Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,144
Mhhhh wamependeza sana sana kwanza napenda kuwapa hongera baada ya hapo nimeshangaa mmejitahidi kuelzea vyakula mlivyokuta na picha za menu...mbona hamjawahi kupiga picha zile pweza za feri jamani na umuhimu wake katika jamii hamuoni mnatangaza soko la watu wakati kwenu wanakimbia....haya Zanzibar nako ndio hivyo wamarekani no.
Asalaleh!
Mwisho nawapongeza maisha na raha wajipe jamani msisubiri kupewa na kampuni ama mashirika
=====================
SAFARI YA KUELEKEA JELA ALIPOFUNGWA MWANAMAPINDUZI WA KWELI COMRADE MADIBA
Vivutio mbali mbali ambavyo vipo Waterfront ni pamoja na huyu mtu wa Gold ambae akisimama hatingishiki unaweza ukadhani ni sanamu ila ukimtupia pesa kwenye ki box kidogo kilichopo pembeni ndio ana swing kama ishara ya kushukuru
Kuna duka linalouza suvenir mbali mbali za Mandela zikiwemo tshirts, keyholders, magnet za kwenye fridge n.k mi nilikamata ya kwangu...size zote hazikunitosha ikabidi ninunue ya size ya watoto wa miaka 7-8 ndio ikanikaa...kazi kweli kweli
Mlango wa kuingilia sehemu ya kupandia Boat kuelekea Robben Island,(Nelson Mandela GetAway)
Huku nako kumbe mpaka kuna cha kiswahili nimepanga nitarudi kukila
Manka na Mtu wa dhahabu
Manka na mtu wa silver
Berna na Gardner kuelekea katika boat (Sikululekhile)
Mkiwa nje ya boat kabla ya kupanda mnapigwa picha wakati wa kurudi mnazichukua kwa kumbu kumbu, kama bongo vile
Tuko kwenye foleni kabla ya kuingia kwenye boat, sio unampita tu mwenzio ukikuta amesimama...na utake kuhudumiwa wewe kwanza huku wa kila sehemu unapanga foleni
Sio lazima kungoja wadosi wakuuzie, kama wanazingua sio mbaya kwenda front mwenyewe..African Marimba Band wanapiga na kuuza Cd's zao wenyewe hapo hapo, pia watu wanaopendezewa wanawapa chochote kila wanapopita
Duka la Suvenir za Comrade Madiba, ...wadau wachache nimewachukulia zawadi nikirudi tu nawacheki msikonde
Lango kuu la kuingia jela alipofungwa Comrade Nelson Mandela miaka 18 kabla ya kuhamishiwa magereza mengine mawili tofauti ambapo alikamilisha miaka 27.
Gereza la Posmo alifungwa miaka 7 na Gereza la Paarl alifungwa miaka 2
Moja kati ya watu waliokuwa Tour guide wetu ambae alifungwa miaka 2 katika gereza la Robben Island na sasa ndio anawaelezea watalii vizuri kuhusu yaliokuwa yanajiri humo ndani...
Aliwahi kuchapwa viboko mwili mzima. Lakini alipojaribu kuwaonyesha wahusika wakuu na doctors kuwa ameumizwa sana hawakujali na walikuwa wanamfukuza na kumuita muongo, na kudai kuwa ni stress tu za yeye kutokulala usiku, huyu guide ni moja kati ya wanaoitwa coloured (halfcast)
Alipona kwa kudra za mwenyezi MUNGU
Kumbukeni gereza hili walikuwa wanafungwa watu weusi, Asians na Coloured tuuu, hakuna mzungu aliekuwa anafungwa humu.
Pia wanawake walikuwa hawafungwi humu
Ubaguzi ulikuwa wazi wazi, kabla Comrade hajaachiwa na kuibadili Afrika Kusini
Moja ya Picha za kumbukumbu zilizopo kwenye kisiwa hicho, ya wafungwa waliokuwa wakiingizwa huku wamefungwa minyororo miguuni na mikononi tayari kwa mateso.
Mkono wa kulia katikati ni askari weusi waliokuwa wanapewa mikuki na rungu tu kwaajili ya kuwalinda weusi wenzao wasitoroke,
Wakati askari wa kizungu walikuwa na bunduki,
Askari mweusi hakuruhusiwa kuwa na bunduki
Tukiwa kwenye Bus kuelekea gereza kuu hii ni moja ya barabara za ndani ya gereza hilo
Kulikuwa hakuna vitanda gerezani humo wafungwa wetu walikuwa wanalala kwenye matandiko kama haya, na hapo juu pichani ni Tour Guide mwingine akituelezea habari zote kuhusiana na gereza hilo
Menu ya chakula ilikuwa kama hivi, Coloured na Asians walikuwa wanapewa chakula cha afadhali, na Chakula cha wabantu (watu weusi) kilikuwa kibaya kuliko vya wote.
Soma Menu vizuri utaona, upande wa kushoto ndio chakula cha Coloured na Asians na upande wa kulia ni chakula cha mtu mweusi, gerezani humo
Watalii mbali mbali hufika gerezani hapo kutembelea, na gereza limefungwa kuwa kama gereza limebaki kuwa kivutio cha kitalii ambacho kinaingizia South Africa pesa za kuisaidia nchi.
Hiki ndicho chumba alichofungiwa Comrade Nelson Madiba Mandela (Our Miracle Father)
Tanzania pia tulikuwa nae wa kujivunia Our Miracle father J.K Nyerere
Hapa ndipo alipokuwa akijiegesha, maana humu huwezi kuita ni sehemu ya kulala wala kujipumzisha, unaweza ukalia mwanzo mpaka mwisho wa safari unapokwenda kisiwani humo.
Ukielezewa story ya kusikitisha kama hii
Captain akishuhudia jela aliofungwa Madiba miaka 18, kabla ya kuhamishiwa jela zingine alizokamilisha miaka 27
Berna, Flower la Venture ndani ya gereza la Mandela
Manka ndani ya Gereza alilofungwa Madiba
Mlango mkuu wa kutokea ukiwa umeachiwa huru, na picha ya gereza kwa nje kama linavoonekana
Tour Guide aliekuwa akituhadithia yaliojiri, yeye alifungwa miaka 7 ndani ya gereza hilo. Mwanaharakati wa mapinduzi, ambae alibambikiwa kosa la ugaidi lakini hivi leo yuko huru na anatuelezea makaburu walivowatesa
Watalii mbali mbali tulioongozana nao, wakipiga picha gereza la Komandoo wa Afrika, COMRADE NELSON MADIBA MANDELA.
Miaka 27 gerezani, katoka akiwa hai na kawasamehe wote waliomtesa na kumfunga?????????
Mungu nisaidie niwe na roho ya hivo...eeehhhhhhhhh!!
Na hakutaka kufukuza wazungu kaamua taifa liwe la amani kwani binadamu wote ni sawa, Wazungu na weusi wote ni sawa hapa Afrika ya Kusini na hii yote ni kwasababu ya Mandela...we love you tata Madiba
Berna na Manka nje ya gereza