Jichunguze hapa kama wewe au mtoto wako mnatatizo la Dyslexia

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
10,132
2,000
Basi Natumaini ulikua na Dyslexia na ADHD maana asilimia kubwa ya watu wenye dyslexia hua na tatizo hili la ADHD. Maybe ulikua na Dyslexia ila ukaweza kui-overcome kutokana na mazingira uliyopo na Experience.
Kuhusu Autodidact soma hapa..

Nami ni msikilizaji mzuri mtu akiwa anaongea mambo ya kuelimisha hasa kwenye nyumba za ibada. Sometimes hizi childhood trauma ndio hutupelekea kupata shida mbalimbali so inawezekana wewe yako uliweza kuitatua bila kujua
Kabisa mkuu sasa hivi nina mkakati wa kutaka kuwasomesha watoto wangu ama kuwasimulia visa ambavyo vitawafanya wawe na jwezo wa kusikiliza
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
10,132
2,000
Basi Natumaini ulikua na Dyslexia na ADHD maana asilimia kubwa ya watu wenye dyslexia hua na tatizo hili la ADHD. Maybe ulikua na Dyslexia ila ukaweza kui-overcome kutokana na mazingira uliyopo na Experience.
Kuhusu Autodidact soma hapa..

Nami ni msikilizaji mzuri mtu akiwa anaongea mambo ya kuelimisha hasa kwenye nyumba za ibada. Sometimes hizi childhood trauma ndio hutupelekea kupata shida mbalimbali so inawezekana wewe yako uliweza kuitatua bila kujua
Asante mkuu nitapitia hizi nyuzi
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
31,214
2,000
Kabisa mkuu sasa hivi nina mkakati wa kutaka kuwasomesha watoto wangu ama kuwasimulia visa ambavyo vitawafanya wawe na jwezo wa kusikiliza
Ili kama nikijaliwa watoto niweze kuealea vyema kwa kuanalyse tabaia na matendo yao ka kudeal nao psychologically ndio kulinipelekea nipende maswala ya falsafa na Saikolojia. Ndio maana napenda pia kuandika Psychology based topics humu ili watu wajifunze hayo machache
Asante mkuu nitapitia hizi nyuzi
Much obliged Sir. My pleasure ✌️
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
10,132
2,000
Ili kama nikijaliwa watoto niweze kuealea vyema kwa kuanalyse tabaia na matendo yao ka kudeal nao psychologically ndio kulinipelekea nipende maswala ya falsafa na Saikolojia. Ndio maana napenda pia kuandika Psychology based topics humu ili watu wajifunze hayo machache

Much obliged Sir. My pleasure ✌️
Kabisa mkuu,nataka watoto wangu mpaka kufikia miaka 7 wawe na uwezo mkub2a sana wa kupambanua mambo na kujua solution ya matatizo yao ya kihisia.
 

olele

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
1,274
2,000
y’all.....
Kutokana na uelewa na muamko hafifu wa elimu ya malezi ya watoto from prenatal to postnatal (Psychology) kuna mambo hua yanawakumba watoto na wazazi bila kuelewa wanachukulia ni swala la kawaida mtoto kua hivo. Wengine wanaweza ihusisha hali Fulani aliyonayo mtoto na maswala ya nguvu za giza kumbe sio kweli, ni mtoto anakua anahitaji uangalizi na huduma ya kiasaikolojia ili kuondoa hali yoyote isiyo ya kawaida aliyonayo mtoto.

There’s this person I know mtu mzima tu ukiongea nae ana tatizo la kusahau maneno, kuna yale maneno common tunayotumia siku zote kwenye maongezi yeye inakua shida kwake kuyajua mpaka anaulizia labda kufanya kitu falani wanaitaje? Unaweza kujua anajifanyisha au ndio mapozi yake ya mazungumzo but ndio yuko hivyo hua hajui maneno so ukizungumza nae inatakiwa umchukulie kama alivyo…Yeye binafsi anaona ni jambo la kawaida kwamba ndio alivyo lakini in reality ana tatizo ambalo kwa umri aliofikia natumaini haliponi tena.

