Jicho la tatu: Michuano ya CAF itavurugika? Kaizer Chiefs nayo yapigwa stop kuingia Morroco

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,490
215,330
Hii ni kwa sababu CAF yenyewe haijajipanga kabisa kuhusu Ugonjwa wa Corona.

Ikumbukwe kwamba kila nchi ina sera yake kuhusu namna ya kujilinda na Corona, wengine wanapiga nyungu za malimao na Tangawizi na wengine wanafuata muongozo wa WHO.

Baadhi ya nchi haziruhusu kabisa wageni, huku nyingine zikiwaruhusu na kuwaweka karantini, lakini ziko nchi nyingine kama Tanzania ambazo kwao wageni wanaingia bila masharti yoyote.

Kitendo cha baadhi ya Timu kuzuiliwa kuingia nchi zingine kunafanya ugumu wa mashindano haya kuendelea kufanyika, kwa mfano Kaizer Chiefs ya South Afrika imenyimwa ruhusa ya kuingia nchini Morroco kupambana na Waydad Cassablanca. Hii ni kwa sababu sera ya nchi yao hairuhusu wageni kuingia nchini humo kibwege na makorona yao.
 
Wasituletee ubwege, wameshaona tuna moto tunapiga mtu mpaka kwake, ndio wavuruge mchezo, wanataka kutuletea mambo ya MKALI WA RHYMES.

Watupe tu kombe letu, kisha mengine watajuana wenyewe kwa wenyewe huko, sie tayari pointi 3 kibindoni.
 
Angalau hii habari itabalance.

Namungo kuzuiliwa Angola wazambuli walianza kuishushia lawama Tanzania kama nchi wakati Tanzania aijaleta Corona apa duniani.
 
Match tata walete neutral ground Tz, match itapigwa watatuletea pesa za hotel na michango mingine, then wataondoka zao...
Hii ni fursa , serikali na TFF changamkieni pesa za bure hizi
 
Sasa neutral gani itapokea wageni hawa magumashi, saa sita unapima Mabibo negative unapanda ndege kufika Angola unapima positive
Taratibu za CAF kwa kipind hiki cha Corona zinawapa mamlaka Home Team kuwapima Corona Away Team ndo maana Namungo wamekutwa watu watatu na Corona. Hata kipindi simba wameenda Zimbabwe, walisema kina Chama na Miquison walikua na Corona. Hii inawezekana ni mbinu ya kuwatoa wachezaji tegemezi katika kikosi.

Sasa hivi CAF wamebadilisha utaratibu, watatumia maafisa wao kuwapima wachezaji Corona ili kuondokana na matatizo kama haya. Au watumie Neutral Ground kwa maana ya kwamba Hiyo Team itoke Angola na Namungo itoke hapa zikutane Mahali kama Sudan hivi alaf wapimwe na kuchezea kulekule
 
Morocco wanaakili nyingi kutuzidi...wanawathamini na kuwalinda raia wao...pongezi nyingi ziwaendee morocco country...wamatumbi tuendelee kujinadi kuwa "Tanzania hakuna corona" huku watu wake wakiangamia. Sifa inauwa!


I wish nikaishi Morocco mahala ambapo salama kabisa.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom