Jielewe, kipato chako kinakusaidia nini?

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,483
5,799
ASSET AND LIABILITY
Asset
ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

Liability ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri, hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.
Matajiri wote wananunua Assets, lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kua ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza una Asset gani unayomiliki atakutajia vitu kama nyumba, gari, simu, laptop, duka.
Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa, lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba, kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana maana haikuingizii hata mia, badala yake inakutolea pesa, utalipa umeme, maji, ukarabati na marekebisho ya vitasa, taa, furniture n.k, hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini kama nyumba umepangisha, hiyo ni Asset. Gari, kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa, itahitaji mafuta, service na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi, ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.
Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchart,hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia,maana siku umelifunga huingizi chochote,matumizi yoote unategemea dukani,badala ya duka kukupa faida,unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiriwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV, radio, simu kubwa, gari, fridge, nguo, viatu badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine, mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara watatatua matatizo yao, badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara(Income) ukiongezeka,matumizi(Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa dalasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato(Income) na kupunguza upande wa matumizi(Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities,wananunua Luxuries kama gari,tv ,sm kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida,hivyo faida ndio inanunua magari,nyumba,TV nnk, ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili,lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka.
Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

Wealth is a person’s ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today,how long could you survive?
Maana yake,kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato,una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani??
Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.

Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities, na pia ujiulize are you Wealth or not?
 
Ngoja tuendelee kupambana kutafuta assets , ingawa liabilities ni sehem ya maisha pia , sema hazitakiwi kuzidi
 
Umeongea vitu vya msingi lakini pia sio vizuri kuchukua kila kitu kama kilivyo.
Watu wanatofautiana sana hali kadhalika vyanzo na shughuli zao za kutafuta kipato zinatofautiana pia.

Hata kama suo sahihi mara zote, ukiwa na kwako inakupunguzia gharama A kulipa kodi, kwa upande wangu nyumba ya kuishi ni asset.

Gari binafsi ikiwa inakurahisishia shughuli zako za kukuingizia kipato na inakupa wepesi, ni asset pia.

Shida ni pale unakopa au kujiingiza kwenye madeni ili upate hivyo vitu ili kujiweka kundi na watu flani, una miliki gari ambayo hauwezi hata kuihudumia mafuta achilia mbali kuifanyia service.

Hiyo ni hasara.
 
Sawa ina mana pasi ya kupiga bguo inyooke nayo nisiwe nayo mana inakula umeme.friji abayo inasaidia kutunza vitu visiharibike kwa muda mrefu nayo ni liabilitieS mana inakula umeme.na ghamu yotee hio ni kama utaishi miaka 150 mbele
 
Kama nyumba ni liability unanishauri niuze nyumba yangu nikapangishe ili niondokane na hii liability?

Kama gari ni liability unanishauri niuze gari yangu niwenatumia public transport ili niondokane na hii liability?

Tofauti ya liabilities na basic needs ni nn?
 
Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu kama,nyumba,gari,simu,laptop, duka.
Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa,lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.
Aiseee noma Sana ....
 
What if I’m getting salary and saving 75% of it? And then investing it on treasury bonds or fixed account...where by from the later I can accrue 4 million....where at the end of the day if I want my money back I have an assurance to that....is that an asset or liability?
 
Back
Top Bottom