Jicho langu la Kiufundi na Tahadhari kwa Simba SC kuelekea katika ' Desicive Game ' yake na AS Vita Club tarehe 2 April, 2021

Hivi nyie utopolo mtaendelea kututisha Simba kwa riwaya katika media?

Kama club bingwa Afrika amefungwa,unaanzaje kututisha na wengine ambao ni size yetu tu?

Hivi hamjui nao wanatuogopa?
Hata sijui nikujibu nini..

Kipi kimekufanya uhisi mimi ni yanga, sasa tusiseme ukweli
 
Mkuu, jamaa kaongea points za ukweli kuhusu chama, wakati mwingine anazingua sana kwa kupozesha mashambulizi, aambiwe ukweli. Ni kheri ukosolowe ili uyaone mapungufu yako na kuyafanyia kazi.
Mpira ni mchezo wa wazi, watu wanaona mkuu. Chama angekuwa na maamuzi km ya condeboy, team ingekuwa inapata magoli mengi sana.

Best,
Kejuu
 
Umenena ukweli mtupu

Kuna kipindi nilibishana na mpuuzi moja kibanda-umiza,ila game ya merreikh kutoka nao sare, Kutokuwafunga wale vibonde kule kwao, bado kunatuweka wakat mgumu...
Kibonde kwenye group akifungwa na wenzio woote kisha ww usimfunge ana kudhurumu mahesabu

Ile mechi ilikuwa muhimu saana, kwanza ingeamua sisi kufuzu kwa kushika usukani, jambo ambalo ni zuri zaidi, hatua inayofata tungekutana na maji yetu, ila tukifuzu watu wa pili, robo fainali tutaangukia kwa mamelodi, esperence ama wydad casablanca aisee.. Hawa sio watu wazuri kabisa..

Pili mpaka sasa hatujafuzu, tutegemee mechi ngumu mnoo kutoka kwa as vita, vita watakuja kichwa, miguu, mikono, kila kitu yaani wazima wazima, hawana cha kupoteza na mpira hauna adabu unaweza ukapigwa kimoja, ikawa chomoa, chomoa na ww.

Yote kwa yote kila la kheri chama langu
Nimewaangalia sana hao akina sundown na wydad (msuva et al). Uchezaji & level yao haitofautiani na Simba
 
Back
Top Bottom