Jicho la tatu:Kutajwa hadharani kiwango cha malipo ya posho na mishahara aliyolipwa Lissu huenda ni mkakati wa kutaka kupunguza stahiki za wabunge

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Huu ni mtazamo wangu kuhusiana na hili swala.

Binafsi nilikuwa najiuliza maswali mengi juu ya nia hasa ya Spika kutaja jumla ya pesa alizolipwa Lissu kama mbunge tangu awe kwenye matibabu baada ya yeye kupigwa risasi na nikapata majibu mengi na jioni hii nimepata wazo huenda lengo ni kutaka wananchi waelewi ni fedha kiasi gani wabunge wanalipwa na kupitia reaction ya wananchi, basi watakuwa wamepata pa kuanzia.

Alafu ukiangali hata hapa JF utaona ni vijana wa Lumumba humu ndio wanaoonekana kuvalia njuga swala la ghrama utadhani Lissu ndio mbunge wa kwanza kulipwa kiasi hicho cha fedha akiwa nje ya Bunge kama mgonjwa.

Mpaka hapa naanza kupata wasiwasi kuwa huenda kuna agenda ya siri kwasababu Lissu hakuwa kulalamika kuwa halipiwi mshahara na stahiki zake zingine bali kilio chake siku zote kimekuwa ni Bunge kugharamia matibabu yake.

Tujipe muda wa kufuatulia jambo hili ila binafsi jioni hii nimepata hisia kuwa haya huenda ni maandalizi ya kutaka kupunguza stahiki za hawa waheshimiwa na ili ieleweke, ni lazima umma uelewe ni pesa kiasi gani waheshimiwa hawa wanalipwa.

Narudia, huu ni mtazamo wangu ambao unaweza kuwa sahihi au vinginevyo maana sioni logic ya spika kutaja jumla ya fedha Lissu alizolipwa wakati hata Lissu mwenyewe ameweka wazi kuwa haki zake hizo amekuwa akilipwa.

Tusubiri.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,324

Ni sawa kabisa wapunguziwe yaani wanalipana mahela utadhani Tanzania ni shamba la bibi!
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Unaona mbali, hapa kuna kitu kinachezwa behind the scene!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sitaki kuamini kama Spika alikuwa haoni hatari ya kuanika kiasi cha feha wabunge wanazolipwa bali naona huu unaweza kuwa ni mkakati utakaotekelezwa kuanzia 2020.

Na kama hali ni tete kama dalili zinavyoonyesha huku wafadhili wakisita kuchangia bajeti, basi ni lazima watafute namna ya kupunguza ghrama.
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,768
2,000
Hapo spika kashaahidiwa dau nono ili apitishe mswada!!
Lakini jew kama ni. Kupnguza maslahi si itajadiliwa bungeni ina maana wabunge watajinyonga wenyewe??
Au wanataka kuweka mswaada kua ukiumwa usilipiwe matibabu?
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Hapo spika kashaahidiwa dau nono ili apitishe mswada!!
Lakini jew kama ni. Kupnguza maslahi si itajadiliwa bungeni ina maana wabunge watajinyonga wenyewe??
Au wanataka kuweka mswaada kua ukiumwa usilipiwe matibabu?
Kwa ile sheria ya vyama vya siass walioipitisha jana, bwana mkubwa ana nini tena cha kuhofia?

Alafu hujui hilo likitokea kama nilivyowaza, huoni atakuwa amejipatia sifa kutoka kwa wadanganyika?
 
KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
763
1,000
Around 20m per month... kisha jiwe anatulaghai kuwa analipwa 9.5m. Wanasiasa wote wanastahili kupigwa risasi hadharani. Mishahara ya wanyonge walimu, manesi, nk haipandishwi. Wabunge DHAIFU, wanyonge wananyonywa mpaka tone la mwisho la damu kisha wabunge wanalipana 20m per month?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,996
2,000
Kama ndio mkakati basi Job nitamuunga mkono kwa kila jambo mana atakua amesikiliza kilio cha wengi.

Kwa kweli kwa mfumo tulio nao wa Chama kushila hatam na serikali yake bunge lekua ni sehemu ya kupoteza mapato ya serikali.

Tunatala maendeleo sio porojo za wabunge wagonga meza.

Mshahara wa mmbunge hautakiwi uzidi mil.2 tu. Wote tufunge mikanda.
Kila mbunge na diwana anapaswa kuwa na shughuli nyingine za kiongeza kipato chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom