Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,888
- 143,986
Huu ni mtazamo wangu kuhusiana na hili swala.
Binafsi nilikuwa najiuliza maswali mengi juu ya nia hasa ya Spika kutaja jumla ya pesa alizolipwa Lissu kama mbunge tangu awe kwenye matibabu baada ya yeye kupigwa risasi na nikapata majibu mengi na jioni hii nimepata wazo huenda lengo ni kutaka wananchi waelewi ni fedha kiasi gani wabunge wanalipwa na kupitia reaction ya wananchi, basi watakuwa wamepata pa kuanzia.
Alafu ukiangali hata hapa JF utaona ni vijana wa Lumumba humu ndio wanaoonekana kuvalia njuga swala la ghrama utadhani Lissu ndio mbunge wa kwanza kulipwa kiasi hicho cha fedha akiwa nje ya Bunge kama mgonjwa.
Mpaka hapa naanza kupata wasiwasi kuwa huenda kuna agenda ya siri kwasababu Lissu hakuwa kulalamika kuwa halipiwi mshahara na stahiki zake zingine bali kilio chake siku zote kimekuwa ni Bunge kugharamia matibabu yake.
Tujipe muda wa kufuatulia jambo hili ila binafsi jioni hii nimepata hisia kuwa haya huenda ni maandalizi ya kutaka kupunguza stahiki za hawa waheshimiwa na ili ieleweke, ni lazima umma uelewe ni pesa kiasi gani waheshimiwa hawa wanalipwa.
Narudia, huu ni mtazamo wangu ambao unaweza kuwa sahihi au vinginevyo maana sioni logic ya spika kutaja jumla ya fedha Lissu alizolipwa wakati hata Lissu mwenyewe ameweka wazi kuwa haki zake hizo amekuwa akilipwa.
Tusubiri.