Nikiwa shule ya msingi japo sikufanikiwa kusoma chekechea na niliomea shule za st kayumba toka kwa walimu wa UPE ila ndani ya miezi 6 ya kwanza nilikua nishajua kusoma vizuri tu na nalikua nawaelekeza wenzangu jinsi yakusoma na kuunga maneno. Niliwahi zaidi na mpaka leo nina speed kubwa sana kwenye kusoma vitu, shida yangu ilikua kwenye kuandika tu. Nilichelewa kujua kuandika maneno kwa ufasaha na nina muandiko mbayaaaa sana bora sasa kidogo umebadirika, nilikua naandika minyoo minyoo mwandiko wangu nadhani ni mimi na mwalimu ndio tuliweza kuusoma ……nimeweza kujua kuandika vizuri nikiwa darasa la 4 baada ya kupigwa sana sana na mwalimu wa Kiswahili hopefully mwafahamu jinsi walimu wa 90s walivyokua wanatandika bakora. Mpaka leo hii naandika hapa namba 2,3,8,5 na herufi g, y,r k siwezi kuzinadika vyema. Lakini kwanini mtu huyo ashindwe kufahamu maneno ya kawaida tu yanayotumika kila sikua na mimi kwanini nishindwe kuandika vyema?

Dyslexia ni tatizo ambapo muhusika mwenye tatizo hili anakua inamuwea vigumu kuandika na kusoma ajili kushindwa kutambua sauti za matamshi, Wernickes’s area ni sehemu inayopaktikana kwenye posterior superior temporal lobe ambayo ipo kwenye ubongo wa mbele. Katika eneo hilo ndio kunahusika na kuchakata matamshi kama yameandikwa au yametamkwa, hivyo basi Dyslexia hushambulia eneo hili linalohuika na kuchakata lugha.

Kwakawaida dalili za huu ugonjwa hua ni ngumu kuugundua kabla ya mtoto kuanza shule lakini kuna baadhi ya viashiria ukiviona kwa mtoto basi vitakuashiria kwamba mwanao pindi akifianza shule anaweza kua na tatizo hili. Zifuatazo ni dalili za ugonjwa huu

Kabla ya kuanza shule
Hivi ni viashiaria amabavyo mwanao anaweza kuvionyesha kabla ya kuanza shule ambavyo vitakuashiria kwamba mwanao akianza shule atakua na dyslexia.
 • Kuchelewa kuanza kuongea​
 • Kujifunza maneno mapya taratibu​
 • Kushindwa kukumbuka kwamba hii ni namba ngapi au herufi gani, kushindwa kutambua rangi​
 • Kushindwa kuunda maneno kwa usahihi pindi anapotamka au kuchanganya maneno ambayo yanafanana katika matamshi​

Akianza shule
Hizi ni dalili ambazo mwanao atazionyesha pindi atakapoanza shule​
 • Kushindwa kutambua na kuelewa kile anachosikia​
 • Kusoma chini ya kiwango alichotarajiwa​
 • Kushindwa kutambua neno sahihi au kuunda jibu la kitu anachotaka kujibu/kutamka​
 • Kushindwa kukumbuka mfuatano wa vitu. Mfano mtoto anashindwa kukukumbuka kua baada ya 5 inafuata 6 au baada P inafuata Q​
 • Kushindwa kuona au kusikia ufanano na utofauti uliopo kati ya maneno na herufi (kama neno “mama” yeye atalitaja herufi moja moja na kama ni herufi "m" yeye atalitaja mama)​
 • Kuchukua muda mrefu kumaliza kazi ambayo inahusiana na kuandika au kusoma​
 • Kushindwa kutaja spelling /herufi za maneno​
 • Kukwepa kufanya kazi zinazohusiana na usomaji​

Kwa vijana na watu wazima.
Kijana au mtu mzima mwenye ugonjwa huu hua na sifa zifuatazo au huonyesha dalili zifuatazo​
 • Kushindwa kusoma vzuri hasa kwa sauti​
 • Kusoma au kundika taratibu​
 • Kushindwa kutaja herufi za maneno/spelling​
 • Kukwepa kufanya kazi zinazohusiana na usomaji​
 • Kutamka maneno vibaya au kushindwa kutoa maneno pindi anapoongea​
 • Kushindwa kuelewa matani, au kuelewa maneno ambayo maana yake imefichwa hasa nahau.​
 • Kutumia muda mrefu kusoma au kundika​
 • Hua hawawezi kufupisha story pindi anapohadithia jambo​
 • Inakua ngumu kwao kujifunza lugha mpya​
 • Kushindwa kukumbuka yale waliyoyasoma​
 • Kushindwa ku-Solve maswali ya mafumbo kwenye hisabati​

Hivi maana halisi ya neno Disorder ni ugonjwa au tatizo? Maana mara nyingi kitu kikiitwa Disorder hua hakina tiba ya dawa , mara nyingi hutibiwa kwa kuonana na wataalam wa saikolojia. Hili tatizo la Dyslexia hua hauna tiba. Kwa wenzetu wanakua na program maalumu ya kuwaelekeza vyema kutokana na hali yao na huku kwetu hua kuna program yao maalum ya kutandika bakora wanafunzi wasioweza kusoma vyema na kuandika mnyoo/wakama bata kapita kwenye daftar kama mimi.

