana nae zaidi ya mara tano na kila mara hatumalizi miezi miwili lazima tuachane...

Basi nitajaribu kufata ushauri wako...

Ila sijui kama nitaweza
mkuu sio wewe tu,hayo ni maumivu ya kimyakimya watu yanatupata! kuna demu pia nilimuacha mda,akarudi kaniambia kote alikopita hajapata wa kumridhisha moyo wake kama mimi anaomba tusahau yaliyopita turudiane nikamwambia sawa ila nikawa namchunguza na sikuwahi enda naye uwanjani tena haijakaa miezi mitatu tukazinguana hiyo hali na huyo demu imejirudia mara tatu mara ya mwisho nilimblock whats up na kumfuta fb alimaindi kichizi lakini namuepuka wanakuwa wamedata wengine hawajui wanachokitaka
 
Back
Top Bottom