Jicho la Tatu ziara ya Mteule Urais CCM Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Naam, ni wakati mwengine tunakupatia taarifa.
Jana tarehe 15 Julai, 2020 kulikuwa na mapokezi ya Mteule wa urais wa CCM Zanzibar dkt Hussein Mwinyi.

Ziara ilifana na iliandaliwa vya kutosha. Tutatoa tathmini fupi kutokana na taarifa zetu.

Shabaha na kupima upepo.
Ziara si tu kwamba ilenga kumtambulisha mgombea, lakini ilijaribu kuwavuta mahasimu wote waliokuwemo kwenye mchakato ili kuweka mazingira sawa. Itoshe tu kwamba kuna kundi la CCM asili Zanzibar hawakuridhika na minongono ipo.

Jana ilikuwa ni kipima upepo cha CCM na mwelekeo wake wa kampeni. Taarifa tulizonazo CCM ilitumia nyenzo zake zote za uhamasishaji na waungaji mkono wake. Magari yalikodiwa na kupelekwa mashamba na mjini, Vilitumika vikosi vyote vya SMZ wakiwemo valantia, KMKM, Magereza, JKU hata wanafunzi waliokuweko mafunzo wote walivalishwa uniform maalumu za kichama ili kunogesha mapokezi.

Vyombo vya dola vilishiriki kwa asilimia 100 kutoa ulinzi kwa mgombea wa CCM na ilikuwa na ziara rasmi yenye baraka za serikali.

Baadhi ya wafanyakazi na maofisa mbali mbali walishiriki kwa uratibu rasmi wa makada ndani ya vitengo na shughuli za serikali baadhi ya ofisi zilisimama kwa muda

JICHO LA TATU.

Kujaribu kuondowa kiwingu kwa kuwalazimisha mahasimu wote kuhudhuria. Taarifa zipo za baadhi ya watia nia kununa na kutoridhishwa

CCM bila kutumia vyombo vya dola na vikosi mbali mbali na nyenzo za serikali shughuli zao hazinogi. Wananchi hawatoi sapoti ya kutosha na kujitolea bila kuwezeshwa.

Hutuba za Rais Dk Shein za Kulazimika kusemea Uzawa wa Dkt Hussein Mwinyi kwamba ni mzawa wa Zanzibar , technically CCM imebaini uwepo wa ufa na inajaribu kuuziba.

Ziara ya Mteule itatumika kama kiashiria cha kupanga mikakati ya kukabiliana na nyufa mbali mbali.

Ziara ya Jana ni kama CCM imeanza kampeni Zanzibar. Wananchi wanahoji jee wapinzani wataruhusiwa na wao na watapata ulinzi na ushirikiano?


Ni hayo tu kwa leo


Kishada
 
Back
Top Bottom