Kumchapa mtoto kwamba haujui kuandika vyema bila kujua cahnzo cha yeye kuandika hivyo kunamfanya mtoto azidishe hofu ..hofu inampelekea ashindwe zaidi. Acheni kuwazonga watoto zenu kua wana”hati” mbaya bila kujua sababu husika, kaeni nna watoto zenu muwachunguze matatizo waliyonayo bila kuwafokea na kuwachapa. Hili tatizo hua linarithishwa au anaweza kulipata pindi akipata ajali ya kichwa. Ukosefu wa eleimu ya saikolojia kwa wazazi wetu umetufanya sisi watoto zao tunaoelekea kua wazazi kuishi kwa shida kiakili kutokana na Trauma tulizopata kutoka kwa wazazi na walimu. Natumaini watoto zetu watalea vizuri watoto wao kadri ya misingi ya malezi kisaikolojia inavyoagiza ili kuepusah trauma kwa watoto zao kama tulivyozipata sisi wazazi.

Je kuna yeyote aliyegundua kama ana tatizo hili au mwanae?? Shea nasi jinsi unavyokua tujifunze. We scare because we care

-Vinjii
Umeshatazama movie ya Taare Zameen Par ya Amir Khan..??

yule dogo ndio ana ugonjwa huu unaouzungumzia??
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
31,214
2,000
Kabisa mkuu,nataka watoto wangu mpaka kufikia miaka 7 wawe na uwezo mkub2a sana wa kupambanua mambo na kujua solution ya matatizo yao ya kihisia.
Naam, pia usisahau kiroho maana Saikolojia inaendana na mambo ya kiroho. Unapomuandaa mtoto kimalezi bora ya Saikolojia usisahau na Kiroho pia. Ni muhimu
 

olele

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
1,274
2,000
Naifahamu ila sijawahi kuitazama. Niliwahi kusoma plot yake tu Coz hua Napenda kazi za Aamir Khan
nzuri sana mkuu itazame, kama unapenda kujifunza kuhusu malezi ya watoto..
nimefuatilia yule dogo alikua na huo ugonjwa na hakuna mtu alikua anajua, kuanzia wazazi hadi walimu.. dogo alipata shida kweli, mwl wake aliyekua na huo ugonjwa ndio alikuja kumgundua

nzuri sana
 

Baljurashi

JF-Expert Member
Dec 30, 2017
208
250
Umeshatazama movie ya Taare Zameen Par ya Amir Khan..??

yule dogo ndio ana ugonjwa huu unaouzungumzia??
Mkuu, wakati nausoma huu uzi hiyo Movie ya Kihindi imenijia kichwani. Nataka kuizungumzia hapa (japo niliisahau jina) ndio nakutana na Comment yako hii. Hiyo Movie niliiona miaka kadhaa iliyopita. Ni nzuri.
 

Jomy

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
550
500
Hapa ni shule tosha, nina mtoto wangu sasa hv miaka mitatu na miezi saba lakini hajui kuongea vizuri lakini ukimwambia chochote anakuelewa ila kujibu dah mtihani. Shulen ni yeye peke yake hajui kuongea kati ya wenye umri wake yaan ata sielewi atakuwa hivi mpaka lini, ukimuuliza kitu na yeye anarudia ulichosema japo yale common anaelewa kwa mbali
 

AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,523
2,000
Kuna msemo unasema Never understemate the power of your mind, Trust your mind it knows the way. Kila kitu chaanzia akilini ukiidhibiti akili basi na mwili unafuata kadri ya udhibiti wako. Ndio maana kuna mada niliwahi kuandika jinsi mtu unavyoweza kujitibu kwa kutumia akili yako tu.
Mkuu naweza pata link ya hii mada yako ya kujifunza kwa kutumia akili yako?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom