Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Rais ni mamlaka ya kwanza kinchi na kiserikali. Wapo hata wanaosema kuwa Rais ni raia nambari moja wa nchi. Kiutawala na kinchi,Rais si mtu wa kawaida. Ni wa kipekee kwa maelezo ya namna tofautitofauti.
Pale ambapo Rais anashiriki au kushirikishwa katika jambo fulani,hasa katika kutekeleza sheria au agizo,ushiriki huo ni kielelezo cha umuhimu na uzito wa zoezi hilo. Natoa mifano miwili. Wa kwanza ni kuhusu agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda juu ya zoezi la kuhakiki silaha.
Rais alijitokeza na kushiriki zoezi hilo. Kimsingi,zoezi kuanzia hapo likawa madhubuti,muhimu na lenye uzito mkubwa. Mfano wa pili,ni kuhusu nia na matarajio ya kukata kodi kwenye mafao ya kustaafu ya Rais. Ilivyo sasa,mafao ya kustaafu ya Rais,Makamu wa Rais,Waziri Mkuu,Mawaziri,Wakuu wa mikoa na wilaya,Spika,Naibu Spika na Wabunge hayakatwi kodi.
Sasa,Waziri wa Fedha na Mipango,Mhe. Dr. Philip Mpango amesema wote hao waliokuwa wakiachwa kando,mafao yao ya kustaafu yatakatwa kodi. Rais anahusishwa sasa kulipa kodi. It is a serious business. Kodi hazitakwepeka kirahisi. Kutakuwa na ukali kwelikweli katika kukusanya na kuwashughulikia wakwepakodi. Hakika,Rais anapohusika panakuwa pa utofauti. Na mishahara yao ihusishwe pia.